Kariakoo imehamia Stendi ya Magufuli, Mbezi Louis

swala siyo malengo , kuwa Jiji inatokana na mtukufu atakavyoamua , si umeona mwenyewe Chanika na ulongoni pamoja na buguruni kwa Mnyamani ni Jiji lakini Oysterbay , Masaki na Mbezi Beach ni nje ya jiji !
Kwani mbezi beach na Obay na Masaki kuna nini zaidi ya makazi ya watu!?
 
kwa nilicho kiona hapa kweli nakubali maendeleo hayana chama.
wakuu mnisamehe nimeshindwa kupata "position" nzuri ya kupiga picha nzuri.
 
Mbona nipo huko sijakuona
 
Sasa nini hatma ya wasafiri na mali zao! Itabidi serikali ijenge stendi nyingine kwa ajili ya abiria baada ya hii kugeuzwa soko, nashauri na uwanja wa ndege wamachinga wanyonge waruhusiwe kufanya biashara kando ya njia ya kurukia ndege, hii itawawezesha wageni kununua bidhaa wanapoondika nchini.
 
nimeambiwa kuna vyumba vya biashara vinapangishwa juu kabisa, na pia nimeambiwa kuna shopping malls zitakuwepo juu.
kuna mpangilio ulio pangwa vizuri kwa wafanyabiashara ndogondogo.

lkn mimi ktk andiko langu nilimaanisha uwekezaji nje au pembezoni mwa kituo, sio lazima sote tujazane ndani.

kutokana na umbali wa mbezi kariakoo ni vyema tukajenga maduka makubw yenye bidhaa za kutosha ktk maeneo ya mbezi/Luguruni/kibamba/kiluvya n.k maaana wafanyabiashara hawataki usumbufu kwenda kkoo.
hii ni fursa kwa wajasiriamali.
 
tumehangaika sana jana kutafuta bureau de change hapa mbezi, hzio ni huduma muhimu na za haraka kwa wafanyabiashara kuchangamkia, changamkieni fursa ktk eneo hili.
 
acha kukurupuka maji hayajawahi kupanda mlima kariakoo bado iko kariakoo,halafu huna hata kapicha au upo kwenye ile timu ya kusifu na kuabudu
 
Kariakoo huwezi ifananisha mkuu kile ni kijiji cha biashara...ni kama mbezi luis yote iwe maduka ndo itaanza fanana na kkoo. Ila ni ukweli mbezi miaka mitatu ijayo itakua mbali sana kwenye biashara na tutashuhudia sky scrapers zinaanza kujengwa za kutosha. Tuwekeze mbezi aisee mi nahama makumbusho soon
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…