Karim Seleman 'Chiba' akielezea mkasa wake ulipelekea akatwe mguu

Karim Seleman 'Chiba' akielezea mkasa wake ulipelekea akatwe mguu

X_INTELLIGENCE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2014
Posts
10,400
Reaction score
14,339
"Baada ya kuona maisha yamekuwa magumu niliamua kukimbilia kwa baba aliyekuwa anaishi Lindi ambapo alinipeleka gereji kujifunza ufundi wa magari. Nilikuwa na ndoto nyingi kupitia ufundi huo lakini ikatokea siku moja ambayo siwezi kuisahau maishani mwangu kwani ndiyo ilifuta ndoto zangu japo namshukuru Mungu kwa kila jambo.

Nakumbuka ilikuwa mwaka 2014 nilitoka nyumbani kwenda stendi ya mabasi ya Lindi katika kijiwe nilichozoea kupiga stori na washkaji. Wakati nikiwa kijiweni hapo kuna mama mmoja anayeitwa Mama Royal alikuwa akigeuza gari lake. Kwa bahati mbaya badala ya kukanyaga breki, alikanyaga mafuta na gari lilirudi nyuma kwa kasi na kunivamia ambapo lilinijeruhi mguu.

Nilikimbizwa hospitali ya Sokoine kwa matibabu ambapo nilifungwa plasta gumu (P.O.P). Pamoja na kufugwa hogo lile, nilijisikia maumivu makali hadi kumlalamikia baba aliyenitaka kuvumilia hadi siku niliyopangiwa kurudi hospitali.

Mguu wavuja damu na kujaza beseni.
"Siku moja baada ya kufungwa hogo nilipata maumivu makali na hogo likaanza kulowa damu kadri siku zilivyosonga mbele. Ilifika wakati damu hiyo ilijaa beseni. Hali hiyo iliwaogopesha wazazi wangu hivyo wakaamua wanirudishe hospitali ambapo daktari alipofungua hogo alikuta mguu umeanza kuoza. Daktari alinisafisha mguu na kuuacha bila kuufunga kwa siku 3 lakini hakukuwa na mabadiliko kwani damu ziliendelea kuvuja.

IMG_0948.JPG

AKATWA MGUU NA KUBATIZWA JINA JIPYA

"Kutokana na maumivu makali, nilijikuta napoteza fahamu mara kwa mara. Kuna siku nilizinduka kutoka kwenye kuzimia, daktari akaniambia kuwa wameshauriana na wazazi wangu na kuamua kunikata mguu. Ama kweli hujafa hujaumbika, kwani hapo ndipo nilipobadilishwa jina kutoka Karim Seleman na kuitwa Chiba tofauti na jina nililopewa na wazazi wangu".

Nukuu ya dansa wa Yamoto Band, Karim Seleman 'Chiba' akielezea mkasa wake ulipolekea akatwe mguu mmoja na kubaki mlemavu 'Chiba'.

chiba.jpg
 
alisema anaweza kudansi na mguu mmoja jukwani mda mrefu lakini kutembea bila gongo lake hawez..hata mwenyewe anajishangaa...
Mungu akikunyima hiki jua kakupa kile!
Ila tatizo ni jinsi ya kugundua hiko kipaji sasa
 
"Baada ya kuona maisha yamekuwa magumu niliamua kukimbilia kwa baba aliyekuwa anaishi Lindi ambapo alinipeleka gereji kujifunza ufundi wa magari. Nilikuwa na ndoto nyingi kupitia ufundi huo lakini ikatokea siku moja ambayo siwezi kuisahau maishani mwangu kwani ndiyo ilifuta ndoto zangu japo namshukuru Mungu kwa kila jambo. Nakumbuka
ilikuwa mwaka 2014 nilitoka nyumbani kwenda stendi ya mabasi ya Lindi katika kijiwe nilichozoea kupiga stori na washkaji. Wakati nikiwa kijiweni hapo kuna mama mmoja anayeitwa Mama Royal alikuwa akigeuza gari lake. Kwa bahati mbaya badala ya kukanyaga breki, alikanyaga mafuta na gari lilirudi nyuma kwa kasi na kunivamia ambapo lilinijeruhi mguu. Nilikimbizwa hospitali ya Sokoine kwa matibabu ambapo nilifungwa plasta gumu (P.O.P). Pamoja na kufugwa hogo lile, nilijisikia maumivu makali hadi kumlalamikia baba aliyenitaka kuvumilia hadi siku niliyopangiwa kurudi hospitali.
Mguu wavuja damu na kujaza beseni.
"Siku moja baada ya kufungwa hogo nilipata maumivu makali na hogo likaanza kulowa damu kadri siku zilivyosonga mbele. Ilifika wakati damu hiyo ilijaa beseni. Hali hiyo iliwaogopesha wazazi wangu hivyo wakaamua wanirudishe hospitali ambapo daktari alipofungua hogo alikuta mguu umeanza kuoza. Daktari alinisafisha mguu na kuuacha bila kuufunga kwa siku 3 lakini hakukuwa na mabadiliko kwani damu ziliendelea kuvuja.
IMG_0948.JPG

AKATWA MGUU NA KUBATIZWA JINA JIPYA
"Kutokana na maumivu makali, nilijikuta napoteza fahamu mara kwa mara. Kuna siku nilizinduka kutoka kwenye kuzimia, daktari akaniambia kuwa wameshauriana na wazazi wangu na kuamua kunikata mguu. Ama kweli hujafa hujaumbika, kwani hapo ndipo nilipobadilishwa jina kutoka Karim Seleman na kuitwa Chiba tofauti na jina nililopewa na wazazi wangu".
Nukuu ya dansa wa Yamoto Band, Karim Seleman 'Chiba' akielezea mkasa wake ulipolekea akatwe mguu mmoja na kubaki mlemavu 'Chiba'.
chiba.jpg
Waliomfunga hogo ndo walimpatia ulemvu kama ilivyojieleza hapo juu .After bone fracture huwa wanafunga back slab (plaster za kawaida za Ku position eneo lililopata shida) kwa Siku kadhaa ili kuacha uvimbe upungue.baadae ndipo plaster ngumu hufungwa.unapofunga na eneo ambalo mfupa umevunjika kwa plaster ngumu moja kwa moja na pakiwa pamevimba unabana mishipa ya damu na unatengeneza gangrene.lna maana hakuna supply yeyote hivo ni lazima pataoza. Mwisho wa siku wanafanya amputation.
 
Oh kumbe asante mheshimiwa kwa kunifungua macho
 
Mungu fundi sana jamani,huyu kijana sasa anaishi vizuri kuliko alivyokua na miguu miwili
Ni kama kijana saidi,mungu kampa mitihani halafu kamnyanyua kimaisha,bajaji mbili,boxer4 na nyumba,asingepofuka asingeyapata yote hayo
 
Ni budi yetu kumtukuza Mungu
 
Back
Top Bottom