Karma is real

Karma is real

Staki kuandika sana but nobody is perfect, binadamu ndivyo tulivyo na maisha ndivyo yalivyo.

Kwani before hujamkopesha iyo 500k yeye hakuwahi kukusaidia hapo kabla na umesema kabisa alikua mtu wako wa karibu au wewe ndo ulikuwa rafiki yake ila yeye hakuwa rafiki Yako?
 
Ni jambo linauma ila mimi nimejifunza kuwaelewa watu. Mara nyingi watu huwa karibu kwa sababu ya jambo fulani.
Kuna jamaa yetu fulani sasa hivi ni naibu waziri aliteuliwa na magu, wana wanalalamika siku hizi hapokei simu zao sijui anaringa.
Ila mimi namwelewa kwa sababu amepanda ngazi sasa hana cha kuongea nao. Sasa hivi simu zake za mawaziri na watu wengine hakuna connection hapo.
Yale yale ya Hashim Thabiti wana kulalamika haji kijiweni akiwa TZ, jamaa walikuwa wanasahau anacheza NBA si Hashimu yule wa zamani.
Maisha yakipanda na wewe unabadilika. Kuna wale wanabaki hivyo hivyo ila kama mtu akibadilika mwelewe tu ila la msingi akifulia sio anakuja tena kwako maana hapo sasa itakuwa kakugeuza wewe ni rafiki wakati wa majanga.
Niliishi na ndugu wa baba vizuri kabisa na nilikuwa nikiwasaidia kwakuwa wengi hali zao si nzuri na baba alikuwa si haba nami nikafuata nyayo cha kushangaza baba alipokufa wakasema hawanitambui kwa kuwa baba hakufunga ndoa na ma nima.

Nilishangaa sana yaani wakawa hawanitaki kabisa pale msibani kitu ambacho sijawahi kushuhudia Ktk umri wangu nikamuona baba mkubwa akikomalia hiyo hoja, nikakumbuka nilivyotoa 3.4 milion kwa matibabu ya kichwa ya kijana wa huyu mzee pale mhimbili kumbe lengo lao nisimiliki mali za baba na wakaweka zuio mahakamani nikawa shinda kwa sheria za nchi wao waliegemea imani.

Nikapiga bei hadi kuku nikaanzisha miradi yangu Mbaali kabisa sasa naona ndugu walewale wanakuja tena kuniomba Msaada kiukweli sijafukuza, kukata wala kukemea mtu yeyote hadi sasa lakini kuna mambo yanakera sana hapa duniani.
 
Back
Top Bottom