Kariakoo Derby na utalii.

Kariakoo Derby na utalii.

busha

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2019
Posts
1,712
Reaction score
2,577
Nawasalimu kwa jina la muungano wa Tanzania.
Kama mnavyojua Kariakoo derby inahekaheka mpaka mikoani huko,mechi inachezwa Dar lakini miji mingine ya Tanzania kunakuwa na patashika nguo kuchanika kiasi kwamba utadhani mechi inachezwa kwenye huo mkoa.

Wapenzi na mashabiki wenzangu hasa wa mpira wa miguu kwenye Kariakoo derby kumekua na ongezeko kubwa la wageni kutoka nje ya mipaka ya Tanzania.

Wataalam wa mambo ya utalii watumie taaluma zao kubuni ni namna gani watatumia fursa ya hizi mechi kubwa za watani wa jadi kuongeza utalii wa nje na ndani ya nchi.
Hapa kikubwa kinacho hitajika ni"taaluma na ubunifu"
narudia tena kinachohitajika ni"taaluma na ubunifu"sio mihemko,siasa na kutengeneza nyufa za upigaji.

Wizara ya michezo na wizara ya utalii wakutane kufanya jambo.
Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom