Karia kugombea tena urais wa TFF. Je, Karia anastahili nafasi nyingine?

Karia kugombea tena urais wa TFF. Je, Karia anastahili nafasi nyingine?

Linguistic

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2021
Posts
3,669
Reaction score
8,268
Wakati akihojiwa na Mtangazaji wa Efm Radio, Bwana Wallace Karia amesema ni wazi kwamba mwaka huu atagombea tena nafasi ya Urais wa TFF.

Amesema atafanya hivyo ili atekeleze mambo aliyoongeza kwenye Ilani yake na mengine mapya aliyoanzisha.

Je, KARIA ANASTAHILI NAFASI NYINGINE?
 
Hofu yangu CCM watauingilia huo uchaguzi, watataka limwana ccm ndo lishinde ata kwa figisu. yamekuwa kama mafisi kila mahali yapo yanasubiri mizoga...
 
Wakati akihojiwa na Mtangazaji wa Efm Radio, Bwana Wallace Karia amesema ni wazi kwamba mwaka huu atagombea tena nafasi ya Urais wa TFF.

Amesema atafanya hivyo ili atekeleze mambo aliyoongeza kwenye Ilani yake na mengine mapya aliyoanzisha.

Je, KARIA ANASTAHILI NAFASI NYINGINE?
Karia kama malinzi tu.
Mimi sina maoni mkuu
 
Karia hafai na kaharibu ligi kuu na vile vile marefa wote wana maagizo ya kuibeba Simba ,ingawa simba ina timu nzuri
 
Karia hafai na kaharibu ligi kuu na vile vile marefa wote wana maagizo ya kuibeba Simba ,ingawa simba ina timu nzuri
Acheni kuweweseka refa aliyekataa penati ya prison na yanga alikuwa qnaibeba Simba na yule aliyewakatalia goli aiku ya Gwambina nq Simba pia alikuwa anaibeba Simba.
Timu lenu libovu mnasingizia refa
 
Anafaa sana. Apewe mitano mingine.

Chini ya uongozi wake kumekuwa na mafanikio mengi.
1. Soka la wanawake limekuwa sana - Ligi inachezwa na Timu za Taifa za wanawake zimerudi na vikombe vya ubingwa wa Cosafa.
2.Usimamizi mzuri wa fedha za FIFA pale TFF hadi Zanzibar nao walionja mgao
3.Ligi ya Timu za vijana inakuza soka letu hadi kufanya vizuri kwa Timu ya Taifa Serengeti Boys
4.Ligi kuu Tanzania imepata mvuto mkubwa chini ya uongozi wake hadi kushika nafasi ya nane ya ubora Africa. Inaoneshwa live na mapungufu ya Marefarii yamepungua sana tofauti na enzi za watangulizi wake wote.
5.Tiketi za ki-electronic zimesaidia kupunguza wizi wa fedha za mapato ya viwanjani
6.Mafanikio ya Timu ya Taifa kutinga kwa mara ya pili Afcon na zile fainali za CHAN
7.Kudumisha mahusiano mema na nchi nyingine hadi kuvutia timu za nchi nyingine kuomba kutumia uwanja wa Taifa kwa ajili ya mechi zao.
8. Simba na Namungo zimefanya vizuri kimataifa chini ya uongozi wake

Mapungufu yake machache ambayo hayafuti mazuri yake;
A. Kukataa kufanya kazi na Makamu wake Michael Wambura ambaye alichaguliwa na kikao halali
B. Kutotoa tamko lolote la ukweli wa tuhuma za kipa Kabwili na huyu mchezaji wa Prisons juu ya kusudio lao la kutaka kupewa Rushwa
C. Kumpa adhabu ndogo Makamu Mwenyekiti wa Yanga kwa makosa ya wazi aliyoyafanya hasa kwa kutamka amemsajili mchezaji wa Timu nyingine ambae bado ana mkataba pia akitishia kujitoa kwenye ligi kisa wamenyimwa penart na Refa.
 
Karia hana jipya, hata hayo mafanikio ya kutupeleka Afcon anayojisifia, ni kama Uganda walitubeba ile game, na ushahidi wa kuwa hatukuwa na timu bora ni vichapo tulivyopokea kule,

Na kuhusu ubora wa ligi yetu kama nilivyomsikia anajitapa, wa kusifiwa ni Azam kwa kuibrand na kuitangaza ligi na Mo na GSM kwa uwekezaji na siyo TFF.

Karia hana jipya, ni style ya uongozi ile ile ya kina Ndolanga na Malinzi, fungia fungia style, ukionekana unakosoa unapigwa ban maisha[emoji706]
 
Karia hana jipya, hata hayo mafanikio ya kutupeleka Afcon anayojisifia, ni kama Uganda walitubeba ile game, na ushahidi wa kuwa hatukuwa na timu bora ni vichapo tulivyopokea kule,

Na kuhusu ligi ubora wa ligi yetu kama nilivyomsikia anajitapa, wa kusifiwa ni Azam kwa kuibrand na kuitangaza ligi na Mo na GSM kwa uwekezaji na siyo TFF.

Karia hana jipya, ni style ya uongozi ile ile ya kina Ndolanga na Malinzi, fungia fungia style, ukionekana unakosoa unapigwa ban maisha[emoji706]
Huyu Karia hafai kabisa, na amejiwekea kinga kwenye uchaguz kwa kuwatoa kwenye system wale wote waliokuwa wanampinga na kuchomeka watu wake mikoan, serikali iingilie kati huu uchaguz la sivyo hakutakuwa na uchaguz ni mapichapicha tu, na ndiyo maana wame mute tarehe na siku ya huo uchaguz.
 
Karia ni football VIRUS hapa bongo, mtu gan na yake hawataki kukosolewa! Ukiwakosoa tu wanakutafuta kwenye 18 zao unapigwa ban maisha, watu wengi wana uzoefu na weled huko mikoan wamefanyiwa rafu za kipumbavu eti kisa walikuwa wanafanya kaz na viongozi wa TFF ya zaman!
 
Wakati akihojiwa na Mtangazaji wa Efm Radio, Bwana Wallace Karia amesema ni wazi kwamba mwaka huu atagombea tena nafasi ya Urais wa TFF.

Amesema atafanya hivyo ili atekeleze mambo aliyoongeza kwenye Ilani yake na mengine mapya aliyoanzisha.

Je, KARIA ANASTAHILI NAFASI NYINGINE?
hastahili tena
 
Karia ni football VIRUS hapa bongo, mtu gan na yake hawataki kukosolewa! Ukiwakosoa tu wanakutafuta kwenye 18 zao unapigwa ban maisha, watu wengi wana uzoefu na weled huko mikoan wamefanyiwa rafu za kipumbavu eti kisa walikuwa wanafanya kaz na viongozi wa TFF ya zaman!
Kweli kabisa, Karia hakuna solution ya matatizo ya mpira wetu aliyo solve, waamuzi wabovu kama zaman na hawalipwi posho, upangaji wa ratiba za ligi mbovu kama zaman, rushwa bado kama zaman, kiufupi takataka zote za zaman bado hazijatatuliwa kwenye uongozi wake, tunahitaji mtu mpya walau atupe hope!
 
Karia hafai, ana kiburi na majivuno. Muda aliofanya kazi Tff unatosha aende akafanye shughuli zingine.
 
Back
Top Bottom