Al gator
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 1,029
- 565
Asante kwa kunijibu na kunielewesha. Shida ya wakulima wa tz wanaishi kama Yatima. Serikali haijigusi wala haiwasaidii kwenye kitu chochote hadi pale wanapo taka kuingiza pesa, Soko la uyoga lipo juu sana kwenye mataifa ya Asia na Ulaya na pia kama serikali ingefanya kampeni walau ndogo ya kuhamasisha watu kula uyoga basi hali ingekua nzuri kidogo. Bila serikali kuingilia kati kwa kuzishirikisha wizara ya kilimo, wizara ya viwanda na Biashara na wizara ya mambo ya nje wakulima watabakia kuwa ma peasant (small scale farmers)Hata Mimi nimeshawahi kulima Uyoga. Bei inaweza kupungua iwapo italimwa kwenye large scale. Lakini kwenye small scale haiwezekani ikawa ndogo. Kinachosababisha watu washindwe kulima large scale sababu hakuna soko LA uhakika sana kutokana na uelewa mdogo wa watu wanaotakiwa kuwa soko. Kingine thamani ya kitu inatokana na ubora wa kitu chenyewe kulinganisha na kingine kinachoshindana nacho (substitute). Uyoga huandaliwa katika mazingira ya umakini mkubwa kiasi kwamba kosa moja hasara yake ni kubwa sana ndio maana being huwa Juu kwa kiwango hicho.
Altenativu ya hapo ni kwa wakulima kuwa na umoja but its too bad tokea tukiwa Primary school tunafundishwa ubinafsi na kutokushirikiana.