FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,246
- 123,145
Tafiti ndogo tu, yangu binafsi na isiyo na shaka kabisa niliyoifanya kuhusu jina la jiji letu kuu "Dar Es Salaam" na jina la soko letu kuu "Kariakoo" ninaihitimisha kwa ufupi (summary) hapa chini kwa kusema wanahistoria hususan wa hapa Tanzania hawayatendei haki hayo majina kwa kutuaminisha maana ya majina hayo isiyo halisi na isiyo ya kweli.
Dar Es Salaam
Kila ninapokutana na maana ya jina Dar Es Salaam naona makosa ya wazi kabisa au ya wanaotoa maana kutokufanya tafiti japo kidogo au kuwaamini sana wanahistoria ambao au wao kuwaamini waliowafundisha au waliyoyasoma bila kuyafanyia tafiti na kuiamini tu maana inayotolewa. Au ni makusudi inafanyika ili kuifuta maana halisi ya jina hilo na lilipoanzia kihistoria.
Mara nyingi, kama si zote, tumeaminishwa kuwa maana ya neno Dar Es Salaa ni "bandari ya Salama", na wanatuaminisha kuwa historia yake ni Waarabu waliotoa jina hilo kutokana na kuwepo bandari hapo Dar Es Salaam. Huo tunaoaminishwa sio ukweli.
Ukweli ni kuwa neno Bandari halimaanishi bandari kwa Kiarabu bali neno Bandar ni neno la Kiajemi (Persia) linalomaanisha bandari. Na ipo miji maarufu ya Kiajemi (Persia) yenye jina hilo.
Jina Dar Es Salaam halina neno "Bandar" la Persia au Kiarabu hata maana yake iwe ni "Bandari". Jina hilo lina neno la Kiarabu"Dar" linalomaanisha Nyumba au "dari" kwa maana "haven". Kwa akirefu chake ni Dar Es Salaam ni Nyumba ya Amani au vile vile Dar Es Salaam ni "haven of Peace". Ambayo ni maana halisi ya jina la lililokuja kuwa jiji letu pendwa.
Neno Dar Es Salaam linatokana na neno la Kiarabu fasaha "Dar Us Salaam" linalopatikana ndani ya Qur'an Tukufu, utalipata katika sura ya 10 aya ya 25 na sura ya 6 aya ya 127 likimaanisha jina la pepo (Abode or Haven of Peace).
Kwa maana hizo, jina la jiji letu la Dar Es Salaam lilianzia kilipojengwa chuo cha kwanza cha Kiislam (Madrassa) hapo ilipo sasa Ikulu ya Dar na jengo hilo la la chuo hicho ndio likaitwa Dar Us Salaam (Nyumba ya amani) na ilipo Hospitali ya Ocean Road ndipo palikuwa mabweni ya chuo hicho. Mjerumani ndiye akja kukifanya chuo hicho kuwa nyumba ya gavana baada ya kukitengeneza upya lakini aliacha mjengo ule ule wa asili kwa kiwango kikubwa. Athari za majengo ya Kiarabu na Kiislaam kwenye Ikulu yetu ipo mpaka leo. Haipingiki kwa aijuae Ikulu hiyo.
Kama hiyo haitoshi, pia kuna nchi, Brunei, jina la jiji lake linaitwa Dar us salaam kama jiji letu Dar Es Salaam, lakini kwenye jiji hilo hilo bandari yake inatwa Bandar Seri Begawan. Hiyo inaonessha tofauti iliyopo katika maana ya maneno "Bandar" na "Dar".
Baadhi ya miji yenye jina hilo na maana yake ikielezewa Kiingereza...
From Wikipedia, the free encyclopedia
Darussalam (Arabic: دار السلام) is an Arabic word which means "abode of peace" and is the name of one of the layers of Jannah (Paradise in Islam). It may refer to:
Post ijayo ntawaletea maana ya jina Kariakoo.

- Aceh Darussalam, a special administrative region of Indonesia
- Brunei Darussalam, a country in Southeast Asia
- Darussalam Publishers, a Saudi based multilingual international publishing house operates in 35 countries.
- Darussalam (actor) (1920–1993), Indonesian actor
- Darussalam Seminary, an Islamic Seminary (Hawzeh) in Iran