Kariakoo na Dar es Salaam: Wanahistoria tendeeni haki Historia za majina hayo

Sijagadhibika ila umepta elimu, ishikilie.
Kobello,
Ninapokusoma naona hujapendezwa na niandikayo.

Nami nakueleza haya upate kunifahamu kuwa sifurahi kuona mwenzangu kaumizwa na sababu ni kalamu yangu.

Kuhusu elimu hiyo uliyoweka ni kitu kidogo kinahifadhika kirahisi sana.

Mimi nimekuwekea historia ya vizazi vitatu vya ukoo wangu hapo Kariakoo kuanzia Bi. Debora 1890 - 1995.

Huyu bibi yetu alisoma na alifanya kazi kwa gavana na wanae wote walipata elimu nzuri mmoja alifikia kuwa ofisa balozi baada ya uhuru na wengine walishika nafasi za maana baada ya uhuru.

Hawa wote wamezaliwa Swahiili Street nyumba no. 88 kona na Narung'ombe karibu sana na soko la Kariakoo.

Hii nyumba bado ipo ingawa sasa imejengwa upya na si nyumba ya makazi bali ni godown imepangishwa kwa wafanyabiashara tofauti wenye maduka Kariakoo.

Jirani na hapo ziko nyumba nyingine mbili Mtaa wa Sikukuu na Narung'ombe na nyingine Sikukuu na Makisi Mbwana zamani Stanley.

Nyumba hii imepeana ubavu na nyumba ya Abdul Sykes.

Nyumba zote hizi zimejengwa upya lakini kumbukumbu ya zile nyumba za asili bado zipo kichwani mwangu.

Nimeishi na kucheza utotoni katika nyumba hizi zote.

Hiyo picha hapo chini ni soko la Karikaoo kwa upande wa Mtaa wa Swahili na soko hapo lipo mkono wa kushoto.

 
Mwaka 1900, Hayo maeneo yalikuwa yanaitwaje?
 
Unapata faida gani kwa mfano iwe kweli ni kiingereza au kiarabu kuna lolote unafaidika bwa mdogo?mbona mnakua hamna busara namna hii matusi ya nini sasa kijana jiheshimu japo kidogo maalun shaitwan weye[emoji109]
 
Shukrani, kwa upeo wangu binafsi hoja yako ni ya msingi ukizingatia na kiarabu unakifahamu. Labda binafsi najiuliza kwanini walipotosha tafsiri ya hilo jina?!! Hawakuwa na uelewa wake?!
Kuna mtu amepost amesema mama anajua kiarabu Sana.
 
Yangu sio tafsiri, nimeleeta maana halisi ya jina lilipotokea ki "anthropology".

Qariah Kuu.
 

Una lingine zaidi? Kama huna sasa kanisome tena vizuri uipinge hoja.

Sikushangai unapodai kuwa Waislam hawana elimu, kweli kabisa hatuna, ikiwa elimu yenyewe ndiyo hiyo yako ya kuandika namna hiyo, Waislam hatuna kabisa hiyo na wala hatuihitaji.
 
Shukrani, kwa upeo wangu binafsi hoja yako ni ya msingi ukizingatia na kiarabu unakifahamu. Labda binafsi najiuliza kwanini walipotosha tafsiri ya hilo jina?!! Hawakuwa na uelewa wake?!
Swali lako zuri sana, labda ni kujikweza kwa wazungu au labda kwa Mwafrika kuonekana ana mila za Kizungu ndio maendeleo.
 
Shukran kwa elimu nzuri.
 
Mpaka sasa utafiti wa FaizaFoxy haujapata mpinzani hasa kuhusu asili ya neno Dar Es Salaam. Bado ni ujinga kukataa evidences alizotoa kwa sababu nyepese za kiimani..
Yote mawili ndugu yangu ndiyo ukweli, Dar na Kariakoo vyanzo vya majina hayo ndivyo hivyo, asikwambie mtu.


Hii pwani yote ya Mashariki ya Afrika kuitenganisha na Uarabu na Uislam ni ngumu sana.

Msome Ibn Batuta aliyekuja pwani hii kabla ya wazungu, utanielewa.
 
Kama ikulu ilijengwa na mjerumani, kwanini kuna sehemu pale ikulu, mpaka leo ina maneno ya kiarabu?

Aina ya majengo yaliyojengwa pale kwanini yana aina ya usanifu wa majengo ya kiarabu?
 
Vipi kuhusu Ngorongoro na Loliondo??
 
Historia ya nchi hii imepindishwa pindishwa na hakuna anaesema kweli. Ni kama vile tunavyodanganywa Rais wa kwanza wa Zanzibar na mwanamapinduz alikuwa ni Mzee Karume wakati sisi tunajua ni uongo alikuwa John Okelo. Utasikia cjui Nyerere na akina Sheikh nan na kundi lao ndio walipigania Uhuru wa nchi hii wakati sisi tunajua ni uongo. Sisi tunajua tunajua wapigania Uhuru halisi walikuwa akina Kinjikitile ngwale, Mkwawa,Mirambo Mangi Sina, Songea na wengine. So hakuna msema kweli. Kila mtu anavutia kwake.
 
Vyanzo ni lugha ya Kiarabu kama nilivyoelezea. Qariya ni mji au kijiji kwa Kiarabu, kuu sina uhakika wa Kiarabu chake lakini kwa Kiswahili ni wazi kabisa, inajulika maana ya "kuu".

Kariakuu kuwa kariakoo inaleta maana zaidi kuliko "carrier cops"
 
"bandar" ni Kiajemi, siyo Kiarabu. Kaiarabu bandari ni "Mina". Usichanganye lugha.

Dar Es Salaam ni wazi kabisa kwa Kiararabu, Dar ni nyumba au Kingereza unaweza pia kusema "abode au "haven" lakini siyo "bandari".

Pia nimeona juu "argument" yako ya Kariakoo kuwa haipo kwenye ramani. Ramani siyo kielelezo cha lugha na jina la sehemu, hususan miji au vijiji vya zamani.

Tafiti yangu ndogo ime "base" kwenye lugha siyo maandiko ya zamani au ramani za zamani.

Kiswahili Qaria kuu inaleta maana zaidi kuwa ni kariakoo ya leo kuliko Kingereza "courier cops".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…