Karudi Baba Mmoja (Toleo Jipya)

Karudi Baba Mmoja (Toleo Jipya)

NI mojawapo ya mashairi ambayo wengi waliosoma shule za msingi za umma za Tanzania watakuwa wanalikumbuka; lilianza hivi:

Mwanakijiji asante sana, ni wiki mbili zilizopita nilikua najaribu kuwaimbia watoto wangu hili shairi nikawa nimesahau beti zake nikawaambia nitawatafutia lol umenisaidia kutimiza ahadi, thanks!!!
 
Dah Ahsante sana mkuu.
Sasa nitalihifadhi vizuri hili ,maana beti nyingine ilizisahau kabisa.
 
Hili ni miongoni mwa mashairi maarufu sana nchini Tanzania. Mtunzi wa Shairi hili (kwangu) hafahamiki , ila katika video hii, shairi hili limeimbwa na mshairi Filipo Lubua, katika tamasha la Siku ya Lugha za Kiafrika (African Languages Day), katika Chuo Kikuu cha Ohio, nchini Marekani. Wale vijana wa zamani, tukumbushane enzi zetu. Shairi hili si kama bigijii, haliishi utamu kamwe!


<a href="http://www.youtube.com/watch?v=6HX3-fIflg4">
 
Last edited by a moderator:
Dah umenikumbusha miaka ya 1993 au 1994 kama sio drsla 3 basi la 4 sijui kama watoto wa siku hizi wana mambo matamu kama haya
 
karudi baba mmoja, toka safari ya mbali,
kavimba yote mapaja, na kutetemeka mwili,
watoto wake wakaja, ili kumtaka hali,
wakataka na kauli iwafae maishani.

Akatamka mgonjwa, ninaumwa kweli kweli,
hata kama nikichanjwa, haitoki homa kali,
roho naona yachinjwa, kifo kimenikabili, KAMA MNATAKA MALI MTAIPATA BUNGENI..
 
Wadau kwa kizazi chetu cha digitali nadhani shairi hili linafahamika na wote

1. Karudi baba mmoja, toka safari ya mbali,
Kavimba yote mapaja, na kutetemeka mwili,
Watoto wake wakaja, ili kumtaka hali,
Wakataka na kauli iwafe maishani.

2. Akatamka mgonjwa, ninaumwa kwelikweli,
Hata kama nikichanjwa, haitoki homa kali,
Roho naona yachinwa, kifo kimenikabili,
Semeni niseme nini, kiwafae maishani.

3. Yakawatoka kinywani, maneno yenye akili,
Baba yetu wa thamani, sisi tunataka mali,
Urithi tunatamani, mali yetu ya halali,
Sema iko wapi mali, itufae maishani?-(P.T)

4. Baba aliye kufani, akajibu lile swali,
Ninakufa maskini, baba yenu sina hali,
Neno moja lishikeni, kama mnataka mali,
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.

5. Wakazidi kumchimba, baba mwenye homa kali,
Baba yetu watufumba, hatujui fumbo hili,
Akili zetu nyembamba, hazijajua methali,
Kama tunataka mali, tutapataje shambani?

6. Kwanza shirikianeni, nawapa hiyo kauli,
Fanyeni kazi shambani, mwisho mtapata mali,
Haya sasa buriani, kifo kimeniwasili,
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.

7. Alipokwisha kutaja, fumbo hili la akili,
Mauti nayo yakaja, roho ikaacha mwili,
Na watoto kwa umoja, wakakumbuka kauli,
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.

8. Fumbo wakatafakari, watoto wale wawili,
Wakakata na shauri, baada ya siku mbili,
Wote wakawa tayari, pori nene kukabili,
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.

9. Wakazipanda shambani, mbegu nyingi mbalimbali,
Tangu zile za mibuni, hadi zitupazo wali,
Na mvua ikaja chini, wakaona na dalili,
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.

10. Shamba wakapalilia, bila kupata ajali,
Mavuno yakawajia, wakafaidi ugali,
Wote wakashangilia, wakakumbuka kauli,
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.

11. Wakanunua na ng'ombe, majike kwa mafahali,
Wakapata na vikombe, mashine na baiskeli,
Hawakuitaka pombe, sababu pombe si mali,
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.

12. Wakaongeza mazao, na nyumba za matofali,
Pale penye shamba lao, wakaihubiri mali,
Wakakiweka kibao, wakaandika kauli,
"KAMA MNATAKA MALI MTAYAPATA SHAMBANI".
 
Asante sana... nimetafuta sana lyrics za hili shairi...

Ubarikiwe sana
 
Duh! We jamaa, hili shairi umekariri au umelikopi toka kwenye kitabu? Maana ulivyotiririka!
Lakini mimi huwa nashindwa kuelewa lipi maarufu zaidi kati ya hili na lile la jingine la
"Hadithi inayokuja ni ya sungura sikia..."
 
Back
Top Bottom