KWELI Karoti ni nzuri kwa afya ya macho, lakini haiongezi uoni kuzidi kawaida unapokuwa gizani (Usiku)

KWELI Karoti ni nzuri kwa afya ya macho, lakini haiongezi uoni kuzidi kawaida unapokuwa gizani (Usiku)

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Msemo huu kuwa ulaji wa Karoti unaongeza uoni wakati wa usiku uekuwa maarfu sana miongoni mwa watu lakini je uhalisia ni upi?

Makala iliyochapishwa na Medical News Today inataja faida mbalimali zitokanaz0 na ulaji wa karoti kutokana na wingi wa virutubisho ilivyo navyo.

“Karoti zina vitamini, madini na viambata vya kuzuia uharibifu wa seli (antioxidants). Kula karoti kama sehemu ya lishe bora husaidia kuimarisha kinga ya mwili, uponaji wa vidonda, afya ya mfumo wa mmeng’enyo wa chakula na inaweza kupunguza hatari ya baadhi ya saratani.”

Kwanini karoti inatajwa kuwa nzuri kwa afya ya macho?

Karoti zina beta-carotene, kirutubisho ambacho hubadilishwa na mwili kuwa vitamini A. Vitamini A ni muhimu kwa afya ya macho na husaidia kuona vizuri hasa kwenye mwanga hafifu.

Vitamini A husaidia kutengeneza rhodopsin, kemikali inayowezesha macho kuona gizani. Pia husaidia kulinda konea na kuweka uso wa jicho ukiwa na unyevunyevu.

Je, husaidia kuongeza uoni wakati wa usiku?

Licha ya umuhimu mkubwa wa ulaji wa karoti kwa afya ya macho lakini Si kweli kuwa karoti inaweza kukupa uezo wa kuona gizani kuliko kawaida.

Karoti hazibadilishi uwezo wa kuona kimiujiza kama una matatizo ya macho tayari, kama vile kuona karibu (myopia) au kuona mbali (hyperopia).
1784203043035.png

Kula karoti nyingi hakutaondoa hitaji la kutumia miwani au lenzi za macho.Hata hivyo, lishe yenye vitamini A inaweza kusaidia kudumisha uoni wenye afya na kupunguza hatari ya baadhi ya matatizo ya macho kadri umri unavyoongezeka.

Ni, wapi ilipotokea nadharia hii?

Imani hii ilienea sana wakati wa Vita vya Pili vya Dunia, baada ya Uingereza kueneza taarifa kwamba marubani wake waliweza kuangusha ndege za adui usiku kwa sababu walikula karoti nyingi. Ukweli ni kwamba siri ilikuwa teknolojia mpya ya rada, lakini propaganda hiyo iliwaaminisha watu wengi.
 
Ninachoamini ni hiki, kila suluhisho la changamoto ya afya ya mwanadamu, tiba yake ya asili ipo.

Niliwahi kutokwa na malengelenge sehemu ndogo na baadae yakajenga kama kikidonda baada ya ngozi kubabuka. Niliwahi kusikia kwamba aloe vera ni nzuri kwa ngozi, nikapaka. Kesho yake ngozi ikaanza kukakaa na baada ya siku mbili hata yale maumivu ya kidonda yalipotea.

Kuna siku niliwahi kuumwa na mdudu fulani, nikaambiwa ni tandu baada ya kumuua. Nilipata maumivu mguu mzima na ganzi ilikuwa ni kubwa kiasi, hata nikitembea mwendo ulibadilika. Dawa za maumivu kama Tramadol hazikusaidia, mtu mmoja akasema paka kitunguu maji, nikakata kisha nikapaka, ile ganzi na maumivu yake yakapotea haraka tu nilipoamka.

Ninachotaka kusema ni kwamba, haya tunayoyasikia kuhusu vyakula na dawa za asili, yanaweza yakawa na uhalisia mkubwa. Na yamkini hata madawa tunayokunywa wenzetu wanatengeneza kupitia mitishamba hiihii tu.

Kuna mtu aliwahi kuumwa tumbo had akawa analia tena ni mtu mzima, akachemshiwa majani akanywa, tumbo likakata. Toka siku hiyo sijawahi puuzia wasemalo wahenga.
 
Back
Top Bottom