KARIAKOO DERBY: Simba SC yatakata kwa kuirarua Yanga SC goli 1-0, Uwanja wa Taifa-Dar

KARIAKOO DERBY: Simba SC yatakata kwa kuirarua Yanga SC goli 1-0, Uwanja wa Taifa-Dar

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2012
Posts
2,046
Reaction score
3,971
IMG_20180429_122918.jpg
Leo ndio leo miamba ya soka nchini, Simba SC na Yanga SC wanakutana katika mchezo wa Ligi Kuu Bara unaofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar

Tambo zimetawala kutoka kwa mashabiki wa kila upande kuwa watawafunga wenzake. Simba anangalia uwezekano wa kumliza ligi mapema kabisa huku Yanga akiangalia namna ya kuweka heshima

Historia ya mechi kati ya timu hizi mbili
Zimekutana mara- 100
Yanga imeshinda- 38
Imefunga magoli 105
Simba imeshinda- 27
Imefunga magoli- 94

Kikosi cha Simba SC dhidi ya Yanga SC leo
Aishi Manula; Erasto Nyoni, Nicholas Gyan, Yusufu Mlipili, James Kotei, Jonasi Mkude, Asante Kwasi, Shomari Kapombe, John Bocco, Emanuel Okwi, Shiza Kichuya

Wachezaji wa akiba
Mohamed Ndud, Paul Bukaba, Said Ndemla, Mzamiru Yassin, Laudit Mavugo, Rashid Juma
IMG_20180429_135328.jpg


Je nani kumgaragaza mwenzake?

Tuungane hapa.......
=======

MWAMUZI:
Mwamuzi ni Emmanuel Mwandembwa, Yanga wapo na Jezi zao za njano huku Simba wakiwa na jezi zao za Nyekundu na nyeupe

Mpira unaanza hapa

01': Mechi inaanza na Yanga ndiyo wanaanza kusukuma gozi kuelekeza upande wa Simba

02': Ajibu anageuka vizuri na kuachia mkwaju lakini manula yuko vizuri

04': Ajibu anamweka chini Gyan, mwamuzi anasema ni faulo naye anasema hakufanya madhambi
Okwi alimsukuma Rostand wakati akipiga mpira, ameishaamka na mpira unaendelea

06': Mpira bado unachezwa katika ya uwanja, Simba wakiwa wamerudi nyuma kidogo na Yanga wanamiliki zaidi mpira

07': Bado game inaonekana haijatulia na hakuna mashambulizi makali na badala yake mpira unachezwa katikati zaidi

08': Manula analazimika kutoka nje ya 18 na kupiga mpira kichwa ili kuuondoa na kumuwahi Chirwa aliyekuwa katika kasi

10': Okwi anawatoka mabekiwa Yanga lakini anazuiliwa vizuri kabisa na Yondani

11': Mhilu anamuacha Kwasi na kupiga krosi safi kabisa, lakini krosi aliyopiga inapita nje ya lango la Simba

13': Ukiangalia mchezo umekuwa hauna ladha sana kwa kuwa kila upande uko makini sana na unavizia

14': Krosi ya Kwasi ndani ya lango la Yanga lakini Gyan anamsukuma Ajibu, faulo

17': Si pambano lenye mvuto sana, kila upande unasikilizia sana na faulo ndogondogo zimekuwa nyingi sana

18': Krosi nzuri ya Asante inaokolewa na kuwa kona ya kwanza, inachongwa na Kichuya
Kichuya anachonga kona nzuri kabisa, inaokolewa na kuwa kona tena, anaichonga tena, inaokolewa

21': Mpira wa kuchonga wa Kichuya kidogo uingie nyavuni lakini Rostand anadaka kwa umakini mkubwa

22': Okwi anaingia tena, mpira unaokolewa na kuwa kona nyingine. Ni kona ya tatu kwa Simba

23': Kona inachongwa na Kapombe, inatua kichwani mwa Okwi, mpira unatoka sentimeta chache nje ya lango la Yanga. Goal kick

24': Dante anafanya kazi ya ziada kuokoa shuti la Kampombe na kuondosha hatari

25': Mpira wa adhabu wa Ajibu, unadakwa vizuri na Manula

28': Simba wanamsahau Chirwa, Mhilu anapiga krosi maridadi lakini Manula anadaka vizuri

30': Kipa Manula yuko chini pale akipatiwa matibabu, inaonekana aliumia alipokwenda kuokoa mpira

32': Simba wanagongeana vizuri lakini Yanga wanaonyesha umahiri tena katika kuondosha hatari

34': Kichuya alikuwa chini, ameishaamka na Yondani anamuweka chini Kapombe, faulo
Faulo inachelewa kupigwa hapa baada ya wachezji kuvutana nadani ya box la 18 la Yanga

37': Gooooooooooooooooooaaaaaaaaaaaaaaaallllllllllll. Erasto Nyoni anaiandikia Simba bao la kwanza
Faulo nzuri liyopigwa na Kichuya kutoka pembeni mwa uwanja inampata kichwani mchezaji wa Yanga na kukutana na Erasto Nyoni ayeweke mpira ule kimiani kwa kichwa kirahisi kabisa

39': Kadi ya njano; Kadi ya kwanza ya njano inakwenda kwa Kessy baada ya kuonyesha uababe

40': Simba sasa wanagonga moja moja tu
Krosi matata ya Okwi lakini Vicent anaokoa na Mhilu anaukimbiza mpira lakini Bocco anautoa nje

43': Kapombe anamuweka chini Tshishimbi na mwamuzi ameona anasema ni faulo

44': Pasi nzuri Okwi ndani ya boksi la Yanga, anakwenda chini na mwamuzi anasema mwanamume kugangamala, twende

45': Yanga wanacheza kama vile waji mbele maana wanakwenda taratibu na zaidi wanacheza katika eneo lao

Dakika 2 za Nyongeza

Mpira ni Mapumziko Simba anaongoza kwa goli 1-0

45', SUB; Yanga wanafanya mabadiliko ya kwanza kwa kumuingiza Juma Mahadhi kuchukua nafasi ya Rapharl Daud

46': Mwamuzi Mwandembwa amewaita Bocco na Yondani na anawaonya Dk 45 mpira umeanza kwa kasi na Bocco anagongwa na Yondani na sasa yuko chini, kuna mzozo pale unaendelea

47': Mahadhi anaingia vizuri kabisa, krosi nzuri lakini Manula yuko makini, anadaka

48', KADI NYEKUNDU: Kessy analambwa kadi ya njano ya pili na kuandika nyekundu, ilikuwa ni baada ya kumuangusha Kwasi

50', KADI YA NJANO: Kotei analambwa kadi ya njano kwa kucheza kibabe
Dk 50 Bocco anamchambua hadi kipa, lakini mpira wa Bocco uliokuwa unakwenda nyavuni unaokolewa na Dante

52': Krosi ya Mahadhi, Tshishimbi anaachia mkwaju, Manula anaruka na kudaka

55': Simba bado hawajaonekana kama kweli wanaitumia nafasi ya Yanga kucheza
pungufu kwa kuwa hakuna mashambulizi mengi na Yanga wamerudi nyuma
> Kwasi anampa Bocco, naye anamuachia Okwi lakini anapiga shuti kuuuuuuubwaaaa

56': Okwi anaachia mkwaju mkali kabisa, unatoka sentimeta chache pembeni mwa lango

57': Shambulizi jingine kali la Simba, pasi nzuri ya Bocco, mkwaju wa Kichuya unaokolewa na kuwa kona

58': Mpira wa kona ya tano ya Simba, Mkude anaachia mkwaju mkuuuubwaaaa
>>Tshishimbi anamshika Okwi na kumuweka chini, mwamuzi anasema faulo

59': Okwi anagongeana faulo na Kichuya lakini inakuwa ya kizembe na Yanga wanafanya kazi nzuri ya kuokoa, mwisho offside

61': Mpira wa adhabu wa Ajibu unatoka nje na kuwa goal kick. Mwamuzi anakuwa mkali kwa Manula ambaye anaonekana kama anataka kupoteza muda hivi

62': Mahadhi anamuweka Kichuya chini, nje kidogo ya msitari wa 18
>>SUB; Yanga inafanya sub ya pili, Pius Buswita anaingia kuchukua nafasi ya Ajibu

63': Mpira wa Okwi unaokolewa na kuwa kona ya sita ya SImba, inachongwa na kuokolewa

65': Yanga wanaonekana wanaanza kufunguka lakini Mlipili yuko makini, anaokoa unakuwa wa kurushwa

67': Kichuya anamtoka Makapu, anaingia na kupiga krosi safi kabisa, Dante anapiga kichwa na kuokoa

70': Bado inaonekana Yanga wanafanya mashambulizi ya kufunga, lakini Simba wanapoteza nafasi nyingi na lazima wazitumie mapema maana Yanga bado nao wana uwezo wa kufunga
>> Kichuya anapangua watu wawili, anatoa pasi kwa Bocco, naye anampa Kapombe kona ya saba ya Simba, Yanga hawana kona hata moja

74': Mpira unachezwa huku Simba wakionekana kkujiamini zaidi, na Yanga kucheza harakahara wakipata mpira

76': Krosi maridadi katika lango la Simba, Chirwa anaruka na kupiga kichwa lakini ni goal kick

79': Bado Simba wanatawala eneo la katikati lakini Yanga wanajitutumua

80', SUB: Yanga wanafanya sub ya mwisho, wanamtoa Tshishimbi na nafasi yake inachukuliwa na Emmanuel Martin

82': Mahadhi anaingia na kujaribu kupiga krosi, Mkude ameunawa ni faulo si mbali na lango la Simba

83', SUB: Simba wanamtoa Gyan nafasi yake inachukuliwa na Paul Bukaba

84': Okwi ndani ya boksi la Yanga lakini Rostand anafanya kazi nzuri na kuokoa

87': Yondani anaonekana kuhaha kila eneo kujaribu kuhakikisha bao linarudi
>>Yondani yuko chini pale, inaonekana ameumia ni nyama za paja na tayari madaktari wameingia kumganga

88': afasi nzuri kwa Simba lakini Kichuya anakuwa na papara kwa kupaisha juuuuuuu

90': Yanga wanaingia lakini Simba wamejaa nyuma

DAKIKA 4 ZA NYONGEZA
 
Back
Top Bottom