benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Yawezekana watu wengi sana wanatizama na kuona kuwa soka la Bongo limekuwa katika miaka ya hivi karibuni. Lakini tujiulize mbali na mafanikio binafsi ya vilabu hasa Simba na jitihada binafsi za mchezaji mmojammoja kama Samatta na Msuva ni nini kingine ambacho sisi kama Taifa tunaweza kujivunia katika suala la michezo:
1.Bado timu zetu za Taifa ni WASHIRIKI katika mashindano mbalimbali na sio WASHINDANI. Tunawaza kucheza World CUp wakati hatuwezi hata kumfunga DR Congo katika uwanja wetu wa nyumbani, (NDOTO ZA ALINACHA HIZI)
2.TFF hii imekuwa ni ya magumashi na kuungaunga ikiongozwa na watu ambao kwa nyakati tofauti uraia wao umewahi kutiliwa mashaka na mamlaka husika juu ya uraia wao (Hili sio la msingi leo tuliache). Nadhani tunakumbuka namna ambavyo Rais wa sasa wa TFF alivyoingia madarakani kwa sarakasi huku wapinzani wake WAZITO wote wakiondolewa kwa kilichoelezwa eti kukosa sifa. Tujiulize tu, hapa Tanzania ni Karia pekee mwenye sifa za kuongoza TFF?
3. Tuhuma za rushwa, ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha zimekuwa zikitawala siku baada ya siku. Nadhani tunakumbuka kuwa kuna jalada TAKUKURU kuhusu TFF kufanya matumizi mabaya ya fedha ikiwemo kiasi cha shilingi bilioni 1 zilizotolewa na Hayati Rais Dkt John Magufuli. Hivi karibuni TFF imeingia na mkataba na kampuni ya GSM ambao umeleta mvutano mkubwa wa mgongano wa kimaslahi. Karia na timu yake wako kimya tu na zaidi walitoa barua ya TISHIO kuwa mkataba huo ni kaati ya TFF na GSM na hakuna anayeruhusiwa kuujadili. TFF wanasahau kuwa wao ni kampuni ya umma inayopaswa kundeshwa kwa kuzingatia uwazi
4. TFF mwaka huu wameliingiza Taifa katika aibu ya karne baada ya timu kutoka Tanzania, Biashara United kushindwa kusafiri kwenda Libya kwenye mchezo wa marudiano wa michuano ya shirikisho licha ya kuwa mchezo wa kwanza walishinda 2-0 hapa Tanzania. Kwanini nawahusisha TFF kwenye hili, NAWAKUMBUSHA tu kuwa baada ya mchezo wa awali, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa aliitaka Wizara ya Sanaa, Michezo na Utamaduni kwa kushirikiana na TFF kuhakikisha timu ya Biashara United inasafiri kwenda Libya. Kilichotokea sote tunakifahamu, Biashara haikusafiri, Walibya wakapewa ushindi na TFF HAIKUWAHI KUTOA MAELEZO YOYOTE KWA UMMA JUU YA KUSHINDWA KUTEKELEZA MAAGIZO YA MTENDAJI MKUU WA SHUGHULI ZA SERIKALI, WAZIR MKUU KASSIM MAJALIWA
Leo tuishie hapo kwa uchache lakini tutambue kuwa, unapokuwa kiongozi na mfumo au chombo unachokiongoza kikasuasua au kughubwika na kashfa chafuchafu, basi unapaswa kuwajibika, unapaswa kung'atuka, lakini kama Karia kashindwa kuona haya na anazunguka tu kwenye kiti pale Karume mpaka sasa hata vifungo vya shati havifungi vizuri basi ni vyema aondolewe (ALIWE KICHWA) kwa manufaa ya soka la nchi hii, kisha walio chini yake watamfuata.
SWALI NI JE, KUNA WA KUMTOA KARIA PALE KARUME KWENYE OFISI ZISIZOVUTIA ZA MAKAO MAKUU YA SOKA NCHINI, MAANA INASEMEKANA NYUMA YAKE YUKO KIGOGO MMOJA SERIKALINI AMBAYE PIA NI SHABIKI NGULI WA MOJA KATI YA HIZI TIMU PACHA ZA KARIAKOO