Kardinali Pengo: Wanaomuita Rais Dikteta wajitafakari upya. Je, watoto kusoma bure na kujenga Hospitali ni udikteta?

Kardinal Pengo nimsomi mkubwa sana na mtu mwenye akili sana. Watu wamechukua maneno yake kuhusu Makonda kuwa Rais baada ya Mh Magufuli kama yalivyo nakufikiri ndio alivyo manisha.

ila nilazima tukumbuke Kadrinali Pengo ni mwana theologia mkubwa ktk maswala ya uongeaji na uwandishi.

Neno kasema lina maana kubwa sana hasa kwa kijana mwenyewe kiasi angejuwa basi angesali sana maana maneno hayo ni mazito na yana maana ktk maana nyingine.

Ukipenda sifiwa basi kubali sifa zote hata kama kejeli pokea ujifunze kwazo.

Sisi wenginetunapita tu alie kutuma ndio ukamlilie kama hukutumwa ujifunze kwa mwaka umeita viongozi wa dini mara ngapi?
 
Hii komenti ndo ingebidi ianze baada uzi.
 
Askofu anajitoa akili.kaona elimu bure na kujenga hospitality tu.vipi kuhusu kutekana hovyo,watu kupotea, wapinzani kuzuiwa kufanya mikutano na kufunguliwa kesi za ajabu ajabu, watumishi kufukuzwa kazi bila kupewa kiinua mgongo, ukosefu wa ajira, wakulima was korosho ,
 

Mimi pia mkatoliki
 
Gwajima aliwahi kuuliza hivi huyu "Pengo amekula maharage ya wapi sijui".... kwa maana yamedhuru afya ya akili yake
 
Was Gadaffi a Dictator ?

Dictator...
In government, a dictator is a ruler who has total control over a country, with no checks or balances to prevent abuse of power.
 
Nimefurahi sana Magufuli kufananishwa na Mussolinni!!!!
Magufuli=Mussolini!!!!
Wakatoliki tujitafakari sana kanisa takatifu katoliki la roma(roman empire)
Sasa ni kanisa takatifu katoliki.
Kumbe inatakiwa yaangaliwe mazuri tu!!
 
Mm nafikili maana ya neno udikiteta bado haijulikani vizuri hata pengo akaitafute asome aelewee aanze kuongea vizurii
 
Kwan watu wanajua maana ya neno udikiteta kwa upanaa? Je pengo anajua maana ya neno idikiteta na je watanzania wanajua maana ya neno lenyewee?!
 
u supporting him kuwa kuitwa dictator sio lazima uwe kweli dictator.

Gaddafi wasnt dictator ila USA ilimchafua ili wamtoe
Huyu mzee iko siku atamwita shetani savior!!! Gaddafi alitoa Elimu bure, umeme bure, mke bure, harusi bure bado aliitwa dictator! Sasa Elimu kitu gani!!!
 
GUSSIE,
Tumepokea maoni. Ni kweli Hitler alipendwa sana. Alikuwa mwongeaji mzuri mwenye ushawishi mkubwa. Aliingia madarakani kwa kura, wala sio kwa ubavu. Aliinua sana Ujerumani kiteknolojia. Akifanya nazuri mengi. Je, hayo yote yanahalalusha uovu alioufanya?
 
Huyu mzee amenifanyanya mpaka niwe na huzuni kwa kuwa mkatoliki, naona aibu kwa kuwa mkatoliki kutokana na maneno yake, hivi kujenga hospital na watoto kusoma bure kunaondoa haki ya mtu kuishi? Kweli! mbona haoji kupotea kwa kina Azory? Mbona hasemi kuhusu kutekwa na maiti kuokotwa kwenye mifuko? Mbona hasemi yaliyompata Tundu Lisu?! Kweli sio kila asemaye bwana bwana ataurithi ufalme wa mbingu, tutaanza kusali majumbani sasa.
 
Ningemuomba baba yetu Cardinal awaombee wananchi wote watanzania walioko mahakamani na magerezani waliobambikiziwa kesi za kila aina hawana tena muda wa kukaa na familia zao na kutumikia taifa lao.Angewaombea wale wanaoneza chuki na ubaguzi wa kisiasa hili nchi yetu ibaki na amani.
 
Na yeye ajitafakari
Your browser is not able to display this video.
 

Attachments

  • Apandacho mtu ndicho atakachovuna ( 268 X 480 ).mp4
    370.1 KB
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…