#COVID19 Karibu Wakenya milioni moja wakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula

#COVID19 Karibu Wakenya milioni moja wakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula

Yoyo Zhou

Senior Member
Joined
Jun 16, 2020
Posts
126
Reaction score
215
Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) hivi karibuni ilitoa ripoti kuwa, mamilioni ya Wakenya wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula.

Kutokana na ripoti hiyo, tathmini zilizopangwa kufanyika mwezi Julai na Agosti zinatarajiwa kuthibitisha kuongezeka kwa hali mbaya ya usalama wa chakula, huku makadirio mengine yakionyesha watu milioni 3.5 wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula.

Katika maeneo ya mijini, inakadiriwa kuwa watu milioni 1.7 wanaoishi katika maeneo yasiyo rasmi wataathiriwa zaidi kutokana na janga la maambukizi ya virusi vya Corona lililopo sasa. Ripoti hiyo imeeleza kuwa, serikali ya Kenya na wenzi wake wametambua maeneo duni 725,000 mijini ambayo yameathirika zaidi na virusi vya Corona, ikiwemo Nairobi, Kwale, Kilifi, Mombasa na Nakuru, ambayo yanahitaji msaada.

Janga la COVID-19 limesababisha hali mbaya ya chakula kuwa mbaya zaidi, kwani wakulima hawawezi kufanya shughuli zao kutokana na hatua za udhibiti zilizowekwa katika nchi husika. Hivi sasa, ingawa inakabiliwa na uhaba wa fedha, OCHA inatoa msaada wa chakula kwa watu zaidi ya 390,000 nchini Kenya, pia inaendelea kugawa chakula katika maeneo ya Mandera, Wajir, Turkana, Garissa, Tana River, Marsabit, Isiolo, Samburu na Baringo.

Hivi karibuni, rais Xi Jinping wa China alitoa wito wa kuzuia vitendo vya uharibifu wa chakula, huku akisisitiza kuchukua hatua zenye ufanisi, kuzindua mfumo wa muda mrefu na kupinga kithabiti vitendo vya uharibifu wa chakula.

Tangu mwaka 2010, kiwango cha wastani cha nafaka kwa mtu nchini China kimeendelea kuwa juu kuliko kiwango cha wastani cha dunia. Mwaka jana, kiwango hicho kilifikia kilo 470 ya nafaka kwa mtu, ambacho ni kikubwa ikilinganishwa na kigezo cha kimataifa cha usalama wa nafaka. Kiwango cha kujitosheleza cha michele, ngano na mahindi kimezidi asilimia 97. Basi ni kwa nini rais wa China anaendelea kusisitiza kupinga vitendo vya uharibifu wa chakula?

Kwa sababu China ni nchi kubwa yenye watu bilioni 1.4, hivyo uharibifu wa chakula unaweza kuleta hasara kubwa, hivyo ongezeko la uzalishaji wa nafaka na kuzuia uharibifu wa nafaka ni njia bora za kuimarisha usalama wa chakula.

Ni ajabu kwamba China imetumia asilimia 7 ya eneo la mashamba duniani kulisha asilimia 20 ya watu wote duniani. Uwiano kati ya uzalishaji wa nafaka na mahitaji ya watu bado unakabiliwa na changamoto kubwa za usalama wa chakula. Kwanza, kufuatia utandawazi wa miji, wakulima wengi wanaenda mijini kutafuta ajira, huku idadi ya wakulima ikiendelea kupungua mwaka hadi mwaka. Pili, kiwango cha chakula kinachoharibika katika mikahawa kwa mtu nchini China imefikia asilimia 11.7.

Na tatu, kutokana na athari za maambukizi ya virusi vya Corona, janga ya nzige na maafa mengine ya kimaumbile, mgogoro wa nafaka duniani unaweza kuvuruga mnyororo wa uzalishaji wa nafaka hata katika nchi zenye rasilimali kubwa ya nafaka. Hivi karibuni, Umoja wa Mataifa ulitoa ripoti ikisema, nchi 25 duniani zitakabiliwa na hatari kubwa ya njaa, na dunia itakabiliwa na msukosuko mkubwa zaidi wa nafaka kuwahi kutokea katika miaka 50 iliyopita.

Ni jukumu la serikali za nchi mbalimbali duniani, hususan zile zinazokabiliwa na hali mbaya ya usalama wa chakula kubuni ama kutumia kilimo cha kisasa kuondoa hatari hiyo kwa wananchi wake. China imefanikiwa kudumisha utulivu wa chakula kutokana na maendeleo makubwa katika sekta ya kilimo kwa kufanya uvumbuzi na teknolojia muhimu, nchi nyingine hususan za Afrika zinaweza kuiga uzoefu wa China ili kukabiliana na hatari ya usalam wa chakula na kujenga jamii yenye afya bora.
 
Uncle kutoka UK atawaletea yellow corn kutoka USA, khe khe khe khe kheeee ndio raha ya lockdown.
 
Back
Top Bottom