safi mkuu,
swali:
mimi nina approach 40 yrs, nimekutana na rafiki zangu niliosoma nao na kufanya kazi miaka ya 25-36 kwakweli nimestaajabu baadhi wameanza kuchoka; vitambi, sura inazeeka, wengine pombe sana sura zimeisha, wengine mara waseme miguu imevimba, wengine wanachagua vyakula.(ila sio wote maana ilikuwa msibani). sasa daktari kupitia uzi huu naomba utupe njia ya kuishi ili kwa kula nini na kuishi mfumo upi ili tusizeeke. wenzetu china na western europe wanaishi sana kwanini???
Ahsante sana kwa swali lako. Its a very broad question, but i will try my best.
-Pata mlo uliokamilika yaani uwe na virutubisho vyote kama wanga,protini,mafuta,vitamins na madini kwa uwiano sahihi... Na hii wala si gharama kama wengi tunavyodhani;katika mlo wako hakiksha unapata mboga za majani na matunda kwa wingi kuliko vyakula vya wanga(wali/ugali)!! kwa wabongo wengi tunakula kinyume na inavyoshauriwa kiafya, i.e ugali mkubwa mboga kidogo;unatakiwa ule kwa mfano ugali robo sahani-robo tatu iliyobaki ujazie mboga za majani, nyama/samaki/dagaa/maharage, na
matunda.
-Pia tuepuke nafaka iliyokobolewa(sembe) na badala yake tupendelee dona zaidi.
-Wakati wa asubuhi(kifungua kinywa) ndo kinatakiwa kiwe kizito zaidi,halafu mchana unapunguza kidogo, na jioni unakula kidogo zaidi(usile chakula baada ya saa moja usiku!!)
-Tuepuke kabisa pombe,sigara,vinywaji vya makopo kama soda na juice za viwandani. Badala yake tunywe zaidi maziwa,juice za matunda(sio za viwandani).
-Chakula tunachopika tuepuke sana kuweka mafuta mengi ya kupikia(kwa siku moja kiafya unatakiwa usizidishe kijiko kimoja cha chakula cha mafuta ya kupikia!!!!) Ni vizuri pia kupikia kwa mafuta ya mimea(kama alizeti) kulikoya wanyama;pia tupendelee zaidi vyakula vya kuchemsha na kupunguza vyakula vya kuunga.
-Tuepuke vyakula vya kukaanga kwa mafuta.
-MAZOEZI- Ni muhimu sana kuhakikisha kila siku tumepata angalau dakika 30-45 za kufanya mazoezi ya viungo mpaka kutoa jasho!!