House4Sale Kariakoo: 4 Bdrm Apartment For Sale - Dar

Hata ukiwa kwenye nyumba ya peke yako hizo gharama utalipia
 
Huwezi kunifungia geti langu nisipite ati kwa kuwa sijalipa bill za kuzoa taka, kwenye hayo ma apartment ya maghorofani wanaweza kukuzuia kuingia nyumbani kwako tu kwasababu hujalipa bill za matengenezo ya lift.
Hakuna wa kukuzuia kuingia kwako kwa sababu ya kutokulipa tozo ya huduma.
Kitakachofanyika ni kukusitishia huduma husika au kupelekwa mahakamani.
Kwa mfano tozo la taka ngumu wanakusanya almashauri au manispaa; maji safi na maji taka wakusanyaji pia ni taasisi ya serikali. Hawa wanaweza kukupeleka mahakamani ukiwa mdaiwa sugu.
Kuhusu lift manager wa jengo anaweza kukunyima huduma hiyo ikiwa huchangii.
Kwa mfano kuna baadhi wanaoishi ghorofa ya kwanza huwa wanajiondoa kwenye utumiaji lift hivyo huwa inazuiwa (locked) kusimama ghorofa ya kwanza
 
Matajiri wengi wanapenda sana apartment za hivyo maana huwezi kumjua maisha yake
Asubuhi mnashuka nae wala hujui anaenda wapi na yeye hajui wewe ni nani
Salaam tosha
Usalama kama wote na ni changanyikeni
Natafuta sana za hivi unakaa kwa amani sana
 
Huwezi kunifungia geti langu nisipite ati kwa kuwa sijalipa bill za kuzoa taka, kwenye hayo ma apartment ya maghorofani wanaweza kukuzuia kuingia nyumbani kwako tu kwasababu hujalipa bill za matengenezo ya lift.
Hakun kitu kama hiko
 
Hii bado ipo sokoni?Na punguzo la bei lipo?
 
Kama nataka niivunjevunje apartment yangu iliyoko floor ya 9 siitaki tena, je alie juu yangu floor ya 10 ana haki ya kunizuia?
 
Kama nataka niivunjevunje apartment yangu iliyoko floor ya 9 siitaki tena, je alie juu yangu floor ya 10 ana haki ya kunizuia?
Hayo maghorofa hauvunji kama tunavyovunja nyumba za chini. Kila maboresho ya jengo lazima yapate kibali kutoka mamlaka husika za serikali kama TBA, CRB, n.k
Hivyo ukitaka kuvunja pia lazima uombe kibali kwenye mamlaka hizo. Kama watakupatia, basi we vunja tu.
 
Bado lipo eneo nikucheki fasta
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…