Kariakoo imehamia Stendi ya Magufuli, Mbezi Louis

Kariakoo imehamia Stendi ya Magufuli, Mbezi Louis

Sawa. Kariakoo itabakia majengo. Mbezi itabakia kuwa kitovu Kipya Cha biashara
Hiki ni kichekesho. Yaani jengo moja linachukua nafasi ya kitongoji chote kinachoitwa kariakoo?
 
Ndio maana halmashauri ya ubungo wamepewa hekari zingine 75 na mheshimiwa rais ili wafanye uwekezaji mkubwa wa miumdombinu ya kibiashara.
It's coming soon kwamba baadhi ya bidhaa zitapatikana hapo hapo karibu na kuwarahisishia wafanyabisahara urahisi wa kufupisha safari.
 
Tunamshukuru ubungo mateja wamepungua.......
Kariakoo 'a mbezi wapi na wapi
 
Mi bado sijaelewa, kwa hiyo sasa hv mabasi hayafiki ubungo yanapotoka mikoani, au yanapoenda yanaanzia mbezi moja kwa moja au?
 
Vibaka wote pia wamehamia hapo ukitoka nje ukibofya bofya unakutana nao

Ova
 
Je uwepo wa stendi Ubungo ulisababisha KKOO kuumia

Sent from my TECNO W2 using JamiiForums mobile app

Tunazungumzia stendi ya Magufuli Mbezi Louis ambayo ina hadhi ya juu zaidi sana na siyo hilo genge la wahuni na gereji bubu la Ubungo ambalo halikuwa na madhara kwa Kariakoo ukilinganisha na Mbezi Louis
 
imekuwa "hub" kitovu cha kibiashara.

1. Daladala kutoka pembe zote za Jiji lazima zifike mbezi.

2. Mabasi kutoka mikoani na nchi jirani lazima zifike mbezi.

naiona Mbezi baada ya miaka michache mbele itakuwa centre kubwa ya kibiashara.
 
Ni kweli mtoa mada Mbezi baada ya muda itachangamka kibiashara,ila tatizo ninaloliona mbezi ni kwa wenye nyumba zilizo centre ya mbezi,wengi wao hawajiongezi katika kuboresha Fremu zao.yani utakuta wanajenga vijifremu vidogo vidogo kwa lengo la kukusanya kodi nyingi za wafanya biashara wadogowadogo badala ya kujenga fremu za maana kama wenzao wa kariakoo ili kuwafanya wafanyabiashara wakubwa kuja kuwekeza.
 
Halafu shida nyingine ya Mbezi ni kutokuwa na mpangilio mzuri kwa wafanya biashara.
Mfano,utakuta Nyumba moja ina mlundikano wa biashara aina tofauti tofauti kama kumi..huo si uchafuzi?
 
Back
Top Bottom