Karibu Tarime mama Kilango 2010

Karibu Tarime mama Kilango 2010

- Unajua inafurahisha sana tunapomng'ang'ania msanii na mbabaishaji, I mean kila kona ya JF ina Mama Kilango what a msanii? Je ina maana JF tumeshuka kiwango kiasi hiki cha kumjadili msanii mmoja tu kila kukicha?

- Uwanja mkubwa kama huu kumjadili kiongozi mmoja tu tena mbabaishaji na msanii, tena ni mbunge tu mbona naona kama tunamjenga sana, au?

Respect.

FMEs!
 
FMEs! hakikaumenena nadhani hapa si suala la kumjadili ila hebu kweli mama Anna Kilango anaweza kuwa hana uzalendo kwa kiasi hicho? kufikiri kuuangamiza upinzani kwa mbinu chafu si swala la kiungwana hata kidogo.

Siku zote sikuwahi kumsikia akipiga vita yoyote pale mjengoni , ila tangu hawa ndugu zetu walipoanzisha vita hiyo sasa imegeuka imekua yake.
Nahdani sasa kama ataweza ajiulize kwanza .
 
Haya ni matatizo ya kuingia vitani bila kujua adui ni nani? Kama wachangiaji wengine walivyosema kwamba kama yeye ni mpango wake kuhakikisha kwamba wapinzani wanaondoka bungeni, kwanza yeye ni mtu mdogo sana kufanikisha hilo kwa sababu alishawahi kuahidi mambo ya Richmond yasipowekwa sawa bungeni hakutakalika, mbona hatuna tatizo lolote la viti pale bungeni na watu bado wanakaa vizuri tu, wakiwemo hao mafisadi wenzake.

Hao wote ni wachumia tumbo tu, msingi wa kelele wanazopiga ni ili maisha yaendelee, kwani angekuwa mtu makini kama alivyowaaminisha watanzania wengi angeamua kuondoka baada ya kuona mambo mengi anatofautiana na chama chake. Hajafanya hivyo na badala yake anataka wapinzani waondoke bungeni wabaki peke yao na bunge la chama kimoja ili watumalize kimyakimya.

TANZANIA BILA VIONGOZI WAZUSHI INAWEZEKANA.
 
Mie nilisha wahi kusema kwamba CCM hakuna mpambanaji wala mpiganaji . Nilitegemea Wapinga mafisadi wa CCM ama wapambanaji wangalikuwa wanaombea Upinzani uwe na wabunge wengi Bungeni ili Bunge liwake moto na kuibana serikal juu ya maendeleo ya watanzania na kupinga rushwa kumbe hakuna kitu .
 
Lunyungu; Ni kweli mkuu hapo ndipo mwenye akili hana haja ya kuumiza kichwa , haka ni kamchezo ka kitoto, "jifiche nisikuone!!!" kumbe nguo ya mtoto mwezie inaonekana , tena ina rangi myeupe.

Lunyungu; siku zote mimi husema siku za kufanya mabadiliko huenda zikaanzia kule Mara, ambapo moja(1) ni moja na si tatu(3) napata shida sana kuwajua wanasiasa wetu wa leo.

Lunyungu; Unamkumbuka Mtikila? alikwenda na yale anayoyaamini huko nadhani majibu unayo .

Mungu ibariki Tanzania

Mungu inusuru Tanzania na hawa wajanja wa siasa.
 
Kweli sasa tutaona wale majemedari wa CCM wakizunguka huko na huko kwa ajili ya kuua upinzania sio ajabu maana wanachofanya wao ni kwa ajili ya mkate wao wa kila siku
 
Back
Top Bottom