Karibuni tujuzane kuhusu BMW 3 Series

Karibuni tujuzane kuhusu BMW 3 Series

Habari naomba kupata mawasiliano ya fundi wa ac wa benz c class 180, AC imenisumbua fundi akasema compressor imekufa tukabidili nilvyosafiri kuja Moshi. Hali ikaanza Tena AC inatoaa joto tu...naombeni msaada
 
Mimi nashangaa watu kukataa Bmw kama series 3 m3 sport 320i mbona affordable tuu mfano unazingatia service huna mizunguko mingi, rough road unaenda mdogomdogo shida ikwapi
 
Mimi nashangaa watu kukataa Bmw kama series 3 m3 sport 320i mbona affordable tuu mfano unazingatia service huna mizunguko mingi, rough road unaenda mdogomdogo shida ikwapi
1. Unachanganya M-3 na M-Sport.
2. Kama unaongelea E90 (2005 hadi 2013) nashauri 6 cylinders, yenye N52 engine, (323i kuja juu) kama 4 cylinders ukipata diesel (ngumu sana kupata)
3. Kwenye service upo sahihi.

Unajua kwanini watu wanasema kumiliki ni ngumu, sio issue ya reliability, ni issue ya cost of ownership.

Nenda kwa Azizi Umeme, badirisha oil ya 323i ya 2007 afu mwingine aende Total na Crown ya 2007 abadirishe oil, au nunua plugs zote 6, au nunua coils zote 6.
 
Wakuu Habari.

Leo nilipenda tujuzane kidogo kuhusu BMW 3 Series. Kila mtu aliewahi kumiliki au kuendesha au ata kama kuna fundi aweze kutupatia Experience yake kidogo kuhusu hizi gari. Hii itawasaidia waliokua na wazo la kununua hizi gari au wamiliki waweze kupata mwongozo zaidi.

Mi nitaanza kidogo na Historia ya BMW 3 series.

Hadi sasa 3 Series imeshatengenezwa katika generations (models) 6 ambazo ziko sokoni, E21, E30, E36, E46, E90, F30 na Model ya 7 ni G20 ambayo itaanza kua sokoni 2019. BMW 3 Series zinakuja kwa bodystyles 5 ambazo ni Sedan, Couple, Hatchback (hii sio common sana), convertible na wagon. Pia zina engine size tofauti tofauti kuanzia cc za chini (1500cc) hadi za juu (4000cc), zipo cylinders 3-inline, 4-inline, 6-inline na v8, na zipo petrol, diesel na hybrids models, pia turbo na non-turbo, na zipo special editions zenye package ya ///M Sports. Pia kuna manual na Automatic gearbox.

Kwa leo ningependa tuongelee Model tatu tu ambazo ni common, E46, E90 na F30.

E46

Nadhani hii ndio BMW 3 Series common zaidi Tanzania, na ndio moja kati model ambayo watu wengi duniani wanaisifia kuanzia durability na driving experience. Ukiwa una search kwenye website za kuuza magari, hawatakuambia hii ni E46, ila utajua kwa mwaka uliotengenezwa. E46 ilitengenezwa kuanzia 1997-2005, ikapokelewa na E90.
Mara nyingi tunakutana nazo E46 ambazo ni 318i zenye engine ya N46B20 au N42B20 zote ni 4 Cylinders.

View attachment 879995
Ukitaka kununua E46 nashauri ununue kuanzia mwaka 2001 kwenda mbele, kwakua BMW wanatabiia ya kuboresha 3 series kila baada ya miaka mitatu (LCI aka Facelift) kwa kurekebisha vitu vidogo vidogo kuanzia muonekano na perfomance.
Kwenye website za kuuzia magari, CIF ya E46 ni kati ya Million 5 hadi 7 na kuendelea kutegemeana na hali ya gari.
Ushuru wa TRA kwa E46 utakua kati ya Million 6 hadi Million 8 hivi kutegemeana na umri wa gari, engine size na aina ya mafuta.

E90
Kutokana na watu wengi sasa kupenda luxury cars, BMW wakachange uelekeo na kuanza kutengeneza magari luxury zaidi kutoka E46 ambayo ilikua na muonekano wa "kigumu". E90 zilitengenezwa kuanzia 2005 hadi 2012 na ni kubwa zaidi, luxury, na ipo technological advanced zaidi ya E46.


View attachment 880000
E90 zipo zenye body tofauti tofauti pia. Kuna E90 sedan, E91 Touring, E92 Couple na E93 Couple. Wewe tu unachopenda.
Engine size zipo za ukubwa kuanzia cc1600 hadi 4000 na kuna 4 Cylinders 6 cylinders na V8 pia (///M version).
Ni gari nzuri sana kwa muonekano, nje na ndani, pia perfomance yake na fuel economy iko vizuri. Usidanganywe na ukubwa wa engine, ulaji wa mafuta upo vizuri tu.

Ukitaka kununua hii E90 nashauri ununue kuanzia mwaka 2009 kwakua ndio LCI Facelift ilifanyika kwa kuboresha zaidi hii gari. Pia kuna maneno maneno kua 320i ambazo ni 4 Cylinders (zina engine N46B20s)ni worse model ya hii generation. Kwahiyo watu wengi wanashauri ununue 6 cylinders (mfano 325i, 328i, 330i etc) ambazo zinatumia engine ya N52, N53. Pia Turbo models N54 na N55 i6 watu wanazipinga wanasema zina matatizo.

Kwa Tanzania tunakutana sana na 320i ambazo zina run smooth tu na hazina shida, so hayo maneno ya watu sio ya kuyapa kipaumbele sana.
**watu=Wachangiaji mbalimbali katika forums mitandaoni, sio lazima wawe Watanzania.

Challenge kubwa ya hii gari ni:
- Water pump. Sijui BMW waliamkaje wakaanza kutumia electric water pump na wakaachana na mechanical. Aisee hivi vidude vinakufa sana after 70,000 km to 80,000 km. Na inauzwa kwenye Tsh 800-Milion na ukinunua na thermostaat yake kama laki 3.

-Kuvuja oil. Kwasababu imetengenezwa kwa plastic sana, oil kuvuja ni kawaida.

-Kwa sababu ya umeme sana, kuwaka waka taa ni kitu cha kawaida, kwahiyo better ukawa na diagnosis machine yako kabisa.

Ila ni moja ya fun car kuendesha, mfano ukapata E90 BMW 325i au 330i, Sport Package, dah.

CIF ya hii gari ni Mill 9 na inaweza kufika hadi Mil 14 kwa base models, ila ukitaka zenye mbwembwe zaidi uta pay zaidi.
Ushuru wa hii unaanzia Million 9 na unaenda hadi Million 13. Itategemeana na sababu mbalimbali.

F30
Hii ndio current generation ya BMW 3 series hadi leo tunavoongea hapa. Ni maboresho ya kila makosa na mapungufu yaliyowahi kujitokeza katika magari yaliyopita. Liko perfect! F30 ni sedan, F31 ni Touring/Estate wagon, F34 fastback na F35 ni sedn ila ina long wheel base.
F30 zimeanza kutoka 2013 hadi leo, tunategemea zitapokelewa na G20 kuanzia mwakani 2019.
F30 zote ni turbo charged, na hapa BMW wali introduce hadi 3 cylinders na hawajawahi kuweka F30 yenye V8 ata M sports Model. Pia katika F30 ndio wali introduce plug-in-hybrid ya kwanza katika 3 series mwaka 2016.

View attachment 880023

Kama uchumi sio tatizo, ni gari zuri la kununua. Especialy XDrive na turbo walivozi equip, vimefanya kuendesha gari iwe starehe zaidi. Na Facelift/LCI ilifanyika kuanzia models za 2015 na walifanya maboresho zaidi katika technology, perfomance na muonekano.
F30 ina trim (lines 3) kuna base-line, sports, na luxury kutegemeana na matakwa ya mteja.

Ushuru wake umechangamka sana inafika hadi Mill 15 na CIF zake pia ni above Mil 16.


HITIMISHO
Nimeandika kwa ufupi ila nategemea wadau wataongezea na kwingine watanikosoa. Kwa kukumbushana tusiwe na uwoga kwamba BMW cars ni kichefu-chefu, kwamba zikianza kuharibika zinasumbua. Ni kweli, ila pindi ukiifanyia service ipasavyo, na kwa wataalamu waliobobea, hautaona likisumbua sumbua.

Kuna mdau Mshana Jr alianzisha Uzi hapa ukiwataka kubadirisha mtazamo juu ya BMW na wadau mbalimbali walichangia mawazo yao na ushuhuda, unaweza kuupitia ukajifunza zaidi.

Karibuni.

View attachment 1991027
1719330780578.png

hii gari ni moja kati ya gari za bei rahisi sana hata ukitafuta mtandaoni, one of the cheapest car to buy but is very expensive to maintain it.

Hizi gari hata mjerumani mwenyewe anaziogopa mjapani anaziogopa anauza bei ya kutupa aepukane na mabalaa yake. FOB ya gari ni dola 800, bei ya kuifikisha bongo ni dola 2500. bei ya hiii gari ni sawa na bei ya iphone 14 used ...

Ukipiga safari ya Posta mpaka vikindu na hii gari lazima taa ya check engine iwake. Ghaaiiii sheeeeeilaa 😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom