Karibu upate uyoga mbichi na mkavu

Bei iko juu kwa mkavu maana supermarket g50 ni elf 5 napenda sana hiyo kitu
 
Alafu nyie walima uyoga mnatakiamtafute mbinu ya kushusha gharama za uzalishaji kama zipo juu na pia kushusha Bei. Uyoga ni substitute product ya nyama, maharage na karanga. Na kwenye nyama hapo kuna nyama ya mbuzi, kuku, Nguruwe na Ng'ombe. Sasa kwa hiyo bei yenu ya Shillingi Elfu kumi kwa gram 100 mnaona mpo sahihi!? Kwanini msije fanya upembuzi yakinifu na mje na bei ambayo Middle Class wataimudu bila shida na wakisha zoea na kufanya uyoga kuwa sehemu ya mlo wao ndio muanze kupandisha kidogo kidogo.
 
Hata Mimi nimeshawahi kulima Uyoga. Bei inaweza kupungua iwapo italimwa kwenye large scale. Lakini kwenye small scale haiwezekani ikawa ndogo. Kinachosababisha watu washindwe kulima large scale sababu hakuna soko LA uhakika sana kutokana na uelewa mdogo wa watu wanaotakiwa kuwa soko. Kingine thamani ya kitu inatokana na ubora wa kitu chenyewe kulinganisha na kingine kinachoshindana nacho (substitute). Uyoga huandaliwa katika mazingira ya umakini mkubwa kiasi kwamba kosa moja hasara yake ni kubwa sana ndio maana being huwa Juu kwa kiwango hicho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…