Karibu mjini

Karibu mjini

ZOPPA

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2017
Posts
2,729
Reaction score
2,891
Leo nimeingia Supermarket pale Kibo Complex Tegeta,..Basi nikachukua Mkate Mkubwa na Maji, ..Ajabu tangu nachagua bidhaa kwenye Shelf kuna Mzee mmoja alikuwa ananifuata nyuma nyuma mpaka nikaogopa,

nikaenda kaunta kwa Cashier bado ananifuata nyuma!,..Nikarudi kwenye Shelf kuchukua Soda bado Mzee yupo! Duh!

MZEE : Sory kijana kama nimekutisha, unafanana sana na Mwanangu aliyefariki juzi na kuzikwa Makaburi ya Kinondoni,

MIMI: kwa hiyo mzee unataka kusema nini?

MZEE : bahati mbaya Mwanangu amefariki bila hata kusema bai, naomba unisaidie kitu kimoja, wakati naondoka nikikupa Mgongo walau useme BAI BABA! Ili nijisikie kama niliagwa na Marehemu Mwanangu jamani!, nisaidie (akatokwa machozi)

MIMI: hilo tu? Usijali Mzee!.

Kisha Mzee yule akachukua bidhaa zake mafurushi kibao mpaka pale kaunta akahesabiwa vitu vyake akabeba na kunipa Mgongo ili nitimize alichoomba.

MIMI : Bai baba!

MZEE: Bai Mwanangu Mpenzi, asante!!

Mzee yule alipoondoka nikaenda Kwa Cashier na kupigiwa hesabu

CASHIER : Kaka Unadaiwa Tsh 238,500/=

MIMI : kivipi? Yaani Mkate, Maji na Soda pesa yote hiyo? Acha Wizi wewe dada!!

CASHIER: wewe unadaiwa sh 8500 na Baba yako amesema unamlipia bili yake sh 230,000/=

Nikachoka kabisa!...By the way bado nipo hapa napiga Misamba....BABA umeniachia mateso mimi![emoji23][emoji23]
 
Hiyo Supermarket itakuwa ya kiswahili sana.

Haiwezekani wakampa mtu mzigo ambao haujalipia.

Labda ungechanganya bidhaa zako na za huyo baba ako badae mtenganishe baada ya kulipia zote kwa pamoja.

Hii ni chai ya wazi.
 
Hiyo Supermarket itakuwa ya kiswahili sana.

Haiwezekani wakampa mtu mzigo ambao haujalipia.

Labda ungechanganya bidhaa zako na za huyo baba ako badae mtenganishe baada ya kulipia zote kwa pamoja.

Hii ni chai ya wazi.
Ujinga kama huu unapatikana tanzania tu, alafu usikute kweli hapo kwanzia walinzi mpaka wasimamizi wamekomaa na jamaa ndio awalipe hiyo hela ya vitu alivyochukua huyo mzee.

Mitanzania mipumbafuu sana
 
Back
Top Bottom