Karibia nakuwa kibogoyo

Karibia nakuwa kibogoyo

pole sana mkuu.

Uwezo hupo mkuu wa kuokoa meno yako ufanye maamuzi haraka sana.


Nenda kwa daktari wa meno wa safishe meno.unatoka damu kwa vile fizi zako azipumui na zimevimba.unatakiwa kwenda kwa daktari wa meno kusafisha japo mara moja kwa mwaka.

Baada hapo wewe binafsi inabidi upige mswaki mara mbili kwa siku kila baada ya mlo tumia mswaki laini.tumia mswaki wako laini kukanda fizi zako taratibu kila ukipiga mswaki.kitu kingine muhimi ni kutoa vyakula vilivyo nasa kati kati ya meno (flossing).kwa vile fizi zimevimba kwa sasa inabidi baada ya yote hayo huwe unasukutua na maji ya chumvi ya vugu vugu kila baada kupiga mswaki.piga mswaki kabla kwenda kulala na usile kitu kingine unaweza kunywa maji.


Ukifatisha yote hayo mkuu na atakayoongezea daktari wa meno hutopoteza meno yako na wala kuona tone la damu wakati wa kupiga mswaki.


thanks bro nimekuelewa, nitafanyia kazi ushauri wako, ubarikiwe
 
Jamani wana jf doctor nisaidieni nisijekuwa kibogoyo.

ninatatiza la fizi kutoka damu hasahasa ninapopiga au nikiyanyonya mate kwanguvu mswaki.

pia meno yangu yoote ya sebuleni (ya mbele) yanatikisika mmno kiasi siku nikijichanganya tu na kumchokoza bansa aka ni pa! mdomoni
yote naya tema.
yani yanatikisika mno kiasi hata nikitumia nguvu kungoa yanatoka.
halafu yanauma. nisaidieni jamani.
ni usafi wako tu unahitajika hapo.si lazima umwone dakta wa meno,sukutua meno yako sawia kabla na baada ya kula,sugua fizi na ulimi,osha kwa maji ya chumvi mara kadhaa,chokonoa fizi zako kutoa mabaki ya chakula na nyama nyama ktk fizi ............,

i cnt imagine wife anajisikiaje akitaka kukupa denda,its diguisting mwanaume kuwa mchafu kinywani
 
Ugonjwa wa ufizi



Ugonjwa wa ufizi huathiri ufizi na huweza kusambaa kwenye mifupa inayoshikilia meno. Hii ni mojawapo ya sababu ambazo hufanya watu kupoteza meno. Ugnjwa huwa katika hatua mbili lakini inapokuathiri waweza kutibu kabla ya kusababisha madhara

Ni nini baadhi ya dalili au ishara
Hatua ya kwanza ya ugonjwa huu wa ufizi huitwa ‘gingivitis'
Baadhi ya dalili/ishara ni pamoja na:

  • Ufizi nyekundu na iliyofura
  • Ufizi unaotoa damu unaposugua meno
  • Ufizi uliong'oka kutoka kwenye meno
  • Harufu mbaya isiyoisha

Wanawake wajawazito kwa kawaida huathiriwa na ‘gingivitis'. Ukiwa mjamzito tunza afya yako ni vizuri ikiwemo meno.

Hatua ya pili ya ugonjwa wa ufizi huwa hatari sana.

Waweza kuwa na ishara/dalili zilizotajwa hapo juu

  • Usaha unaotoka kwenye meno na ufizi
  • Meno iliyolegea
  • Nafasi kubwa katikati ya meno mahali ambapo ufizi inapaswa kuwa
  • Kutokuwepo na tofauti katika mpangilio wa meno ukiyauma chini.

Unaitibu vipi?
Ukiwa na dalili zozote za hatua ya kwanza, sugua meno na utumie uzi spesheli kutoa chakula katika meno mara kwa mara na umuone daktari wa meno. Ukiitibu tatizi hili basi utazuia ugonjwa wa ufizi.

Ukiwa na dalili zozote za hatua ya pili, mwone daktari haraka iwezekanavyo. Meno yako yaweza kung'oka au kung'olewa na daktari wa meno ikiwa hutatibiwa mara moja. Ugonjwa huu ukiwa mbaya sana daktari wako wa meno anaweza kukuelekeza kwa daktari wa meno aliye na ujuzi wa ugonjwa wa ufizi.

nenda kwa Doctor akupe pia Vidonge vya Multi Vitamin una upungufu wa Vitamin Mwilini mwako ndio maana unapopiga mswaki unatowa Damu kwenye ufizi wako. Je wewe Mwenzetu una umri wa miaka mingapi? Je wewe ni Mwanamme au Mwanamke?
 
Mbinu za kusugua meno



Toothbrush_0.jpg




Kusugua meno yako ni swala rahisi. Mbinu hii huwa na athari kubwa sana katika afya ya meno yako na afya yako kwa jumla.

Mbinu bora ya kusugua meno:

  • Kwa kutumia mswaki na kwa upole laini na itakayotoshea mdomoni mwako.
  • Mswaki kubwa hautafika kwenye meno ya nyuma ilhali ile ndogo itakufanya kutumia wakati mwingi sana katika kusugua meno. Ukiwa wahitaji usaidizi katika uchaguzi wa mswaki, zungumza na daktari wako wa meno.
  • Tumia dawa ya meno iliyo na floraidi.
  • Watoto wanapaswa kutumia kiasi kidogo cha dawa ya meno na watu wazima watie dawa ya meno inayolingana na urefu wa nywele wa mswaki.
  • Sugua meno yako angalau mara mbili kwa siku, unapoamka na kabla ya kulala. Ikiwezekana sugua meno yako baada ya kula chakula. Kama hauwezi, sugua mdomo wako hasa baada ya kula vyakula vya sukari.
  • Sugua meno kwa dakika mbili. Angalia kwenye saa kujua muda uliotumia.
  • Badilisha mswaki wako baada ya miezi mitatu au unywele ukijikunja.
Kumbuka kusugua pande zote za meno:

  • Sugua meno yako kutoka kutoka nyuma hadi mbele kwa upole.
  • Sugua karibu na ufizi kwa mwendo wa mviringo; ili unywele wa mswaki ufike sehemu ambapo meno na ufizi zinakutania mahali ambapo chembechembe ya chakula haionekani
  • Sugua sehemu zote za meno, sehemu ya nje, sehemu ya kutafuna chakula na sehemu ya ndani
  • Tumia unywele wa juu wa mswaki kusafisha sehemu ya ndani ya meno yako ya juu; kwa mtindo wa juu na chini
  • Sugua ulimi wako kwa upole ili kuondoa vijidudu au viini vinavyosababisha pumzi au harufu mbaya.
Ukitaka zaidi bonyeza hapa https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/85896-mbinu-za-kusugua-meno.html
 
Pole sana kwa yaliyo kukuta maana watu wanaweza kuona mzaha kumbe wewe kweli unaumia
nenda kamuone dentist utapata tiba nzuri ya tatizo lako
 
Tatizo jingine laweza kuwa ni ugaga (dendal calculus) ambalo hutibika kwa kufanyiwa scling kwa dentist, histopathology yake ni ndefu kidogo kuelezea hapa
 
Tarehe 08/02, nilimuona daktari akanipa appointment, aliniambia meno yangu yanahitajika kusafishwa. So tarehe 10/02, nilienda nikasafishwa meno. Kweli kulikuwa na uchafu mgumu uliokuwa umeganda kwenye meno ya chini, hivyo alifanikiwa kuutoa karibia wote. Akaniambia ninunue hydrogen peroxide (mouth wash) niwe naskutua asubuhi, mchana na jioni. Pia akaniambia nirudi baada ya wiki moja tuone kama meno yatakuwa yameanza kukaza.
Kuanzia hapo tatizo la kutokwa damu limekata, ila meno bado yanaum( si mara kwa mara) halafu nahisi bado hayajakaza kama nilivyotarajia kwa haraka. Ngoja nitaendelea kuwapa feedback. Asanteni nyote
 
Tarehe 08/02, nilimuona daktari akanipa appointment, aliniambia meno yangu yanahitajika kusafishwa. So tarehe 10/02, nilienda nikasafishwa meno. Kweli kulikuwa na uchafu mgumu uliokuwa umeganda kwenye meno ya chini, hivyo alifanikiwa kuutoa karibia wote. Akaniambia ninunue hydrogen peroxide (mouth wash) niwe naskutua asubuhi, mchana na jioni. Pia akaniambia nirudi baada ya wiki moja tuone kama meno yatakuwa yameanza kukaza. <br />
Kuanzia hapo tatizo la kutokwa damu limekata, ila meno bado yanaum( si mara kwa mara) halafu nahisi bado hayajakaza kama nilivyotarajia kwa haraka. Ngoja nitaendelea kuwapa feedback. Asanteni nyote
<br />
<br />
Safi sana mkuu umefanya maamuzi mazuri na kwa haraka.

Kukaza meno yatachukua mda kidogo uendelee kufuata maelekezo yote.hydrogen peroxide nzuri sana kwenye kuua bacteria na uendelee kusafisha meno kama ulivyopata maelekezo.


Kwenye kulegea meno,vipi daktari alipiga x ray hili kuangalia roots za meno yako ziko katika hali gani hivi sasa?


Kila la kheri mkuu na endelea na tiba salama.
 
Mkuu inaelekea una gum disease, inabidi ujitahidi sana katika usafi wa kinywa. Hili linaweza kusaidia katika kupunguza kupukutika meno kinywani mwako na kubaki kibogoyo. Kusafisha meno kwa dentist ni muhimu sana katika hali kama hii kama unajiweza jitahidi ufanye kila baada ya miezi minne na baada ya miaka mwili unaweza kufanya mara mbili kwa mwaka. Kila la heri katika juhudi zako za kuzuia ukibogoyo.

Periodontal (Gum) Disease: Causes, Symptoms, and Treatments
 
Si ndo itakuwa vizuri mzee unajipunguzia na matatizo ya kung'ang'ana na mifupa na vitu vigumu. Wewe utakuwa mtu wa softsoft tu, mayai, soda, nk!
Kama hukubaliani na ushauri huo basi kamwone dentist.
 
Pole sana mkuu, ni tatizo kubwa sana hasa katika show na maongezi, yaani speech!
Tatizo lako linasababishwa na matatizo ya fizi, yaani periodontal diseases, ambayo husababishwa na uchavu mgumu kwenye fizi, calculus!
nenda haraka kwa daktari wa meno, atakufanyia matibabu na hayo yaliyolegea yatakaza vzr sana, na kukupa ushauri mahsusi kuhusiana na hali hiyo. hiyo habari ya dawa ya mswaki ya forever haitasaidia lolote mpaka calculus zitoke!NENDA HARAKA KWA DENTIST ALIYE KARIBU NAWE!
 
Si ndo itakuwa vizuri mzee unajipunguzia na matatizo ya kung'ang'ana na mifupa na vitu vigumu. Wewe utakuwa mtu wa softsoft tu, mayai, soda, nk!
Kama hukubaliani na ushauri huo basi kamwone dentist.

acha visa,mwenzako yupo serious.utani mbali,ukiwa huna meno,unakuwa unachekesha,kusmile huwezi,jamani meno ni muhimu
 
nahisi kutakuwa zi zaidi ya uchafu wa meno, kwani hata doctor alisema baada ya wiki yatakuwa at least yameanza kukaza. ila ni wiki sasa, bado yako vile vile. aliniambia after one week i have to go back for the recheck up, itabidi next week nirudi. this week siwezi course itakuwa bado ni below 10 days. then nitawapa feedback kwa yatakayotokea. msijali ndugu niko pamoja nanyi kuona zoezi zima linafanikiwa.
 
Back
Top Bottom