Ni jambo linauma ila mimi nimejifunza kuwaelewa watu. Mara nyingi watu huwa karibu kwa sababu ya jambo fulani.
Kuna jamaa yetu fulani sasa hivi ni naibu waziri aliteuliwa na magu, wana wanalalamika siku hizi hapokei simu zao sijui anaringa.
Ila mimi namwelewa kwa sababu amepanda ngazi sasa hana cha kuongea nao. Sasa hivi simu zake za mawaziri na watu wengine hakuna connection hapo.
Yale yale ya Hashim Thabiti wana kulalamika haji kijiweni akiwa TZ, jamaa walikuwa wanasahau anacheza NBA si Hashimu yule wa zamani.
Maisha yakipanda na wewe unabadilika. Kuna wale wanabaki hivyo hivyo ila kama mtu akibadilika mwelewe tu ila la msingi akifulia sio anakuja tena kwako maana hapo sasa itakuwa kakugeuza wewe ni rafiki wakati wa majanga.