Kariakoo market 1949

Gangongine,
Huo ni mtazamo wako una haki nao hakuna wa kukuzuia.
Nimekuonyesha njia ya kulijua tatizo umekataa hapana ugomvi.

Mkapa alituomba "ushahidi wa kisayansi" tukampa.
Alipousoma alipata simanzi na hofu.

Asingeweza kutuangalia usoni na ushahidi tuliompa.

Matokeo yake aliona njia bora ni kuukataa ushahidi usitolewe kwa kupiga marufuku ushahidi wenyewe.

Mimi nilichofanya ni kukushika mkono tu nikupitishe njia tuliyompitisha aliyekuwa na dhamana ya kusimamia haki Rais Mkapa.

Aliyoyaona yalimdhihirishia ukweli wa dhulma.
Hadi leo hakuna kiongozi aliyetudai tena ushahidi.
 
Gangongine,
Umererejea mara tatu kunifafanulia kuhakikisha kuwa nimekufahamu.
Wala hapakuwa na haja.

Nimekuelewa mara ya kwanza.
Nami narejea tena kwako.

Huna ujuzi wa kutosha kujadili somo hili.
Ukitaka ujadili somo hili soma rejea hizi:
  1. P van Bergen (1981)
  2. J. Sivalon (1992)
  3. Hamza Njozi (2002)
Hao ndiyo wasomi watafiti waliolizungumza tatizo hili.

Wewe hujafanya utafiti wowote na kama ulivyosema, ''No research no right
to speak.

Lakini ukipenda unaweza ukamsoma na M. Said (1998).
 
NIMEWASOMA WOTE HAO NIKAKUTA MALALAMIKO TU. TENA KAMA NJOZI NDIO HAMNA KITU KABISA NI ULALAMISHI TUPU. HAJAELEZA STATUS YA WAISLAM KIELIMU NA NYANJA NYINGINE NA KWA NINI WAPO HAPO. HAKUNA TAKWIMU ZA ULINGANIFU NA MADHEHEBU MENGINE KATIKA NYANJA MBALIMBALI. KAMA AMBAVYO WEWE UNAOGOPA KUZITOA HAPA KWA KUJUA UTASHINDWA MJADALA HUU! RESEARCH INAKWENDA NA TAKWIMU. NDIO NAZISUBIRI NA HII NI MARA YA NNE LAKINI UNAKWEPA!! HUKU NDIO KUSHINDWA KWAKO!
 
Gangongine,
Sijakwepa kitu ninakujibu kadri ya uwezo wangu.
Nami nina maswali naomba nikuulize.

Ikiwa Njozi hamna kitu ni sababu ipi ilifanya serikali ikipige
marufuku kitabu chake iwe kosa la jinai kukutwa na kitabu
hicho?

Sababu gani halikadhalika wachapaji wa kitabu cha Sivalon
wakitoe kitabu kwenye mzunguko na hali kadhalika Bergen?

Unalitumia neno ''woga'' mara kadhaa dhidi yangu.
Mimi jasiri.

Mimi si mwoga na ndiyo maana unaona hapa natumia jina
langu halisi: Mohamed Said.

Si jina tu hata picha zangu nyingi zipo hapa Majlis.

Nakupa changamoto na wewe jitokeze katika jina lako halisi
ikiwa wewe si mwoga.
 
BASI BWANA SITAPOTEZA MUDA KUBISHANA NAWE. HUNA HOJA ZA MSINGI ZAIDI YA UBISHI TU
 
BASI BWANA SITAPOTEZA MUDA KUBISHANA NAWE. HUNA HOJA ZA MSINGI ZAIDI YA UBISHI TU
Gangogine,
Nilijua hutofika mbali na mimi.
Ila nina moja kwako.

Jifunze kuandika.

Watu hawaandiki kwa kherufi kubwa nadhani Maalim Faiza
alikueleza hilo.

Kherufi kubwa maana yake unapiga kelele.
 

Neno sahihi ni "corps" i.e (Carrier Corps) ni kikosi cha vibarua (Wafrica) kilicho anzishwa na watawala wa kikoloni (Waingereza) huko Nairobi wakati wa vita vya kwanza vya Dunia 1914 - 18, kilihundwa mahususi kusaidia kubeba mizigo na zana za kivita katika kampeini za Waingereza kuwang'oa Wajerumani Africa Mashariki (Tanganyika) baadhi yao walipewa mafunzo ya kijeshi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…