Karibu tushirikiane kuendesha NGO's

Karibu tushirikiane kuendesha NGO's

- Andaa JINA la shirika.
1. Andaa Katiba (3 copies)
2. Muhtasari wa mkutano wa wanachama kupitisha hiyo Katiba kwaajili ya usajili. (miongoni mwa wanachama mchague Mwenyekiti, Katibu, na Mtunza Hazina)
3. Endorsement list ya wanachama wote. Yaani jina na saini.
4. CV na picha passport size mbili za kila Kiongozi. Wale viongozi watatu I.e M/Kiti, Katibu, na Treasurer (mtunza hazina).
5. Jaza Form maalumu ya usajili. (Form hii unaipata kwenye taasisi unayotaka kwenda kusajili au idownload kwenye website yao).
6. Barua ya approval kutoka kwa Afisa Maendeleo Jamii wa Kata. Yaani kwenye Kata husika ambapo mtaweka office ya shirika.
7. Barua ya approval kutoka kwa Afisa Maendeleo Jamii wa Wilaya. Yaani kwenye Wilaya husika ambayo mtaweka office ya shirika.
8. Ada ya usajili. Sikumbuki the exact amount, ila ni around Tsh 100,000 hivi kwa mwaka, for national/countrywide coverage.
9. Kisha pelekeni kwenye taasisi ya usajili.

N.B: Taasisi za usajili zipo kadhaa na kila moja ina sheria yake na requirements/taratibu zake. Kuna BRELA (under the Companies Act). Kuna Wizara ya Mambo ya Ndani (under the Societies Act). Kuna Wizara ya Maendeleo ya Jamii (under the NGOs Act). Pia kama sikosei kuna RITA (under the Bodies & Trustees Act).

So, hizo items hapo juu (1 to 8) ni registration requirements under The NGOs Act, at Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto. Pia ni vizuri zaidi mkaiangalia hiyo sheria (The NGOs Act) inapatikana online, just to get assured on the mentioned requirements for registration.
The registration under The NGOs Act, national coverage ni Tanzania Mainland only. Kwamba hamtaweza kufanya any project or activity in Zanzibar.

Wish you all the best of luck katika kuwahudumia hao watoto yatima. Mungu awabariki.

-Kaveli-
Asante sana Mkuu tutayazingatia yote
 
Back
Top Bottom