Idd Ninga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 5,497
- 4,775
1.Kunavyo vingi vizuri
Vizuri vino pendeza
Vyang'ara nakuvutia
2.Vipo kwenye jiji zuri
Lilojawa na mwangaza
Kama utaliingia.
3.Taona mengi mazuri
Ambayo yanashangaza
Miguu ukiitia.
4.Utapofika Dodoma
Macho ukiyaangaza
Ni Kondoa yatatua.
5.Hutokosa la kusema
Ni Furaha utawaza
Tena utafurahia.
6.Kuwaona watu wema
Kwa mazuri Wanaweza
Na mabaya wachukia.
7.Tena wanajua dini
Na kumuamini Mungu
Dini wameshikilia.
8.Vyakula vya ardhini
Vitamu viso vichungu
Kondoa utajilia.
9.Na wanyama wa bandani
Tutapikia kwenye chungu
Kwa raha utajilia.
10.Na ugali wa maziwa
Tunajua kupika
Mtamu unavutia.
11.Ukila utanogewa
Moyo utafurahika
Kondoa utabakia.
12.Machoni utavutiwa
Mapangoni ukifika
Irangi kushuhudia.
13.Michoro ile ya kale
Iliyochorwa zamani
Ni huku imetulia.
14.Walichora babu wale
Waloishi mapangoni
Leo tumejirithia.
15.Leo siyo zama zile
Za kale zama zamani
Bado tumejitunzia
16.Utawaona warembo
Mashaallah wamejaliwa
Wazuri wanavutia
17.Tena waso na matambo
Sisubiri kuambiwa
Njo utajionea
18.Watu waso majigambo
Upole wamejaliwa
Akili zilotulia.
19.Nikisema zote sifa
Basi kesho itafika
Na nyingi zitabakia.
20.Hapa hapa natulia
Ukitaka shuhudia
Basi karibu Kondoa.
SHAIRI -KARIBU ARUSHA
MTUNZI-Idd Ninga,Tengeru Arusha
iddyallyninga@gmail.com
+265624010160
Vizuri vino pendeza
Vyang'ara nakuvutia
2.Vipo kwenye jiji zuri
Lilojawa na mwangaza
Kama utaliingia.
3.Taona mengi mazuri
Ambayo yanashangaza
Miguu ukiitia.
4.Utapofika Dodoma
Macho ukiyaangaza
Ni Kondoa yatatua.
5.Hutokosa la kusema
Ni Furaha utawaza
Tena utafurahia.
6.Kuwaona watu wema
Kwa mazuri Wanaweza
Na mabaya wachukia.
7.Tena wanajua dini
Na kumuamini Mungu
Dini wameshikilia.
8.Vyakula vya ardhini
Vitamu viso vichungu
Kondoa utajilia.
9.Na wanyama wa bandani
Tutapikia kwenye chungu
Kwa raha utajilia.
10.Na ugali wa maziwa
Tunajua kupika
Mtamu unavutia.
11.Ukila utanogewa
Moyo utafurahika
Kondoa utabakia.
12.Machoni utavutiwa
Mapangoni ukifika
Irangi kushuhudia.
13.Michoro ile ya kale
Iliyochorwa zamani
Ni huku imetulia.
14.Walichora babu wale
Waloishi mapangoni
Leo tumejirithia.
15.Leo siyo zama zile
Za kale zama zamani
Bado tumejitunzia
16.Utawaona warembo
Mashaallah wamejaliwa
Wazuri wanavutia
17.Tena waso na matambo
Sisubiri kuambiwa
Njo utajionea
18.Watu waso majigambo
Upole wamejaliwa
Akili zilotulia.
19.Nikisema zote sifa
Basi kesho itafika
Na nyingi zitabakia.
20.Hapa hapa natulia
Ukitaka shuhudia
Basi karibu Kondoa.
SHAIRI -KARIBU ARUSHA
MTUNZI-Idd Ninga,Tengeru Arusha
iddyallyninga@gmail.com
+265624010160