Karanga zinafaa kuungwa?

Karanga zinafaa kuungwa?

TheChoji

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2009
Posts
5,771
Reaction score
17,849
Wakuu,

Kuna mtu amewahi kujaribu kuunga karanga kwa kitunguu na nazi kama unavyounga maharage akaona inakuaje ukila na wali?

Naona kama karanga ni laini na tamu kuliko maharage, njegere, choroko n.k Kama kuna aliewahi kujaribu anipe mrejesho..
 
Karanga kuna baadhi ya Mapishi wanatumia kuunga kama ilivyo NAZI.

Mara nyingi inakuwa MBOGA imeungwa kwa Karanga.

Au SAMAKI ameungwa kwa Karanga.

Au NYAMA pia inaungwa kwa Karanga
 
Karanga kuna baadhi ya Mapishi wanatumia kuunga kama ilivyo NAZI.

Mara nyingi inakuwa MBOGA imeungwa kwa Karanga.

Au SAMAKI ameungwa kwa Karanga.

Au NYAMA pia inaungwa kwa Karanga
Hapa nadhani unaongelea karanga za kusaga ambazo huongezwa kwenye mapishi kama unavyoweka nazi. Mimi nataka kujua kama karange zenyewe zinafaa kuungwa na kutumika kama mboga ya kulia wali, ugali nk kama maharage
 
Wakuu,
Kuna mtu amewahi kujaribu kuunga karanga kwa kitunguu na nazi kama unavyounga maharage akaona inakuaje ukila na wali? Naona kama karanga ni laini na tamu kuliko maharage, njegere, choroko n.k Kama kuna aliewahi kujaribu anipe mrejesho..
Mbona kawaida sana hiyo? Karanga unaweza kuunga na Ikiwa pia kiungio.

Uzuri wa karanga, unaweza kupika mbichi, kavu, za kusaga, kwa sukari, kwa chumvi. Kuunga, kuungwa. Kukaanga, kuchemsha, kuchoma, uji, chakula, tamu tamu. Keki, mkate, kionjo.

Vyovyote zinakubali.
 
Kitunguu na mafuta kidogo sana ya kukaangia kitunguu unaweka nyanya ikikaribia kuiva unaweka karanga zilizosagwa usiweke nyingi weka binzari ya njano na chumvi rost vizuri mpaka ianze kutoa mafuta weka maji kidogooo tayari kwa kula kwa wali, ndizi, na ugali utajiramba kinoma
 
Hapa nadhani unaongelea karanga za kusaga ambazo huongezwa kwenye mapishi kama unavyoweka nazi. Mimi nataka kujua kama karange zenyewe zinafaa kuungwa na kutumika kama mboga ya kulia wali, ugali nk kama maharage
Bibie FaizaFoxy amemaliza kila kitu.

Bila shaka umempata vizuri sana
 
Kitunguu na mafuta kidogo sana ya kukaangia kitunguu unaweka nyanya ikikaribia kuiva unaweka karanga zilizosagwa usiweke nyingi weka binzari ya njano na chumvi rost vizuri mpaka ianze kutoa mafuta weka maji kidogooo tayari kwa kula kwa wali, ndizi, na ugali utajiramba kinoma
Raha zaidi uzichemshe kwanza karanga mbichi, kisha uziunge kama ulivyoelekeza, aaah, utajing'ata ulimi.
 
Nawashukuru sana.. nna karanga mbichi nusu kilo kesho ntajaribu kuziunga kisha ntaleta mrejesho
 
Leo nimepika wali na njegere za nazi.
Ngoja nikaoge nije nipakue nile. Demu wangu sijui atakuja aje anisifie mapishi!
 
Kitunguu na mafuta kidogo sana ya kukaangia kitunguu unaweka nyanya ikikaribia kuiva unaweka karanga zilizosagwa usiweke nyingi weka binzari ya njano na chumvi rost vizuri mpaka ianze kutoa mafuta weka maji kidogooo tayari kwa kula kwa wali, ndizi, na ugali utajiramba kinoma
Waganda hii stew wanaipenda sana kwenye misosi yao.
 
Back
Top Bottom