Karim Mandonga Mtu Kazi azawadiwa gari

Karim Mandonga Mtu Kazi azawadiwa gari

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Bondia Mtanzania Karim Mandonga amekabidhiwa gari aliyoahidiwa endapo angeshinda pambano lake nchini Kenya, amepewa zawadi ya gari hilo aina ya Nadia na Mfanyabiashara Dick Sound bila mashariti yoyote ikiwa ni sehemu ya kutimiza ahadi aliyokuwa ameahidiwa endapo angeshinda pambano hilo.

C572C5CF-DD89-4AD7-85D6-6E9960F0905B.jpeg

Tukio hilo limefanyika leo hii katika Ofisi za DickSound Mall @dicksoundmall maeneo ya Magomeni Dar es salaam ambapo Dick amesema “Nimempa kama zawadi siyo kwa ajili ya Ubalozi, alikuja kwangu wakati anaenda kupambana nikamuahidi akishinda nitaweza kumpa gari, wakati akiwa Kenya nikaona video nikamtumia kumwambia umeniangusha ushapigwa, akasema hapana sio kweli Mimi ndio napanda kupambana, hivyo leo tumemkabidhi kumpongeza na kutimiza ahadi”

Kwa upande wa Mandonga “Namshukuru sana DickSound Kwa hili leo ndoto yangu imetimia, Mandonga anaondoka na usafiri Mungu mkubwa
 
Toyota Nadia ni gari ya kumpa mtu kweli in 2023? Nadia ilikuwa discontinued in 2023 maanake huwezi kupata Nadia ambayo haina miaka zaidi ya 19 at least. Hili gari bora akalitupe azawaizi ni tripu za shamba, gereji, shamba, gereji
Matatizo ya akili ndio haya sasa. Wewe unataka apewe RANGE ROVER NEW MODEL?
 
Bondia Mtanzania Karim Mandonga amekabidhiwa gari aliyoahidiwa endapo angeshinda pambano lake nchini Kenya, amepewa zawadi ya gari hilo aina ya Nadia na Mfanyabiashara Dick Sound bila mashariti yoyote ikiwa ni sehemu ya kutimiza ahadi aliyokuwa ameahidiwa endapo angeshinda pambano hilo.

Tukio hilo limefanyika leo hii katika Ofisi za DickSound Mall @dicksoundmall maeneo ya Magomeni Dar es salaam ambapo Dick amesema “Nimempa kama zawadi siyo kwa ajili ya Ubalozi, alikuja kwangu wakati anaenda kupambana nikamuahidi akishinda nitaweza kumpa gari, wakati akiwa Kenya nikaona video nikamtumia kumwambia umeniangusha ushapigwa, akasema hapana sio kweli Mimi ndio napanda kupambana, hivyo leo tumemkabidhi kumpongeza na kutimiza ahadi”

Kwa upande wa Mandonga “Namshukuru sana DickSound Kwa hili leo ndoto yangu imetimia, Mandonga anaondoka na usafiri Mungu mkubwa
Mimi na masters yangu natembelea Boxer BM 150 kweli mungu sio juma nyosso🤣
 
Muda wake wa kupiga pesa, akituliza akili atakuwa mcharo, akizuzuka na pesa za ghafla na umaarufu, majuto ni mjukuu.
Hamna fedha yoyote ya kupiga hapo. Ukiwa pembeni unaweza kudhani wanapata sana fedha lakini ukweli ni fedha za mbuzi tu. Na wamepita wengi
Dr. Shika, Pierre Liquid...... Tena umaarufu wake unapoisha anarudi kwenye hali mbaya zaidi.
 
Back
Top Bottom