Karagosi kalewa tembo

Karagosi kalewa tembo

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
KARAGOSI KALEWA TEMBO

Naona kama jana vile.
Hata shule ya msingi bado.

Eid imefika na watoto wa mtaa mzima mchana baada ya kupiga pilau tunavishwa nguo zetu tayari kwa safari ya Mnazi Mmoja kwenye mapembea na karagosi.

Kote tutapita kwenye vibanda lakini banda letu lililokuwa likitufurahisha sana ni banda la karagosi.

Karagosi akichezeshwa ngoma na dansi na akicheza kwa juhudi na umahiri mkubwa huku nyimbo yake ikiimbwa, ''Karagosi kalewa tembo.''

Sisi watoto kwa furaha tunamwangalia huku tukipiga makelele na kuimba, 'Karagosi kalewa tembo.''

Hakika karagosi alikuwa amelewa na ndiyo sababu ya yeye kucheza ngoma ile na dansi.

Karagosi hajitambui ameshika kucheza nasi watoto tunamshangilia kwa mayowe na makelele na tukiimba pia kumtia mdadi.

Hakika ilikuwa kichekesho kisicho na mfano.

Sisi tulikuwa watoto na tulikuwa na haki na kila sababu ya kumpenda karagosi kwa kuwa akituchekesha na kutustarehesha.

Lakini mtu ambae jamii inamstahi akatoka nje ya nyumba yake mtaani akajifanya karagosi akaanza kucheza uwanjani kwa matarumbeta...

Watoto hawatacheka wala kushangilia, zaidi watashangaa kwani hilo ni jambo la ajabu kwao si la kawaida.

Mtu mzima anakuwa na staha yake na heshima.

Huyu ajitoae akili leo si alikuwa mwalimu wetu?

Watoto watajiuliza.

Watu wazima hawataweza kustahamili kuangalia kwani wataona wao ndiyo waliovuliwa nguo hadharani.

Bila shaka watageuza sura zao na pengine wajiondoe hapo warudi ndani majumbani mwao ili muradi wasiwe sehemu ya fedheha na aibu ile.

Screenshot_20220129-143555_Facebook.jpg

Screenshot_20220129-143925_Facebook.jpg
 
View attachment 2099571

View attachment 2099574
Natamani kuwa Kama wewe Ila nawaza nitakuaje? Ya Aziz nisaidie [emoji120][emoji120][emoji120]
 
Sasa huyo karagosi ni nani au tuseme huyu aliyemwiga karagosi akaamua kuvua nguo na kucheza uchi ni nani.

Natamani ningeweza kufumbua fumbo lako,
 
Umahiri kedekede wa fasihi. Sina nilichoambua, ninayo subra ikupendeze uning'amulie japo nipate welewa wa mada
 
Back
Top Bottom