Karibuni Lesotho (Maseru) tufanye biashara

Karibuni Lesotho (Maseru) tufanye biashara

Mleta mada maelezo yako mengi hayana ukweli; Textile industry Lesotho iko juu sana na material yao Seshoeshoe ambayo ni traditional; I know wadada wanapenda khanga na vitenge for a change but it cannot be a succesful business. Population ya hapo maseru inakaribia watu laki mbili, mzunguko wa hela ni mdogo watu wengi wanaishi kusubiri mshahara mwisho wa mwezi. hata machangudoa (wanaitwa crocodile) Maseru ni wa kuhesabika; Town hapo kuna Hoteli tatu tu za maana. kazi ambazo zinalipa walau ni Udaktari, Nurse, Waalimu - hasa ukiamua kukaa wilayani (milimani). Kenyans wamejaa wanafanya unesi na ualimu. Wacongo ndio doctors serikalini about 80% kwakuwa nchi ya Lesotho haina medical school wanasomesha watu wao Zimbabwe na south Africa na wengi wakimaliza hawarudi (south Africa inalipa vizuri madoctor ingawa ukilinganisha na Tanzania Lesotho wanalipa vizuri). Pia sio kweli kuwa wenyeji hawapendi kufanya kazi, but Wasotho waliosoma vizuri can easily be employed South Africa kwasababu wanaongea lugha moja upande wote wa jimbo la Free state na pia ni rahisi kujifunza kizulu. Wale wasiosoma Maseru hakuna misheni town wanaenda south africa migodini. But it is a nice city, calm na watu hawana noma na wageni.
Malezo mazuri haya hapa.
 
Back
Top Bottom