Wanabodi,
Kufuatia chokochoko ya kuuchokoa Muungano ilioanzishwa na kikundi cha Uamsho huko Zanzibar, zimeanza kutolewa hoja mbalimbali ikiwemo Watanzania tupewe fursa kuujadili Muungano na ikibidi ipigwe kura ya maoni kuwauliza Watanzania na Wanzanzibari kama wanautaka muungano, jee wanataka muungano wa aina gani, na endapo hawautaki, process ya kuuvunja rasmi aianze.
Wako wengi wanaupenda muungano na wangependa uendelee ila uboreshwe!. Pia wako wanao ona sasa imetosha na muungano uvunjwe!.
Maudhui ya mada hii ni kuwaeleza wanabodi, jambo muhimu liitwalo "kuridhia" ambapo serikali zote zilipaswa kuuriidhia huo muungano kwa utaratibu unaoitwa "RATIFICATION" ambapo ni serikali ya Tanganyika pekee ndio iliyofanya process rasmi ya "ratification", Zanzibar, haikufanya process bali ilitamka tuu kwa maneno ya mdomo bila tamko lolote rasmi la maandishi, na badala yake, hati ya ratification ya Zanzibar, iliwasilishwa kwenye bunge la Tanganyika na dunia kutangaziwa muungano uliridhiwa pande zote!.
Kwa vile Zanzibar, haikuuridhia rasmi Muungano, kama ni kweli hizi chokochoko za Uamsho ni uthibitisho kuwa sasa Zanzibar inataka kujitoa katika muungano wetu huu adhimu, kisheria, mlango uko wazi, yaani wide open for Zanzibar to just walk out, with no regret and no strings attached kwa sababu hawakuuridhia ule mkataba wa muungano in then first place!, hivyo mkataba huo hauko binding kwao!.
Mada yangu hii inakuwa na sehemu zifuatazo.
1. Kuridhia ni Nini (Ratification).
2. Rafication Hufanyikaje.
3. Mikataba ya Kimaifa ni nini? na Jee Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar ni Mkataba wa Kimataifa?.
4. Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
5. Process ya Ratification kwa Upande wa Tanganyika.Process ya Ratification kwa Upande wa Zanzibar.
6. Hadaa ya Ratification ya Zanzibar, ilipangwa na nani na kwa nini?.
7. Kukosekana kwa ratification upande wa Zanzibar kunamaanisha nini.
8. Pamoja na kutokuwepo ratification, Jee Muungano ni halali?
9. A Way Forward 1:Tudumishe Muungano?, Muungano wa Aina Gani?.
10. A Way Forward 2:Tuuvunje Muungano?. What are the Consequences?.
1. Kuridhia ni Nini (Ratification).
Kuridhia, au ratification, ni process inayofanywa kwa nchi husika kuridhia mikataba ya kimaifa ili kuipa uhalali wa kisheria kutumika katika nchi husika. Mfano mzuri ni mkataba wa Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar, Tanganyika ni nchi, na Zanzibar ni nchi, hivyo ule mkataba wa muungano ni mkataba wa kimataifa.
Jee kila mkataba wa kimataifa ni lazima uridhiwe?. Jibu ni hapana, sio kila mkataba wa kimataifa ni lazima uridhiwe, ili mkataba wa kimataifa uridhiwe lazima mkutaba husika uwe na kipengele kinacholazimisha mkataba huo kuridhiwa. Tukirudi kwenye mfano wetu wa mkataba wa muungano, kipengele cha VIII cha Articles of Union, kinalazimisha process ya ratification lazima ifanyike ili kuuhalalisha mkataba ule.
(viii) These Articles shall be subject to the enactment of laws by the Parliament of Tanganyika and by the Revolutionary Council of the Peoples' Republic of Zanzibar in conjunction with the Cabinet of Ministers thereof, ratifying the same and providing for the Government of the united Republic and of Zanzibar in accordance therewith.
Nyerere na Karume wangeweza kuamua wakishasaini makubali yale iishie hapo, ingekuwa hivyo hivyo hitaji la kuridhia lisingekuwepo!.
2. Rafication Hufanyikaje?.
Kwa vile mikataba yote ya kimataifa ni lazima iwe ni ya maandishi, vivyo hivyo, ratifikation lazima ifanyike kwa maandishi na sio kwa kauli.
Kwa bunge letu, masharti ya kuridhia hufanywa kwa mujibu wa kifungu cha 63(3)(e) cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kinachotamka kuwa, Bunge litajadili na kuridhia Mikataba yote inayohusu Jamhuri ya Muungano na ambayo kwa masharti yake inahitaji kuridhiwa na kwa mujibu wa Kanuni za Bunge, Kanuni ya 114(11) ya 2007.
1. Waziri husika huwasilisha mezani kwa spika mkataba husika
2. Spika ataipa kamati husika kupata maoni yake
3. Kambi ya upinzani itapewa fursa ya kuandaa maoni yake.
4. Mkataba huo utatangazwa rasmi kwenye order paper ya siku ya kuwasilishwa
5. Waziri atawasilisha, kisha maoni ya kamati, maoni ya kambi ya upinzani na majadiliano.
6. Bunge litakaa kama kamati kupitia kifungu kwa kifungu
7. Bunge litarudi kama bunge na kuridhia mkataba husika
8. Mkataba huo unakuwa sehemu ya sheria za nchi,
9. Unasainiwa na rais na kutangazwa katika gazeti za serikali GN.
10.Ndio unakuwa umeridhiwa, yaani ratified!.
3. Mikataba ya Kimaifa ni nini? na Jee Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar ni Mkataba wa Kimataifa?.
Mkataba wa Kimataifa, ni mkataba kati nchi moja na nchi nyingine, au mikataba yote ya jumuiza za kimataifa ambayo nchi ama hutakiwa kuridhia, au kulazimishwa kuiheshimu hata kama haikuridhia. Mikataba hii au itifaki mbalimbali (protocals), hupaswa kuridhiwa kabla haijawa sheria kwa nchi husika.
Mfano Tanzania iliridhia mkataba wa mahakama ya kimataifa ya Biashara, ICC. Dowans iliposhinda ile kesi, imepaswa kuisajili hukumu hiyo kwenye mahakama zetu (ratification), ili hukumu hiyo igeuke sheria zetu, (domestic law) na kutekelezwa. Watu humu walipiga sana kelele, nilipouangalia mkataba ule humu jf, nikawaambia wana jf wenzangu, hatuna pa kutokea, tozo ile italipwa tuu mara baada ya tozo hiyo kusajiliwa, kinachoendelea sasa ni delaying tactics ambayo nayo tutailipia dearly!.
Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar, ni mkataba halali wa kimataifa wenye sifa muhimu za mkataba, japo una mapungufu mengi kubwa likiwa ni kitu kinachoitwa "Privity of Contrac" ambapo mkataba ulikuwa kwa lugha ya Kiingereza na signatory mmoja alikuwa msomi anaejua kusoma na kuandika kiingereza, wakati signatory wa pili hakujua kusoma, kuandika wala kiingereza, hivyo alisaini kwa dole gumba!.
Ufafanuzi zaidi kuhusu Muungano kuwa ni mkataba wa kimataifa, unapatikana pia katika ukurasa wa kwanza wa andiko la
Prof. Shivji kwenye kitabu cha "The Legal Foundation of the Union in Tanzania and Zanzibar Constitution, DUP, 1990.
Kwa faida ya wasoma kimombo, tembelea
http://www.scribd.com/doc/45109599/T...A-AND-ZANZIBAR
4. Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Kila mtu anaelewa Mkataba wa Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar, ulitiwa saini na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Abeid Amani Karume, Aprili 22, 1964, Mjini Zanzibar Hapa nitawapa tuu ilivyokuwa kabla na kilichofuata.
Baada ya Mapinduzi ya Zanzibar, na Nyerere kumsaidia Karume kumshughulikia Johh Okello, Karume alikuwa bado ana wasiwasi wa kudumu kwake kama Mwenyekiti wa BLM, kwa kuzingatia Karume hakushiriki mapinduzi yale, Kiongozi wa mapinduzi alikuwa ni John Okello, Karume alikimbilia bara kujificha! (Japo ilikuja kutangazwa ati alikuwa akiwapeleka wanae Amani na Ali waliokuwa wakisoma kwao Karume (Malawi). Okelo ndie alikuwa Mwenyekiti wa BLM na alimuita Karume kuwa mtangazaji kufuatio kuwa na Kiswahili safi. Karume akamzunguka Okello na kwa kusaidiwa na Nyerere, Okello alishughulikiwa na Karume kuitwaa nafasi ya Mwenyekiti wa BLM!.Kwa vile Karume hakushiriki actively kwenye mapinduzi halisi, alikuwa na wasiwasi wakati wote kuwa wale makamanda wangemrudi!, thanks kwa ulinzi wa askari 300 wa Nyerere, vinginevyo hata hiyo 1971, asingefika!.
Mwezi Machi, 1964, Nyerere alizungumza na Karume kuhusu Muungano, Karume alikubali hapo hapo na kutaka Press Conference iitishwe siku hiyo hoyo watangaze kuwa wameshaungana na kuwa nchi moja, Nyerere Rais, Karume Makamo. Mwalimu alimgomea Karume na kumwambia afanye siri ili taratibu zifuatwe.
Mwanzoni mwa Aprili, Mwalimu alimuita AG waTanganyika, Rowland Brown na kumwambia aandae mkataba wa muungano na uwe siri. Kule Zanzibar, Karume akampa likizo AG wa Zanzibar, Wolfgang Dourado ili isitie kauzibe. Akatafutwa Mwanasheria wa Uganda, Daniel Wadada Nabudere (kakaye mwandishi mashuhuri, David Wadada Nabudere) kutoa ushauri kwa Karume kuhusu muungano.
Tarehe, 22 April, 1964 Nyerere aliyeandamana na Rashidi Kawawa, Oscar Kambona na Job Lusinde walitua ghafla Zanzibar na kwenda moja kwa moja Ikulu ya Zanzibar, wakiwa na hati za muungano na Karume alitakiwa azisaini. Wakati wa utiaji saini huo, ulishuhudiwa pia na Abdallah Kassim Hanga, Abdul-Aziz Ali Twala na Salim Rashidi.
Karume alitaka kumtumia mwanasheria huyo wa Uganda kusaini kwa niaba ya mwanasheria mkuu wa Zanzibar, ila Nabudere akakataa na kusisitiza lazima zisainiwe na Mwanasheria wa Zanzibar!. Ndipo Rowland Brown akatinga na Solicitor General wa Tanganyika, PRN Fifoot aliyesimama nafasi ya Dourado!. Hati za muungano zikasainiwa!. Baada ya hapo Nyerere na ujumbe wake wakawaa pipa lao na kurejea Dar!.
Mkumbuke mpaka Karume anasaini, hajaliambia chochote BLM, siku hiyo jioni Aboud Jumbe aliyekuwa Pemba, ndipo akaelezwa na Karume kilichotokea asubuhi, akashangaa sana!. Jambo kubwa kama hilo limefanyika vipi, BLM, hawajui kitu!.
Ni baada ya kusainiwa, Bunge la Tanganyika likatunga sheria ya Muungano, ili kuuthibitisha hati zile, 'ratification', na BLM nalo lilipaswa kukaa na kuridhia hati zile!.
Muungano Ulithibitishwa rasmi na Bunge la Tanganyika kwa kutungiwa sheria na na ikatolewa uthibitisho mwingine uliosainiwa na Fifffoot kuonyesha kuwa BLM liliketi na kuridhia, lakini kiukweli BLM halikukaa, kujadili, wala kupitisha chochote kule Zanzibar!. Kila kitu kilifanywa bara!.
Aprili 27, 1964 Nyerere na Karume, walitinga katika ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Dalaam kubadilishana hati za Muungano zilizosainiwa na Nyerere na Karume, na documents za ratification na tangu hapo Tanganyika na Zanzibar kuwa dola moja kwa misngi inayotambulika kimataifa. Baada ya kuungana, Mwalimu Nyerere alikuwa rais wa kwanza na Karume alikuwa makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Siku hiyo ya Aprili 27, 1964 ndio siku wajumbe saba wa Baraza la Mapinduzi waliapishwa kuwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Watanganyika na Zanzibar ambao ni Amani Karume, Kassim Abdallah Hanga, Abdulrahman Babu, Hassan Nassor Moyo, Aboud Jumbe, Hasnu Makame na Idris Abdul Wakil. Kati yao, Aboud Jumbe na Hassan Nassor Moyo wangali hai. Baada ya hapo, Bunge la Muungano likakamata madaraka yote!.
5. Process ya Ratification kwa Upande wa Tanganyika.Process ya Ratification kwa Upande wa Zanzibar.
1. Msingi mkuu wa ratification mkataba wa muungano ni kifungu hiki kwenye hati za muungano.
Article VIII of the Articles of Union provides:" These Articles shall be subject to the enactment of laws by the Parliament of Tanganyika and by the Revolutionary Council of the Peoples Republic of Zanzibar in conjunction with the cabinet of ministers thereof, ratifying the same and providing for the Government of United Republic and of Zanzibar in accordance therewith2. Lengo la kifungu hicho, ni kwa vile muungano ni mkataba wa kimataifa, ili mkataba huo upate uhalali wa kisheria katika nchi husika, lazima mkataba huo uridhiwe na nchi husika, hivyo kifungu hicho kilimaanisha bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi, walipaswa waridhie mkataba huo kwa kuutungia sheria mahsusi ili kuuhalalisha kisheria ndani ya nchi zao!.
2. Kuridhia au kutoridhia, hakuondoi uhalali wa mkataba, bali unaondoa uhalali wa kisheria, pale yule ambaye alikosa uhalali wa kisheria pale mwanzo, akiamua hautaki tena ule mkataba, hawajibiki kuuvunja mkataba, but he can just walk away!.
3. Baada tuu ya hati za Muungano kutiwa saini ile Aprill 22 kule Zanzibar, Mwanasheria Mkuu Tanganyika enzi hizo, Rowland Brown aliandaa ratification na kupelekwa kwenye kikao cha bunge la Tanganyika, likapitisha ratification ile asubuhi ya Aprili 26, 1964 kwa kutunga sheria No. 243 ambayo ilitangazwa kwenye gazeti la serikali ya Tanganyika, GN No. hivyo kutimiza matakwa ya kile kifungu namba viii cha mkataba wa muungano.
4. Wakati hayo yakiendelea huku Tanganyika, Zanzibar nao kupitia Mwanasheria Wake Mkuu, Wolfgang Dourado, alipaswa kuandaa hiyo sheria ya ratification kule ikiitwa Decree, ili Baraza la Mapinduzi likae na kuipitisha hivyo kuutambua rasmi muungano kisheria. Hili halikufanyika lkwa sababu Dourado alipewa likizo ya siku 7 akapumzike nje ya nchi!. Aliporudi, seven day leter, akakuta game over!. Akaishia kulalamika kichini chini maana angetoa sauti, sijui kama hata unywele ungepatikana!. Ushahidi ni kauli ya Dourado Mwenyewe "I myself have been the Zanzibar Attorney General and Minster responsible for justice between 1984 and 1989. At that time I managed to peruse all the statute books of Zanzibar from 1964 and 1979 when the Revolutionary Council was acting as a legislative Assembly cum the Cabinet. No ratification law or any law to that effect is there. I was not myopic, but even if I was, the first Attorney General of Zanzibar after the Revolution had also testified the same that no law ratifying the Articles of unionexists on the Statute Books of Zanzibar." Dourado aliyasema hayo katika andiko lake la "The Consolidation of Union" alilowasilisha kwenye semina ya Tanhanyika Law Society, Julai 7, 1983 hapa jijini Dar es Salaam.
5. Mpaka Mungu amemuita Dourado mbele ya haki, msimamo wake ulikuwa "No law ratifying the Articles of the union of 1964 exists on the statute books of Zanzibar., I as a Principal Legal adviser to the Zanzibar government was not consulted ……… Zanzibar therefore did not have legal or constitutional advice from its Principal Legal adviser."
6. Badala yake, Solicitor General wa Tanganyika, PRN Fifoot ndiye alieandaa ratification document ya Zanzíbar ambayo aliisaini yeye na kumpatia Karume ile April, 27, 1964, Karume aiwasilishe kwenye bunge la Tanganyika ile siku Nyerere na Karume walibadilishana hati pale Karimjee. Hati ya aliyoiwasilisha Nyerere was a genuine ratified document iliyokuwa ratified na bunge la Tanganyika!. Hati aliyowasilisha Karume, was a fake one as if ni BLM ndilo nalo limefanya hiyo rafication kama lilivyofanya bunge la Tangayika!, It was just a make belive, kuizuga jumuiya ya kimataifa na hapo ndipo hata hao CIA na iteligensia yao wakaingizwa chaka na kubaki kupiga tarumbeta ya ratification kuwa ilifanyika!.
7. Hata kama Fifoot aliiandaa hiyo ratification ya Zanzibar, kwa nini hakumpa Douradau naibu wake, ili aisaini na kuipitisha kwenye kikao cha BLM ili angalau ionekane ilipitishwa Zanzibar?!.Kwa vile Zanzibar hawakuwa na bunge, Baraza la Mapinduzi ndilo lililokuwa Bunge, Baraza la Mawaziri na Mahakama, kwanini ile ratification iliyoandaliwa bara, isipelekwe tuu na kupigwa rubber stamp kwenye BLM ili kuipa uhalali kuwa ni kweli BLM waliridhia na kuratify?!.
8. Siku ile ya April 27, 1964, wakati Nyerere na Karume walipotinga ndani ya bunge la Tanganyika, kubadilishana hati za muungano zilizo kuwa ratified,Nyerere aliwasilisha hati halali ya muungano ilikuwa ratified kihalali na bunge la Tanganyika na kutangazwa rasmi kwenye gazeti la serikali, GN lakini Karume aliwasilisha ile hati iliyosainiwa na Fifoot alijifanya Dourado na kuziwasilisha hati za muungano kwenye bunge la Tanganyika as if ni kweli BLM lilikaa likajadili na kuridhia hizo hati za muungano, na Karume sio tuu amesaini hizo ratification bila kuzipitishia BLM, bali pia amezitungia Decree na kuitangaza katika GN hiyo hiyo ya Tanganyika japo kwenye GN ya Zanzibar sheria hiyo haipo!.
9. Kisheria, kwenye sheria ya mikataba, place of contact maters much as far as domestic laws are concerned, Ule mkataba wa muungano ni international contract, unaweza kusainiwa popote ndio maana Mwalimu Nyerere na time yake, walifunga safari kwenda Zanzibar. Process ya ratification sio international contact, ni domestic contact kutumia domestic laws (municipal) ambapo ratification hupaswa kufanywa na bunge husika likiwa nchi husika. Bunge la Tanganyika lilitimiza wajibu wake hivyo ratification ya Tanganyika ni legal. Kitendo cha ratification ya Zanzibar kuandaliwa na Fifoot wa Tanganyika na kusainiwa nae, halafu Karume kukabidhiwa sheria hiyo wakati sgeria za Zanzibar kwa wakati huo zilikuwa Decrees na kuiwasilisha bunge la Tanganyika, tangazo la ratification kutolewa kwenye GN ya Tanganyika na sio ya Zanzibar, ni mambo yanaifanya hiyo ratification kuwa voidable na sio void!
10. Hoja ya "privity' to contract na "capacity" to contract pia ipo kwa Karume kama Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, alikuwa na capacity to contact kama Karume kwenye zile articles of union, lakini kwenye Ratification, Karume hakuwa na Capacity ya kusaini sheria ambayo haikutungwa na BLM, na kusainiwa na Fifoot badala ya Dourado, na sheria hiyo kutopitishwa na BLM lakini akaiwasilisha as if imeridhiwa na BLM!, na Fifoot hakuwa na capacity to contract kwa niaba ya Dourado!, tena (ninahisi Fifoot alifanya "misrepresentation kujifanya Dourado ndio maana kuna uwezekano mkubwa, Karume hakupewa tena zile original documents!, alikuja mikono mitupu, na kurudi mikono mitupu ndio kule Zanzibar, hizo documents are no where to be seen!!). Emphasis mine!
11. Hata hivyo, kuna mabishano makubwa kati wanazuoni na wasomi mbalimbali wa sheria kuhusiana na hii issue ya ratification. Mwalimu wangu, Prof. Shivji amesema japo hakuna kumbukumbu zozote kuwa BLM liliridhia, kwa vile BLM limeipitisha sheria ya muungano, huko ndiko kuridhia kwenyewe!, kwa hiyo kwa Shivji, muungano uliridhiwa!.
12. Aliyekuwa kiongozi wa kambi ya upinzani kwenye BLW, Hon. Abubakar Khamis Bakary ambaye ndie aliyetoa posa ya ndoa na CCM kule BLW na kuunda SUK ambapo kama mshenga, amezawadiwa uwaziri wa sheria anapingana na Prof. Shivji kwa kusema kuwa sheria ambayo haikutungwa na BLM wala haikupitishwa na BLM, sio sheria halali kwa Zanzibar!.
13. Pamoja na Kutofautiana na Shivji kuhusu uhalali wa ratification, lakini Mhe. Bakari anakubaliana na Shivji kuwa muungano ni halali, kwa sababu, licha yakutokuwepo official ratification kutoka Zanzíbar, hakuna Wanzanzibari wowote waliochukua hatua zozote za kupinga au kulalamika, hivyo hiyo ni dalili kuwa Wanzanzibari wameukubali muungano impliedily not expressly!.
14. Mwanasheria mwingine wa Zanzibar, al maaruf, Ali Salehe, mwandishi na mtangazaji wa BBC, yeye anashikilia, kwa kwa vile muungano haukuridhiwa, lazima uridhiwe ili kuupa nguvu ya kisheria Zanzibar!. Hivyo anasema ratification ifanyike!. Na hapa ndipo na mimi niliposimamia kuwa Wanzanzibari wafanye ratification kama kweli hawautaki tena muungano, BLW likatae ku ratify ili mlango wa kutokea uwe wazi, wide open!.
15. Prof. Haroub Othman ametofautiana na Shivji kwa kusema wajumbe wawili wa BLM, Abrahman Mohamed Babu na Khamis Abudulah Ameir, walimweleza kuwa BLM walijadilili hati za muungano na kuridhia! (bila maandishi wala kumbukumbu?). Prof. Haroub anadai siku anaelezwa hayo walikuwa club ya YASU akiwa anacheza na katoto fulani ambacho kalikuwa bado hata hajabalehe, kakiitwa Ali Juma Shamhuna!.
16. Kufuatia uwepo wa document ya ratification huku bara, na Zanzibar kimataifa ilikufa rasmi siku ile ya April, 26, 1964, hakuna tena anaejali kama hizo ratification documents zili fojiwa huku bara, ndio maana hata tume ya Nyalali, ilizihalalisha na kimataifa everthing is ok na humo humo ndimo hao majasusi wa Marekani, walikolalia na wote wanaoamini muungano uliridhiwa, japo ni kweli kwa bara muungano uliridhiwa kwa kauli na matendo, kwa Zanzibar, uliridhiwa kwa kauli bila matendo!, na sasa tunasikia kauli za kupinga na matendo ya akufukuzaye!.
17. Kiukweli Karume aliliendesha BLM kibabe sana, yeye kama Rais, Jaji Mkuu na Spika, wale wote waliopingana naye, hakuna ajuaye kilichowakuta ili walishughulikiwa kimya kimya na hata miili yao haikubahatika kuonekena (inasemekana walining'inizwa jiwe shingoni na kutoswa baharini!. Kina Babu kuona hivyo, wakajitimkia zao kabla ya kuwakuta, hayajawakuta. Uvumilivu ulipowashinda waliobaki, nao wakamshughulikia Karume!. (Naamini inteligensia ya Mwalimu alishauona mwelekeo wa Karume kwenye majaaliwa ya muungano, hivyo nae akaacha ya kumkuta yamkute, muungano udumu!.
18. Baada ya Karume, Aboud Jumbe akaukwaa urais. Dourado akamjulisha Jumbe kuhusu kukosekana kwan proper ratification na iliyopelekwa UN is fake!, wakaandaa document kuujulisha ulimwengu kuhusu hilo!. Seif Sharif akamtonya Nyerere, Jumbe akashughulikiwa ipaswavyo, huku Dourado akaozea jela!.Tukatangaziwa "kuchafuka kwa hali ya hewa Zanzibar" bila kuelezwa kisa ni absence ya proper ratification!.
19. Wanzanzibar ni watu wazito sana kujifunza, licha ya kujua kilichomkuta Jumbe kilihusu kuutishia muungano, Dr. Salmini nae akataka kucheza karata yake zile siku zake za mwisho mwisho alinukuliwa akisema, wao wanayatambua yale mambo 11 tuu ndio ya halali, hivyo akajenga hoja kubadili katiba aongeze kipindi cha tatu ili ayashughulikie!. Tiss ilimshughulikia yeye na timu yake yote wakatupwa kando!. Hamshaghai kwa nini Salmin baada ya kustaafu hakuitwa popote kuwa mgeni rasmi kwenye shughuli rasmi?, na yule dada yetu naye akaporwa!.
20.Kupitia hoja hizo na nyingine ambazo sikuzitaja, Mimi Pasco wa JF, kwa Mamlaka niliopewa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Chini ya Kifungu cha "Freedom of Expressions", Sasa Natamka Wazi kuwa Muungano Kati ya Tanganyika na Zanzibar, Haukuwa Ratified Properly in Zanzibar!. Ila pia Nasisitiza, Muungano Huu ni Halali, japo ulikosa uhalali kwa njia ya Expressly in Zanzibar, umepata uhalali huo Impliedly!.
Angalizo.
Unaruhusiwa kucoment chochote wakati mada hii ikiteremka, just coments tuu ila naomba sana, maswali juu ya kuhusu hii mada kabla sijafika mwisho, maana sitakujibu mpaka nimalise, ila nikishamaliza sura zote kumi, nitapokea maswali, maoni au mapendekezo. Endepo uliuliza swali kabla sijafika mwisho, na hatimaye ulikuja jibu la swali lako kwenye mada za mbele, sitakujibu upya bali nitakurefer kwenye majibu ya swali lako.
Hii mada siyo accademic paper, naishusha kwa level ya mwananchi wa kawaida wa Tanzania ambaye ni darasa la saba!. Hata hivyo kwa faida ya wasomi ambao wangependa kuzama deep, mwisho, nitawawekea, references za kusoma zaidi.
Natanguliza shukrani.
Pasco.