Karibu JF Mgeni. Naomba nikutambulishe kwa familia yetu

Analyse ,shukhrani! Maelezo yako nimeyafanyia tutorial, kidogo nimeanza kuelewa matumizi ya hii social network, sasa naweza kumtag mtu na ku point maneno machache kwenye reply ya mtu!
[emoji120][emoji120][emoji120]

Kilichobaki ni kufungua fake ID isiyo na jina langu halisi ili nianze kuchambua nyuzi za siasa [emoji23][emoji23]

Pia mkuu, vipi kuhusu kama mtu unahitaji ku quote replies mbili kutoka kwa watu tofauti na kuchangia mawazo kwenye reply yako moja!?
 
Sio mpaka ufungue ID, omba Mods wakubadilishie jina. Waweke unalotaka.

Kuquote watu wawili au zaidi kwa pamoja. Click mtu wa kwanza, then wa pili alaf bonyeza mshale ulio juu kulia. Hapo utaweza kufanya unachotaka
 
asant xana baharia nmeelew
 
Karibu mgeni,
Kuna members ambao kazi yao ni ku reply neno "chai" au "gahawa" au picha za chai na gahawa! katika nyuzi zako!

Wengine wana matumizi ya kauli changamoto za "Watakuja kusema huna akili ngoja waje..." kikubwa ni kuwazoea tu!

Ndugu mgeni, Maxence mello hajaweka limit za idadi ya nyuzi ambazo mtu anatakiwa kuanzisha kwa siku, ila kuna member uchwara, badala ajibu kinachofaa kutoka kwenye thread, yeye ataishia kusema "Dogo, thread ulizotengeneza zinatosha...", "Mkuu, acha sifa" n.k

Ewe mgeni, wana jf wote wana magari jitahidi uwe na gari hata la kuchora, Ewe mwanamke, hakikisha unakuwa financially stable, hata pesa za maboksi tafuta!

Mgeni wangu, wana jf wote ni wataalamu wa lugha fasaha na ya kifasihi, wanakicharanga kiswahili kama lugha yao mama, hivyo matumizi ya r na l yatakuponza kama usipokuwa makini

Ewe mgeni, trophy points ni kitu cha maana kwenye ID yako, lakini usishangae uka participate kwa uchungu kiasi gani lakini Maxence Melo akaishia kukupatia points 1000 tu!

Unaweza tengeneza uzi wako, uwafikie watu 200 tu kwa wiki mbili, lakini wakina Analyse ,DeepPond na Mshana Jr nyuzi zao zikawafikiwa watu 10M within 1 hr na reply zisizopungua 3k

Narudi baadae, ngoja nikayasake madhaifu!
 
Well said........nakupa 5.
 
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]hapo mwisho mbona umenisagia kunguni mkuu?
 
Si mgeni lakini nimekuwa nje ya jukwaa kwa takribani miaka 10 ...hongereni JF imebadilika haswa ...nasi unalo lipi la kutufaa?
 
Skills yake kwenye uandishi ni high level..big up! umeongea Ukweli sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…