and 100 others
JF-Expert Member
- Feb 3, 2023
- 3,707
- 12,367
Hizo nchi inajulikana wananchi wao hawaogopi vyombo vya usalama, wapo tayari kupambana hata na wanajeshi au polisi pale wanapoona hawatendewi haki.
Kenya tumetoka shuhudia juzi hapa vijana wadogo wanaingia bungeni na kuchoma bunge.
Nilichogundua kumbe serikali nyingi za Africa ndizo chanzo cha kupelekea nchi hizo kutokuwepo na amani.
Kuanzia Kaskazini mwa bara Africa Egypt , Tunisia, Libya n.k magharibi Nigeria, Africa ya kati n.k hadi kusini Kenya n.k na wao walikuwa kama wananchi wa Namibia wapole, wanaheshimu vyombo vya dola, wanaogopa silaha za moto, vyombo vya dola vikadhani vinaogopwa, wakajiona miungu, wakajikuta wanaweza kufanya chochote kwa kukamata watu mchana kuwateka na kwenda kuwaua.
Kilichofuatia hakuna aliyeamini. Ukiona mtu mtaratibu mpole usifikiri unaweza mchokoza na kumpiga muda wote , ujue na yeye ana kikomo chake cha uvumilivu.
Kumbe hizo nchi watawala walijisahau wakidhani wanaogopwa matokeo yake ni machafuko makubwa.
Namibia ikiendelea na huu mtindo wa maisha kutokujali uhai na usalama wa raia na mali zao, kuwateka mchana kweupe na wakihoji viongozi wanatoa majibu ya kejeli, dharau na kutokujali, mi nasema Namibia itafika mnapopataka. Na ikifika huko itakuwa mmechelewa.
Nimeona watu kwenye social media wakianza kujadili ni silaha gani za kutembea nazo kwa sasa, hii si ishara nzuri.
Kama kuna waliofahamu na kufuatilia machafuko ya Tunisia, yaliyopelekea machafuko Egypt na hadi Libya, aliyeanzisha ni Mohamed Bouaziz, machinga wa mtaani, jamaa alijichoma moto kutokana na kusumbuliwa na kudhalilishwa na police kutoka udogoni mwake, kijana mwenye miaka 26, kitendo kilichopelekea machafuko yaliyopelekea mapinduzi nchini Tunisia na nchi zingine za kiarabu.
Hii ilipelekea rais wa Tunisia kutoka madarakani baada ya miaka 23 kwenye uongozi.
Hawa viongozi kuna muda huwa wanajisahau wanajikuta ni miungu.