Karibu sana Chalamila Dar es Salaam, sisi wanywaji wa bia tunakuunga mkono

Karibu sana Chalamila Dar es Salaam, sisi wanywaji wa bia tunakuunga mkono

Mmawia

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
122,494
Reaction score
96,074
Sisi wakaazi wa jiji la Dar es Salaam tupo tayari kukupokea na kukupa ushirikiano ndugu Chalamila.

Wana Dar es salaam tunaweza kuchangia mapato ya Serikali kwa kiulaini sana kupitia kupiga tungi a.k.a gambe. Unaonyesha utaiweza sana Dar es Salaam kwani wana Dar wengi wao ni wanachama wenzako na wanafuata falsafa zako za kunywa sana bia.

Karibu sana mwenyekiti mtaafu wa CCM.

 
Jamaa anakwambia walokole waliwahi kwenda kwake kulalamika bar zinawapigia kelele, nae akawaambia hata walevi nao waliwahi kuja kwangu kulalamika mnawapigia kelele kwa mikesha yenu!.

Mwishowe akairudisha kesi kwao, yeyote anayeweza kumbadilisha mwenzie na afanye hivyo, kama mlokole ukiweza kumshawishi mlevi aache pombe kazi kwako, na kama mlevi ukiweza kumshawishi mlokole akufuate bar shwari tu..

Chalamila ni genious.
 
Shida kubwa wenye bar wanataka wawe disco na hapo hapo ukumbi wa rhumba. Na kibaya zaidi wako kwenye maeneo ya makazi na hizo establishment zao ziko wazi, hazikidhi vigezo vya disco au dancehall

Cha msingi,,wafuate masharti ya leseni za biashara zao
 
Tatizo ametetea pombe zaidi badala ya kelele
Huyu jamaa Kaletwa kwa makusudi hiyo tu
Apambane na NEMC sijui ?
Acha tuone kama kina msukuma ndio wamesukuma haya ili aje kuendeleza ujinga na kelele za usiku na mchana
 
Mioyo yetu iko kwake. Bia ina mchango mkubwa kwe uchumi. Nyerere aliwaomba makasisi, watumishi na vioongozi wa dini kunywa bia baada ya vita vya Iddi Amini / Uganda li kuokoa uchumi
 
Ile kampeni ya kupunguza makelele kwenye baa za uswahilini sijui kama zitaendelea maana walevi wamepata mtetezi mlevi mwenzao.
 
Ile kampeni ya kupunguza makelele kwenye baa za uswahilini sijui kama zitaendelea maana walevi wamepata mtetezi mlevi mwenzao.
Ndiyo maana tunamkaribisha sana jijini
 
Ukitaka nikuunge tuma aftatu kwa namba hii
IMG-20230516-WA0044.jpg
 
Back
Top Bottom