Hello the Bosses and Roses.
Katika kuelekea kuufunga mwaka wetu huu wa 2024, embu twende pamoja katika kuwapa tuzo wasanii wetu wa Muziki kwa kuwa wanafanya kazi kubwa kuhakikisha jamii yote inaburudika, inaelimika na pia inafuraha kutokana na talanta za sauti zao walizopewa na Mungu.
JF Music Awards, ni tuzo zetu wana jukwaa kwa ajili ya kuthamini mchango wa wasanii wetu ili kuwapa motisha na kuona kumbe kuna jamii kubwa kutoka mtandaoni inayothamini talanta zao.
JF MUSIC AWARDS, hizi tuzo zitakuwa zikitolewa kila mwisho wa mwaka ikiimaanisha kila mwezi Desemba tutaangalia mafanikio ya msanii/ wasanii fulani na kuwapa tuzo zao.
Tunaweza kukosa kitu (tangible worth) cha kuwapa ila hata tukiwa mention kama kwa mfano msanii bora wa mwaka ni msanii fulani kutoka katika mchuano wa wasanii wengine bora itampa hamasa ya yeye kuwa bora zaidi.
JF MUSIC AWARDS, Inathamini mchango wa wasanii kwa sababu kwa kupitia sanaa yao hii;
- Vijana (wa kike kwa kiume) wamepata ajira.
- Wameweza kufungua biashara zao na kuajiri vijana wengine.
- Wanakuza uchumi kwa kusaidia uwekezaji mkubwa katika sekta mbalimbali
- Wanaitangaza nchi kwa kuwa mziki wao unavuka Tanzania hadi nje ya Afrika.
- Wanavuta watalii kutoka pande mbalimbali za dunia.
- MSANII BORA WA KIUME AFRIKA.
- MSANII BORA WA KIKE AFRIKA.
- WIMBO BORA WA MWAKA AFRIKA.
- MSANII BORA WA KIUME BONGO FLEVA 2024.
- MSANII BORA WA KIUME RAP 2024.
- MSANII BORA WA KIKE 2024.
- WIMBO BORA WA MWAKA BONGO FLEVA.
- WIMBO BORA WA MWAKA RAP
- VIDEO BORA YA MWAKA.
- MSANII BORA WA KUMILIKI JUKWAA.
- MSANII BORA WA SINGELI
- WIMBO BORA WA SINGELI
- MSANII BORA WA GOSPEL
- WIMBO BORA WA GOSPEL
- KUNDI BORA LA MZIKI TANZANIA
- WIMBO BORA WA KUSHIRIKIANA 2024.
- BEST COMEDIAN ( MCHEKESHAJI BORA WA MWAKA)
- MSANII BORA MWEKEZAJI NA MFANYABIASHARA
- MSANII BORA WA ZAMANI ILIYEPO SOKONI MPAKA SASA.(Hapa tunataka kuenzi wasanii wakongwe ambao kwenye game bado wapo wanatoa nyimbo kali mpaka hivi sasa. Kwa hiyo msanii kama miaka 10 iliyopita alikuwa kwenye kilele cha ubora wa sanaa lakini mpaka sasa 2024 bado anatoa nyimbo kali. Tumewafikia wasanii hao, hiki kipengele kinawahusu na hicho kipengele kinachofuata)
21. MSANII BORA CHIPUKIZI
22. PRODUCER BORA WA MZIKI
23. DANCER BORA WA MWAKA.
24. MSANII BORA ANAYESHIRIKI KAZI ZA KIJAMII.
(Lazima wasanii wajue kwa kujihusisha na jamii kufanya kazi za pamoja na jamii kama vile kuwapa misaada, kujitolea muda wake kwenda kufanya kazi pamoja nao kama za mazingira kinastahili kabisa kupewa tuzo hii. Tunataka tujenge jamii ya wasanii wanaojihusisha na jamii)
25. WASANII WENYE FAMILIA ZA MFANO ULIO BORA.
(Hapa tunataka kutengeneza jamii ya wasanii wanajali familia kwa kuheshimu misingi ya familia. Hivyo tuzo hii itahusisha couple ambazo zipo kwenye familia na wanaishi pamoja kama mke na mme.)
Hivyo mdau pendekeza jina la msanii wako bora na wimbo wake bora katika kipengele hapo juu unapoona anafit ili zoezi la kupiga kura litakapoanza aweze kuwa miongoni mwa wasanii wachache watakaopewa heshima kutoka JF MUSIC AWARDS 2024.
Tumeanza kupokea majina ya wasanii baada ya hapo tutafuatiwa na kipengele cha kupiga kura.
Karibu kwa kutaja jina la msanii na maoni kama yapo ili tufanye tuzo hizi kuwa kubwa na za mfano Tanzania.🙏🙏
Tarehe 25/11/2024 zoezi la upigaji kura litaanza huku washindi wakitarajiwa kujulikana 22/12/2024.