Kariakoo market 1949

Kariakoo market 1949

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074

Wanamajlis,
Mara nyingi nimekuwa kila nikieleza historia ya TANU na harakati za kudai uhuru nimekuwa nikimtaja Abdulwahid Sykes na Kariakoo Market ambako alikuwa akifanya kazi kama Market Master.

Soko lenyewe ndilo hilo hapo juu kama lilivyokuwa katika miaka 1950 hadi miaka ya 1970 lilipovunjwa na kujengwa soko hili tulionalo sasa.

Bahati mbaya huwezi kuina ofisi ya Abdul Sykes lakini mkono wa kulia wa picha hiyo ni Mtaa wa Swahili ukikatizwa na Mtaa wa Tandamti (Mtaa wa Mshume Kiyate).

Ukiufuata mtaa huo moja kwa moja utakutana na Mtaa wa Mkunguni na ndiyo mwisho wa soko.

Kushoto ni Mtaa wa Nyamwezi.

Ofisi ya Abdul Sykes ilikuwa katikakati ya Mtaa wa Swahli na Tandamti na Swahili na Mkunguni.

Hapo ndipo Mwalimu Nyerere alipopelekwa na Abdul na akawa Nyerere akija pale ofisini kwa Abdul kila alipokuja mjini kutoka Pugu.

Hapo sokoni ndipo Mwalimu Nyerere alipojuana na Shariff Abdallah Attas mmoja wa watu maarufu wa Dar es Salaam enzi zile na mtu aliyekuwa anajua mengi katika historia ya TANU.

Abdul
aliuza kadi za kwanza za TANU ndani ya ofisi ile kiasi kwamba iko siku alizozana na Town Clerk Mzungu aliyetaka kujua kwa nini kadi za TANU zinauzwa pale.

Katika miaka ile ya 1950 mwanzoni hapo palikuwa moja ya vituo vya harakati na kituo kingine kilikuwa Ilala Welfare Centre ofisini kwa Hamza Mwapachu.

Hizi ndizo zilikuwa baadhi ya sehemu ya harakati wakati wa mchana.

Baada ya kazi walikuwa wakikutana Tanga Club New Street na Mkunguni kujiburudisha na kuzungumza siasa.
 
Mzee Mohamed Saidi sijaelewa vizuri hapo Kati ya Swahili Na tandamti...kama iko mbali mbali hii mitaa???but all in all napenda sana habari zako naomba tu unifafanulie hapo
 
Hakika Jijila DAR-ES-SALAAM lina historia nyingi sana.... Ndg. Mohamed Said naomba ukipata wasaa tumwagie Historia za shule za elimu za hapo dar !!!
Zamiluni,
Sina nijuacho katika hayo.
Zamilu, unaulizia historia za shule kwa Muslim Fundamentalist!, ungeulizia hitoria za madrasa hapo ungepata!, maana Maalim Mohamed Said mwenyewe kasoma shule za mission!, huyo Hamza Mwapachu naye kasomesha wanaye Juma na Bakari shule za mission!, wakati wengine wakijikita kutengeneza mashule kuelimisha, wengine walikuwa bize na madrasa, cha ajabu, hao hao walioponeo shule za mission ndio wamekuja kuwa watu wa maana sana, ila hata shukrani kidogo tuu ya japo kutaja historia ya shule za mission zilizowakomboa, kamwe hutasikia, lakini ....

Yote tisa, kumi Carriers Coop ilipendeza!.
Pasco
 
MNYONGE MNYONGENI LAKINI "HAKI YAKE MPENI"

ahsante Pasco Honestly speaking :- walosoma madrasa wengi au wote ni watu wenye sifa kadha:- Duni, waungwana, masikini,watulivu, wasamria wema na WAMINIFU !!

OMG!! sasa hayo yaliyosoma shule za Missions sifa zao dalili zipo na ushuhuda upo:- ni Waghushaji,Wezi,Shahada feki,Ubadhirifu, Rushwa na UFISADI ulokubuhu !!!

uthibitisho na chanzo:- From 1961 hadi 2016 wananchi wenye uhai !!

Mohamed Said
wakusoma
Chachu Ombara
 
Mimi kuna kitabu kimoja nliwahi kukisoma Historia ya Tangayika kwa kweli machozi yatakutoka kutokana na mambo yalivochambuliwa humo yaani sio mchezo
 
Zamilu, unaulizia historia za shule kwa Muslim Fundamentalist!, ungeulizia hitoria za madrasa hapo ungepata!, maana Maalim Mohamed Said mwenyewe kasoma shule za mission!, huyo Hamza Mwapachu naye kasomesha wanaye Juma na Bakari shule za mission!, wakati wengine wakijikita kutengeneza mashule kuelimisha, wengine walikuwa bize na madrasa, cha ajabu, hao hao walioponeo shule za mission ndio wamekuja kuwa watu wa maana sana, ila hata shukrani kidogo tuu ya japo kutaja historia ya shule za mission zilizowakomboa, kamwe hutasikia, lakini ....

Yote tisa, kumi Carriers Coop ilipendeza!.
Pasco
Pasco carriers coop ya wapi tena? Pls ukiwa na ishu za maana use unanitupiemo
 
Zamilu, unaulizia historia za shule kwa Muslim Fundamentalist!, ungeulizia hitoria za madrasa hapo ungepata!, maana Maalim Mohbize na madrasa, cha ajabu, hao hao walioponeo shule za mission ndio wamekuja kuwa watu wa maana sana, ila hata shukrani kidogo tuu ya jap......
Yote tisa, kumi Carriers Coop ilipendeza!.
Pasco
'Carriers Coop'? Nani alikudanganya.., Kariakoo ilikuwa imepangwa kwa ajili ya makazi ya makazi ya makuli, hivyo kuitwa 'Carriers quarters' na sio coop (banda la kuku)
 
Historia nzuri, ila kama umegusia kidogo sana, tupe vitu adimu hivyo kihistoria tuvijue.

Bahati mbaya, utandawazi huu umetufanya wengi kujua zaidi ya magharibi na ughaibuni huko, kuliko ya huku kwetu.

Binafsi napenda sana historia, hasa hizi za kwetu.

Ahsante!
 
Back
Top Bottom