Kapu la kuchangia wanaopatwa na magonjwa hatari, yanayohatarisha kuzima uhai wao.

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Binadamu wote ni ndugu, kwa sababu safari yetu ni moja.

Kumekuwa na changamoto nyingi za kiafya katika jamii zetu.

Kumekuwepo na watu kuugua muda mrefu, na kupelekea kuporomoka kwa uchumi kwa familia husika, na hatimaye kushindwa kumudu gharama za matibabu.

Ambayo hupelekea kwa mgonjwa kuugua vitu viwili; kupambania uhai wake, na wapi atapata fedha/msaada wa kugharamia uhai wake.

Mi nashauri, kuwepo na kapu la kusaidia jamii pale wanapokutana na hizi changamoto.

Sababu; wote ni safari ni moja, hakuna atakayeishi miaka yote.

Mfano:-watu 5,000,000 wakatoa 1000 tu; itakuwa sawa na shilingi. 5,000, 000,000/=

Kwa nini tushindwe, yaani mtu afe kwa kukosa laki mbili kweli!

Karibuni kwa mjadala.​
 
Kaka yawezekana kuchanga si shida ila shida ni kuwa ni nani hizo hela anapokea na anatunza nani ? Hapo ndiyo nabaki kusema Equation x tupe njia tuone inakuaje.
 
Mkuu, kama watu wataazimia, miongozo itakuwepo. Watu huwa wanasema ugonjwa huwa ni siri kati ya mgonjwa na daktari; lakini inapotokea mgonjwa kuweka ugonjwa wake hadharani; hapo jamii inatakiwa ifanye kitu
 
Bongo bwana unaweza ukafa kwa njaa lakini siku ya msiba wako watu wakala pilau na kusaza!

Ukiwaomba michongo/connection za hela hawakupi, ila siku ya kifo chako hela zinapatikana na sifa kedekede zitakujia ukiwa umeshalala futi 6
 
Huu sio utu, ni bora hata kwenye msiba wasije
 
Anaeshika pesa sasa ni nani
Ebu tuanzie hapa mkuu

Unakumbuka wahanga wa tetemeko pale bukoba, alietupiga yupo mbele za haki. Tuseme Amina[emoji120]
Itabidi kuwepo na umoja fulani, ambapo mapato na matumizi yanakuwa yapo wazi; ila msingi wa umoja huo uwe ni imani.
 
Back
Top Bottom