Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
yah yuko sahihi watu wamepiga sana hela na kuchezea pia helaHapa umetupiga kamba mkuu,hakuna mtu anayetafuta pesa ya halali kwa jasho lake kisha aende kuzigawa hovyohovyo kwenye bendi.
Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
aina gan??Nauza gari
Ukilenga magari ya Zambia vipi process ya kuipitisha mpakani hadi ifike Bongo ikoje?na kuisajili haina mlolongo mrefu?Biashara yoyote mtaji ni nguvu yako tahadhari kubwa uielewe biashara yenyewe na uipende lakini uifanye kwa uaminifu na ukikua kimtaji unaweza kwenda kulenga gari bei chee hadi zambia, malawi maana huko hua wanajiuzia magari bei chee tu, kikubwa tahadhari na umakini mkubwa unaelenga ist hauwezi kulingana na anaelenga greda au skaveta,
Usibishe ndugu hayo mambo yapo sana mimi binafsi ni shuhuda wa hayoHapa umetupiga kamba mkuu,hakuna mtu anayetafuta pesa ya halali kwa jasho lake kisha aende kuzigawa hovyohovyo kwenye bendi.
Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
Karibu zipoMm nataka niwe nalenga magari ya mnada ya serikali. Una hio mifumo?
Haya magari ya Malawi na Zambia ushuru hauhusiki? Na je ukiweka ushuru yatakulipa?Biashara yoyote mtaji ni nguvu yako tahadhari kubwa uielewe biashara yenyewe na uipende lakini uifanye kwa uaminifu na ukikua kimtaji unaweza kwenda kulenga gari bei chee hadi zambia, malawi maana huko hua wanajiuzia magari bei chee tu, kikubwa tahadhari na umakini mkubwa unaelenga ist hauwezi kulingana na anaelenga greda au skaveta,
Ukiona mishe unayofanya hamna polisi anapitia ujue hutengenezi pesa,, 😂😂😂 mimi na mwanangu milandu tukasema tupoint magari tuuze, gari ya kwanza sprinter tumeenda kuipoint mkuranga mbagala mbele mbele huko milion moja na lak 9. Tatizo la kwanza tu tunarudi tukasema embu tukipandishe kasprinter fly over uhasibu tuone....😂😂..... stori yake iliishia pale pale.Hii biashara pia jitahid usiwe muoga wa kwenda polisi maana unaweza ukashikishwa gari muda wowote ukaingia lockup cha msingi hakiki documents kabla ya kununua
😂 Yaliwapata yepi?Ukiona mishe unayofanya hamna polisi anapitia ujue hutengenezi pesa,, 😂😂😂 mimi na mwanangu milandu tukasema tupoint magari tuuze, gari ya kwanza sprinter tumeenda kuipoint mkuranga mbagala mbele mbele huko milion moja na lak 9. Tatizo la kwanza tu tunarudi tukasema embu tukipandishe kasprinter fly over tuone....😂😂..... stori yake iliishia pale pale.
Kipi kilitokea tupate kujifunzaUkiona mishe unayofanya hamna polisi anapitia ujue hutengenezi pesa,, 😂😂😂 mimi na mwanangu milandu tukasema tupoint magari tuuze, gari ya kwanza sprinter tumeenda kuipoint mkuranga mbagala mbele mbele huko milion moja na lak 9. Tatizo la kwanza tu tunarudi tukasema embu tukipandishe kasprinter fly over uhasibu tuone....😂😂..... stori yake iliishia pale pale.
Gari utazipata ila kuziua kazi unayo, wateja wote wanaokuja njaa kali wanakuja na hela kidogo hupati faida uliyojipangia, lazima iwe chini ya matarajio yakoHabari
Kwa majina naitwa Jerry na ninajihusisha na uuzaji wa magari used nikiwa kama dalali kwa muda mrefu ndani ya Dar es Salaam.
Leo ningependa kushare nanyi kuhusu biashara hii ya magari hasa used hapa Dar es Salaam, biashara ambayo ina faida kubwa ambayo wengi sana bado hawajaijua.
BIASHARA HII INAFANYIKAJE?
Biashara hii hufanyika kwa mtu(mfanyabiashara) kutafuta gari na gari hizi mara nyingi hupatikana kwa watu wenye shida, bima na taasisi za mikopo na bank.
Kwa mfano gari aina ya ist inaweza kuwa na changamoto ndogo mathalani ya shilingi 300k mpaka muda mwingine 1m na gari hiyo husika inauzwa na mmiliki kwa gharama za shilingi 6m, wakati thamani husika ya hiyo gari sokoni ni 11 au 10m ukitoa ile 7m unabakia na kama 4m au 3m ikiwa kama faida ya gari husika.
Mara baada ya mfanyabiashara kuipata gari husika, gari ambazo huitwa za kulengwa kwa jina maarufu, then huchukua gari hiyo na kuiweka sokoni kwa bei ya faida, mara baada ya kuiuza hutafuta nyingine na kazi huwa inafanyika hivyo.
JE KAZI HII INACHAGUA JINSIA?
Jibu ni hapana kazi hii inaweza kufanywa na mtu yoyote au mwanaume au hata mwanamke.Na ni biashara ambayo haitumii mda mrefu sana ni kitendo cha kukubaliana bei na mteja na biashara kufanyika.
GARI HUPATIKANA VIPI.
Kama nilivyosema hapo awali kuwa gari hizi za kulenga huwa zinapatikana kupitia watu wenye shida ya hela,taasisi za kifedha za mikopo,bima n.k,ili kuzipata gari hizo za kulenga unaweza kuzipata kupitia madalali wa kulengesha ambao huwa na connection na wamiliki wa gari husika.
MAMBO YA KUZINGATIA UNUNUAPO GARI,
Kama zilivyo biashara nyingine hii pia ni biashara yenye kuhitaji umakini na uzoefu hasa kwenye kuchagua gari nzuri ili upate kuiuza vizuri vile vile,bila kusahau kupiga hesabu sahihi endapo kama gari husika itahitaji matengenezo kwa kuwa na uzoefu wa spear husika .
KARIBU UWEKEZE KWENYE BIASHARA HII NAMI.
Nakukaribisha uje kuwekeza kwenye biashara hii kwa kutafuta gari na kuuza pamoja nami, Nitakusaidia kutafuta gari nzuri ambayo kupitia mimi nitatafuta wateja na kuiuza kwa faida nzuri.
Kinachofanyika baada ya kupatikana gari unaweza kuitumia gari husika/kubaki nayo ukiwa unaitimia wewe mwenyewe au unaweza kuiacha ofisini kwetu hadi pale mteja atakapotokea wakati huo ntakuwa naitangaza ukiaachilia mbali kuwatumia madalali ote wa magari ili nao waiuze,wakati huo documents zote ukiwa nazo mwenyewe mteja akifika unakuja nazo au tunakufata tunamaliza biashara.
Biashara hii haihitaji usimamizi wako labda kama utaamua mwenyewe sababu kuanzia kutafuta gari mpaka kuliuza mie ndo ntakayekuwa na pambana kwa maana hyo unaweza kuendelea kufanya kazi zako nyingine huku ukiendelea kufanya biashara hii ya magari.
Endapo kama utakuwa interested karibu tufanye biashara hii pamoja mie nipo magomeni na ni mzoefu wa hii biashara,endapo utakuwa tayari nakukaribisha japo katika faida ya kila gari ntakuwa nachukua faida ya 30%
Nikiwa na maana kam utabakia na documents na gari kunikabidhi basi gari hyo itabakia ofisini kwetu ambako tuna chama kabisa,ambako gjarama za parking na ulinzi wa gari zitakuwa juu yangu pamoja na hela ya mafuta ambayo wateja watakuwa wanakagulia itakuwa juu yangu pia,lakini gari ikishauzika mie ntakuwa nachukua 30% ya faida ile ambayo tutakuwa tumekubaliana,na ile 70% utabakia nayo wewe kama mmiliki,Karibu uwekeze kwenye hii biashara ambayo haina gharama nyingine yoyote na wala haikatwi kodi lakini yenye faida nzuri.
kwa mwenye kuhitaji anakaribishwa 0659756647 na mwenye maoni au kuhitaji ufafanuzi anaweza nitafuta au kuuliza hata hapa hapa
ahsanteni