dfreym
JF-Expert Member
- Oct 14, 2010
- 342
- 87
- Thread starter
-
- #21
pole sana mkuu.
Uwezo hupo mkuu wa kuokoa meno yako ufanye maamuzi haraka sana.
Nenda kwa daktari wa meno wa safishe meno.unatoka damu kwa vile fizi zako azipumui na zimevimba.unatakiwa kwenda kwa daktari wa meno kusafisha japo mara moja kwa mwaka.
Baada hapo wewe binafsi inabidi upige mswaki mara mbili kwa siku kila baada ya mlo tumia mswaki laini.tumia mswaki wako laini kukanda fizi zako taratibu kila ukipiga mswaki.kitu kingine muhimi ni kutoa vyakula vilivyo nasa kati kati ya meno (flossing).kwa vile fizi zimevimba kwa sasa inabidi baada ya yote hayo huwe unasukutua na maji ya chumvi ya vugu vugu kila baada kupiga mswaki.piga mswaki kabla kwenda kulala na usile kitu kingine unaweza kunywa maji.
Ukifatisha yote hayo mkuu na atakayoongezea daktari wa meno hutopoteza meno yako na wala kuona tone la damu wakati wa kupiga mswaki.
thanks bro nimekuelewa, nitafanyia kazi ushauri wako, ubarikiwe