Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kumbe lile tamko si la Baraza la Maskofu........
tamko gani?
Kiongozi wa kanisa lenye waumini wengi zaidi hapa Tanzania Muadhama Policarp Kardinali Pengo amependekeza kura ya siri ndiyo inayolinda utu... Amesema ni maoni yake kama Pengo na si maoni ya wakatoliki.
Kura ya wazi ina umuhimu mkubwa ndani ya bunge maalumu la katiba kuliko kura ya siri (tafadhalini sana, zingatieni asili ya bunge hili, ni bunge maalumu la katiba).
Bunge maalumu la katiba lina wajumbe ambao wana wajibu wa kufanya maamuzi kwa niaba ya wale wanao wawakilisha. Sasa kwa upigaji kura wa siri, wale wanao wakilishwa watajiridhishaje kuwa maoni yao yamepigiwa kura kama walivyo pendekeza?
Hapa tatizo lipo kwenye kuaminiana tu, na hilo suala la kura siri ni sawa itumike lakini sio katika mazingita haya ya kuandaa katiba ya nchi, katiba ya nchi aihitaji usiri wa namna yoyote, kila hatua iwe wazi tu.
Kuandaa katiba ya nchi ni tukio kubwa, mjumbe wa bunge hili hana sababu ya kuwa na hofu kama atasimama upande wa maslahi ya taifa (maslahi ya Watanzania walio wengi). Lakini kama ana yake ya siri basi hapo ana kila sababu ya kutetea kura ya siri.
Angalizo: Tofautisheni kura ya kuchagua kiongozi na hii ya kupitisha ibara za katiba. Kule kwenye kuchagua kiongozi, sisi hatuna shida na dhamira yako juu ya kiongozi umtakae. Ila kwenye kupiga kura ya ibara, kama taifa tunataka kuona dhamira yako juu ya yale mambo ya msingi yenye maslahi mapana kwa taifa.
Ccm wanajambajamba..
Mawazo yako binafsi yakizidi ni bora uache uongozi wa kanisa na kuingia katika ulingo wa siasa.
Si uongo yaonyesha wazi jinsi vinyegenyege vinavyokupanda na kila wakati kupenda kusema neno kubwa la kisiasa ambalo wajua kama kiongozi wa kanisa ni hatari.
Jitose tu kama Slaa ili uwe huru zaidi.
Pole Kapengo.
CCM hawajiamini sasa wanatafuta jinsi ya kujikwamua , wanapigwa kila mahali kumbuka Amir Kundecha alisema kura iwe siri , naona na Pengo kaja na msimamo kama Amir , hapo maana yake wakristo na waislamu wameamua kuunga na ktk hilo , sasa wapagani kina Kingunge na CCM watafute uungwaji mkono wa mashetani au !