Kariakoo: Nimenunua Raba kali kinoma kwa 15,000/=. Madukani huwa naona zinauzwa 70,000/=

Kariakoo: Nimenunua Raba kali kinoma kwa 15,000/=. Madukani huwa naona zinauzwa 70,000/=

Mlolongo

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2019
Posts
3,483
Reaction score
6,257
Kariakoo baba lao.

Nilikua nimeenda kununua Tende pale Msimbazi msikiti wa Idrisa kwa ajili ya iftar (kufuturisha).

Sasa wakat naondoka nikapita mitaa ya katikati mule, nikaona meza moja Raba kali kinoma, zile wanaziiitaga Air Jordan, Nike, NBA snickers. Kuulizia bei zake akaanzia 20,000!

Daaah nikavikagua na kuanza kujisemea moyoni hivi si naonaga akina David Sportswear, Robyone, NjooKariakoo2020 wanauza kuanzia 65,000 mpaka 70, 0000!!!

Nikamwambia mshikaji mie nina 14,000 akanitolea nje. Nikasepa, akaniita akasema ongeza buku. Nikampa 15,000 nikabeba.

Wakuu, kumbe madukani huwa mnaibiwa. Vitu vya kijanja kwa bei za kijanja vyote vipo Kariakoo.

IMG_20210425_160017_282.jpg
 
Back
Top Bottom