SI KWELI PreGE2025 Kardinali Pengo amuonya Kitima kutumia Kanisa kwenye Siasa

SI KWELI PreGE2025 Kardinali Pengo amuonya Kitima kutumia Kanisa kwenye Siasa

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Source #1
View Source #1
photo_2025-04-23_10-07-07.jpg
 
Tunachokijua
Kardinali Polycarp Pengo ni kiongozi wa kanisa katoliki akiwa ni Askofu mkuu mstaafu wa Jimbo kuu la Dar Es Salaam ambaye aliteuliwa na Papa Yohane Paulo II kuwa Kardinali na kumsimika rasmi tarehe 21 Februari 1999.

Padre Charles Kitima ni katibu wa baraza la maaskofu katoliki Tanzania (TEC) ambaye alipata daraja takatifu ya upadre ambapo mwaka 2022 aliadhimisha Jubilei ya miaka 25 ya Upadre katika Parokia ya Kristu Mfalme Siuyu Jimbo Katoliki Singida mahali alipozaliwa.

Aidha Padre Kitima amekuwa ni moja kati ya viongozi wa dini ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu ya kiraia ili kuwawezesha wananchi kushiriki kikamilifu kwenye michakato ya kidemokrasia.

Mnamo mwezi Aprili 20, 2025 baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) lilitoa wito kwa serikali ya Tanzania kuwaachilia bila masharti viongozi wa kisiasa waliokamatwa kwa kudai haki, likisisitiza kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kulinda amani ya taifa, hasa kuelekea mwaka wa uchaguzi.

Madai

Kumekuwapo na taarifa inayosambazwa mtandaoni inayodaiwa kuchapishwa na Jambo TV ikiwa na kichwa cha habari ''Kardinali Pengo amuonya Kitima kutumia kanisa kwenye siasa''

Uhalisia wa Chapisho

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia maneno muhimu (Key Word Search), imebainika kuwa Taarifa hiyo si ya kweli, kwani haikuchapishwa katika kurasa za mitandao ya kijamii ya Jambo TV.

Aidha kupitia adhimisho la Misa Takatifu ya mkesha wa Pasaka iliyoadhimishwa na Kardinali Pengo, katika jimbo katoliki Bagamoyo hakutoa kauli yoyote iliyomhusisha padri Kitima dhidi ya masuala ya kisiasa.

Hata hivyo Padri Dkt. Charles Kitima aliwahi kusema viongozi wa dini hawawezi kutenganishwa na siasa kwani viongozi hao kuiweka siasa pembeni ni kutokuelewa majukumu ya msingi kama viongozi wa dini kwani ushiriki wao ni kupeleka tunu walizokabidhiwa na mwenyezi Mungu kutoka kwenye biblia na Quaran huku akisisitiza kuwa siasa zote zilianza katika madhehebu.​
Cadinali Rugambwa ndie haswa kawanyooshea kidole viongozi wa kanisa katoliki kua makini na wanachohubiri na kupima ni kitu ambacho kina faida au hasara za kimwili na kiroho? :NoGodNo:
 
Back
Top Bottom