Karia kugombea tena urais wa TFF. Je, Karia anastahili nafasi nyingine?

Karia kugombea tena urais wa TFF. Je, Karia anastahili nafasi nyingine?

Karia hana jipya, hata hayo mafanikio ya kutupeleka Afcon anayojisifia, ni kama Uganda walitubeba ile game, na ushahidi wa kuwa hatukuwa na timu bora ni vichapo tulivyopokea kule,

Na kuhusu ubora wa ligi yetu kama nilivyomsikia anajitapa, wa kusifiwa ni Azam kwa kuibrand na kuitangaza ligi na Mo na GSM kwa uwekezaji na siyo TFF.

Karia hana jipya, ni style ya uongozi ile ile ya kina Ndolanga na Malinzi, fungia fungia style, ukionekana unakosoa unapigwa ban maisha[emoji706]
Mnyonge mnyongeni lkn haki yake mpeni. Chini ya uongozi wa Karia kuna mabadiliko tumeyaona hata nidhamu ya matumizi ya fedha pia ipo ukilinganisha na awamu zilizopita.

Hizo ndio hatua za awali kuanza kupiga hatua mbele kwa kushiriki Afcon...
 
Karia hafai na kaharibu ligi kuu na vile vile marefa wote wana maagizo ya kuibeba Simba ,ingawa simba ina timu nzuri
Mkuu unataka kutuaminisha kuw Yanga haibebwi na marefa?
 
Tanzania ni nchi pekee ambako Rais wa Federation na Mtendaji wake mkuu ni raia wa kigeni. Karia ni Msomali na Kidau ni Mrundi. Tumerogwa jumla
 
Kwani kumtoa ni ngumu sasa?? Pale unaandaa watu watatu tu kwenda kuchezesha katiba yao basi na ikiwa mtashindwa basi ni swala la uhamiaji tu na takukuru kubutua mpira na mechi itakuwa imeisha hivyo.
 
Karia anafaa sana, apewe miaka mingine ya kuongoza shirikisho hilo
 
Karia hafai na kaharibu ligi kuu na vile vile marefa wote wana maagizo ya kuibeba Simba ,ingawa simba ina timu nzuri
Hakika
Kaibeba Simba hadi hatua ya Robo Fainali ya Club Bingwa Afrika.
Kila Simba ikicheza Karia alikuwa anawatuma Marefa wake wafanikisha azma ya kuibeba Simba.

Bila Karia, Simba ingeisha tolewa kwenye mashindano ya Afrika. Anawabeba hata wakiwa ugenini kama kule Kongo, mchezo dhidi ya AS Vita.
 
Back
Top Bottom