IsayaMwita
JF-Expert Member
- Mar 9, 2008
- 1,127
- 140
Nyerere bwana, kila akitaka kwenda nje ya nchi lazima taifa lijue, hebu ni kwanini hakwenda kimyakimya? Daa!!!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Siku ya kuagana na aliyekuwa governor wa mwisho nchini Tanganyika Sir Edward Twining, Waziri mkuu Bw. Julius Nyerere alimwambia
Nenda kisha urudi baada ya miaka 10 uje uone maendeleo ya haraka nchi ya Tanganyika itakayokuwa nayo badala ya kuleta maendeleo hasa katika huduma ya tiba hali ilizidi kudorora baada ya siasa zake za kutaifisha. Mwaka 1971 shirika la msamaria mwema lilimaliza hatua ya kwanza ya ujenzi wa hospitali kubwa ya KCMC ambayo ingetoa tiba za aina zote pamoja na kuwepo na madakitari wanaotembea kwa ndege kutibu wagonjwa ambao wako maeneo yasiyofikika kwa barabara. Mwaka huo huo serikali ikataifisha hospitali ya KCMC, hivyo awamu ya pili ya upanuzi ukawa ndiyo mwisho wake. Nyerere afya yake ilipodorora ilibidi apelekwe London kwa matibabu, Bahati mbaya na kwa fedheha alifia kitandani mwa wakoloni mjini London wakati aliwapa wakoloni miaka 10 waje waone maendeleo ya Tanganyika baada ya kupata uhuru na kuwa chini ya utawala wa waafrika. Lakini bado hata sasa viongozi wetu bado wanadumisha fedheha hiyo ya Nyerere kuhenyea matibabu nje ya nchi.
Siku ya kuagana na aliyekuwa governor wa mwisho nchini Tanganyika Sir Edward Twining, Waziri mkuu Bw. Julius Nyerere alimwambia
" Nenda kisha urudi baada ya miaka 10 uje uone maendeleo ya haraka nchi ya Tanganyika itakayokuwa nayo" badala ya kuleta maendeleo hasa katika huduma ya tiba hali ilizidi kudorora baada ya siasa zake za kutaifisha. Mwaka 1971 shirika la msamaria mwema lilimaliza hatua ya kwanza ya ujenzi wa hospitali kubwa ya KCMC ambayo ingetoa tiba za aina zote pamoja na kuwepo na madakitari wanaotembea kwa ndege kutibu wagonjwa ambao wako maeneo yasiyofikika kwa barabara. Mwaka huo huo serikali ikataifisha hospitali ya KCMC, hivyo awamu ya pili ya upanuzi ukawa ndiyo mwisho wake. Nyerere afya yake ilipodorora ilibidi apelekwe London kwa matibabu, Bahati mbaya na kwa fedheha alifia kitandani mwa wakoloni mjini London wakati aliwapa wakoloni miaka 10 waje waone maendeleo ya Tanganyika baada ya kupata uhuru na kuwa chini ya utawala wa waafrika. Lakini bado hata sasa viongozi wetu bado wanadumisha fedheha hiyo ya Nyerere kuhenyea matibabu nje ya nchi.
Heshima kwenu wakubwa,
Ushauri wa vigogo kukimbiziwa nnje kwa ajili ya matibabu huwa unatolewa na madaktari wao ambao pia hutoa recommendations as to which hospital inaweze kuwa na madaktari competent katika ugonjwa husika. Hao madaktari hufanya hivyo kwa kuona ukweli kwamba huduma zetu hapa.. ndio kama vile..kwa hiyo kama ni suala la uzalendo basi lianzie kwa hawa hawa madaktari kutoa ushauri wa vigogo kulazwa Mwaisela, ama Kibasila, wakipata matibabu hapo..kwa njia hiyo tutakuwa tumeonesha uzalendo halisi ikiwa ni pamoja a vigogo hao kufikiria kwa undani zaidi kuboresha huduma za afya nchini, kwa dhana ya kwamba na wao pia wanatibiwa humo humo..basi yapatikane matibabu bora zaidi, na sio bora matibabu..
...jaman hata sisi tutaelekea hukohuko naomba tumhukum mzee wetu kwa mazuri mengi aliyolifanyia taifa letu na sio kwa kujenga hoja kama hizo...???
Tumhukumu kwa mazuri?
Kuna hoja nyingine zimepinda mpaka Kiswahili kinakataa!
Other people bwana! Mada inahusu safari ya Karume London, lakini duh!
mkuu unaanza hata kuchambua typo?
Mwafrika wa Kike, ile siyo typo!
Anasema tumwangalie Nyerere kwa mazuri tu. Lakini hapo hapo anataka kuipa hiyo analysis ka hadhi ka objectivity kwa kuiita hukumu, au kumjudge, au kumu analyze. Lakini amesha funga hiyo analysis kwa kusema tuangalie mazuri tu. Inabidi umsome kwa makini ili umwelewe.
We unafikiri alitaka kusema nini pale kama ni typo?
Kuna hoja nyingine zimepinda mpaka Kiswahili kinakataa!
...Mtoa hoja amepanua duara la thread yake kwa hii sentensi ya pili. Isitoshe, inaonekana hamna mwenye uhakika na hii safari ya Karume. Majadiliano ya sentensi ya kwanza peke yake yatakuwa kwa kweli ni ku speculate. Au nakosea?
Ujumbe wake mzio ulijaa kwenye BA iliyoingia jana hapa London. Tatizo ni kuwa sielewi kaja kufanya nini na kwa manufaa yanani
au
Inawezekana kaja kufanya medical check up maan watawala wetu hawaiamini Muhimbili
Tafadhali kwa khisani yako nakuomba umwache huyu Idrissa kama alivyo.