Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Halafu tunaambiwa muungano ulifanywa kwa maslahi ya wananchi. Jamani tuachiani tuamue sasa kipi kizuri kwetu na sio kwa faida ya viongozi waliopita!
Njia nyingine rahisi ya kutafiti kuhusu nyaraka za kiserikali ni kupitia nyaraka zote zilizoandikwa katika kipindi husika. Je kuna mtu anaweza kuleta Nyaraka za Baraza la mapinduzi katika kipindi chote kuanzia Januari mwaka 1964 had November mwaka 1964 ambapo ndipo Jina la Tanzania lilipoanza kufanya kazi? At least tumeshaona waraka mmoja wa kutoka kwenye bunge la Tanganyika ukiwa na addendum ya articles of the Union na tumeshaona picha nyingi za Karume na Nyerere wakisaini makubaliano hayo. Hata kama huo waraka huo haupo, ni vizuri tunyeshwe nyaraka nyingine zilizofanyika hapo katikati kwa vile zitainyesha iwapo zilikuwa zinatambu muungano au vipi.
Kama haya ya kweli hivi wambunge wa CCM Zanzibar nani kawaronga au ni hizo laki 3 zimewakosesha uzalendo? wakati ndio huu tuweke kila kitu wazi, mpira urudishwe kwa wananchi kama tunataka Muungano au la na kama ndio ni Muungano wa serikali ngapi? Kama Taifa yatubidi tuanze upya tusiendelea kuweka uchafu uvunguni wa kapeti maana kwa sasa tuko uchi..
Halafu tunaambiwa muungano ulifanywa kwa maslahi ya wananchi. Jamani tuachiani tuamue sasa kipi kizuri kwetu na sio kwa faida ya viongozi waliopita!
Mkuu Manyimbo,Mkuu Pasco,
Nakushukuru sana kwa darasa yako maridhawa ambayo kamwe sikutegemea kuipata kutoka kwako. Hata hivyo napenda nikiri kuwa kwa hakika nimekwazika na maelezo yako haya:
"Baada ya Karume, Aboud Jumbe akaukwaa urais. Dourado akamjulisha Jumbe kuhusu kukosekana kwan proper ratification na iliyopelekwa UN is fake!, wakaandaa document kuujulisha ulimwengu kuhusu hilo!Seif Sharif akamtonya Nyerere akashughulikiwa ipaswavyo, huku Dourado akaozea jela!.Tukatangaziwa "kuchafuka kwa hali ya hewa Zanzibar" bila kuelezwa kisa ni absence ya proper ratification !."
Naomba sana hapo nilipobold na red unifafanulie kwa uwazi kama ulivyofafanua sehemu nyengine muhimu. Nahisi nahitaji kuelewa kitu fulani kilichojificha ambacho naamini wewe unakifamu kwa nafasi yako. Huyu ni kiongozi wetu wa mpambano huu kuelekea ukombozi wa nchi yetu. Sasa inapotokea kutoa shutuma nzito kama hizi bila ya ufafanuzi unaweza kuleta sintofahamu katika jamii. Na kwa kadri nifahamuvyo mimi, lengo la JF sio kuchochea mifarakano lakini kujenga umoja,mshikamano, democrasia na uwazi kwa dhana ileile ya Freedom of expression.