KARMA - Kidamali: Wewe Mwenyewe Ndiye

KARMA - Kidamali: Wewe Mwenyewe Ndiye

Je, bado nina haki ya kumchukia mama Maila ama niwe mpole kama mfalme Daudi?

  • Una haki ya kumchukia (we all have a past lakini alichokifanya sicho)

  • Unavuna ulichopanda (It's Karma!)

  • Nipo katikati (Matukio hayana uhusiano kwangu; so reaction zote mbili naziona justified)

  • Sijui (bado sijaamini kilichotokea, nimeshindwa kutafakari, ...)


Results are only viewable after voting.
Sema neno mkuu...


But why...

- Kwa nini karma iniadhibu zaidi ya niliyofanya wakati wa ujana (foolish age)?

- Kwanini karma isiangalie ambavyo nilibadilika na kuwa mume mwema baada ya kumuoa mke wangu ikakumbuka uovu tu?
Kwani ulitubu?
 
Pole sana mpendwa.
Pia asanteh sana kwa somo maana nimejifunza na kupata woga wa kutendea wengine mabaya kwasababu huwezi kujua wakati sahihi wa kukurudia hayo mabaya.

Tuishi kwa hofu, tupendane tuthaminiane na kutendeana mema siku zote za duniani, malipo ni hapa hapa.
Kama kila mtu angekua na hofu ya kutomtenda mwingine vibaya dunia ingekua sehemu nzuri sana ya kuishi. Nawaambiaga watu kabla hujamtendea mwingine kitu jiweke nafasi yake kwamba ukifanyiwa wewe utapenda? Kama hutapenda basi usimfanyie
 
Mkuu, huenda kutumia neno KARMA kunakuudhi...

Naomba usome maelezo niliyoyatoa. Sijawahi kuandika kisa/mkasa na kuutolea maelezo ya kwa nini nimekiandika lakini kwa hili imenibidi niandike.



Kama huamini hiyo philosophy ya KARMA basi labda unaifahamu ile GOLDEN RULE; usimtendee mtu usilotaka kutendewa.

Ni kweli kabisa kuwa huenda yaliyonipata hayahusiani na uovu nilioutenda (maana pia kiuhalisia nimetenda mwingi zaidi ya niliyoyaandika). Lakini kuna ile dhana ya kumkasirikia mtu kwa kukutendea jambo ambalo wewe mwenyewe ukitafakari utakumbuka ulishamtendea mwingine sawa au zaidi ya hilo. Basi kwa hilo, point ya kuchukua ni kutokukasirika yanapokukuta, KARMA or no KARMA.

Lakini pia, ni mkasa ambao unatoa funzo la kutafakari sasa (NOW) yapi tunayotenda kwa watu na kujiuliza tukitendewa hayo tutafurahi? Nadhani tukienenda kwa kujiuliza hivyo ni mara chache tutaruhusu udhaifu wetu wa kibinadamu (au nia ovu) kuathiri maisha ya wengine.

Naamini wenye dini na wasio na dini wote tunakubaliana na the golden rule. Basi tusitumie kutokukubaliana nami kutumia neno KARMA kisha ukasahau somo zima la mkasa huu. Tukubaliane kuwa tujitahidi kuwatendea wengine kama ambavyo tungependa kutendewa sisi. Haiondoi maumivu ikitokea umetendwa vibaya lakini itakusaidia kupona haraka unapojua hukumtendea mwingine uovu kama huo. Lakini zaidi ni, kila mmoja wetu akijitahidi kuishi hivyo, we can make our lives here on earth 'little paradise'.


Cheers!
Nimemquote Ney kitu kama hicho cha usimtendee mwingine usichopenda kutendewa nakuta na wewe umeandika hapa. Na nimejua leo kumbe inaitwa GOLDEN RULE
 
Back
Top Bottom