Karibu umalizie nyumba kwa mkataba kisha uhamie. Nahama kikazi

Hongera
 
Sawa Faana
Asante sana kwa maoni yako.
Ila mimi nahitaji amalizie mwenyewe kisha ndio tuje kupigiana mahesabu
Ata inflate gharama za materials na ufundi ili gharama iwe kubwa akae muda mrefu, labda utafute fundi wako mwaminifu na duka la mtu wa karibu nawe atakapochukua materials ili mwisho wa siku uwe umetumia gharama halisi unayoijua
 
Hadi kufikia hapo maumivu ya ujenzi ndo huwa yanaanza sasa, japo tayari umeshayaonja kwenye blundering, kupaua , na hizo frame za madirisha na milango
Kabisa.
We acha tu
 
Ata inflate gharama za materials na ufundi ili gharama iwe kubwa akae muda mrefu, labda utafute fundi wako mwaminifu na duka la mtu wa karibu nawe atakapochukua materials ili mwisho wa siku uwe umetumia gharama halisi unayoijua
Ohhh, hapa sasa ndio nimekuelewa kwa umakini mkuu.
Asante sana
 

Nina kijana anasimamia mradi wangu Dodoma, Kama utakubali nimalizie master bed room completely aamie hapo akuangalizie nyumba yako mpaka utakapokuwa tayari kupajenga taratibu!

Mamikata na watu kumalizia Nyumba ya gharama yaweza Kuwa lawama huko mbele, sikushauri!

Na Mimi nitakupa hela umalizie Kama wewe then tutakuwa na mkataba wa kukutunzia tu nyumba yako!

I love Ndachi
 
Kama utafikia hatua ya kuhitaj familia ya kukaa Kwa Kodi kidogo au bure kukulindia nyumba itakuwa Bora zaidi.

Nina family friend alikumbana na changamoto za dunia now anajitafuta hivyo anaweza kuwa msaada.

Family hii ni mtumishi wa umma.
 
Madame B hiyo nyumba cha kufanya usiwe na haraka nayo kwa stage ambayo umefikia unaweza ukafanya ujenzi wako taratibu bila kuwa na bugudha na mtu cha kwanza kabisa tafuta mtu wa kuweza kukaa na kukulindia hapo 2:anza kuiboresha kwa awamu kama utaanza na plaster ndani ndo uje umalizie njee pia sawa 3:hakikisha utakapo kua unachukua material uwepo na kusimamia walau hata siku 2 sio mbaya,au upate mtu mwaminifu wa kusimamia kazi ifanywe kwa ubora ……………
 
Sawa, yote inawezekana.
Na itakuwa vyema sana kama hilo litawezekana.

Ndachi pazuri mno.
Pana hali ya hewa nzuri sana.
Karibu sana tuwasiliane mkuu.
 
Kama utafikia hatua ya kuhitaj familia ya kukaa Kwa Kodi kidogo au bure kukulindia nyumba itakuwa Bora zaidi.

Nina family friend alikumbana na changamoto za dunia now anajitafuta hivyo anaweza kuwa msaada.

Family hii ni mtumishi wa umma.
Sawa yote inawezekana kwa makubaliano maalum.

Pia mpe pole sana kwa changamoto zilizompata.
Mimi niko hapa kwa ajili yenu.
Yote inawezekana.
 
Asante sana mkuu.
Nashukuru sana kwa ushauri.

Ndio, ila mimi kwa kuwa nahama kikazi nadhani jukumu la kusimamia huku na kule naona kama kichwa kitavurugika tu.
Ndio manaa nikaona ni heri nipate wa hivo kabla option ya kuuuza haijanitawala.

Wazo lako ni zuri mno Kasongo Yeyee na nitalifanyia kazi.
Shukrani sana mkuu
 
Kuwa makini na watu wa kuwaachia walinde nyumba. Wengine wanapuliza hadi unaisahau nyumba yako 😆😆😆
Yaani ndio nilikuwa naambiwa hapa kwenye huu uzi.
Ila binadamu si watu kamwe!!!
Inatia huruma sana.
 
Vipi ukiniuzia moja ka moja?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…