Kaseba V Cheka

Lussadam

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2007
Posts
1,341
Reaction score
907
Wazee tunaomba matokeo ya pambano la Kaseba na Cheka linalofanyika leo pindi pambano likimalizika
 
duuh mi mwenyewe niko standby hapa nangoja matokeo
 
Yaani matokeo lazima yawe yameshajulikana vipi jamani??
 
kuna mdau toka uwanja wa uhuru ananiambia pambano ndo linaendelea...tulieni hapa hapa ntawapa matokeo
 
Kaseba alizidi kuwa na mdomo sana afadhali kapasuliwa
 
ilikuwa round ya 8 hivi maana kapasuliwa mapka washabiki wakaingilia kwenda kumuokoa..teh teh teh ,,,,kick boxing na mangumi jiwe ni tofauti kaka kaseba
 
Nasikia alipewa za uso......timu yake ikaona so kubwa....aibu, ikabidi waingilie kati kumnusuru....jamaa alikuwa acheke naye haswaaaaaaa....!

BWT: Hivi hizi tabia za kuingilia mapambano zinatupeka wapi wakuu?
 
mkuu Next Level ilikuwa ni soo.Yani Cheka ana ngumi nzito acha kabisa..jamaa kila round alikuwa anangushwa kwa uzito wa makonde
 
halafu cheka na yeye ana minguvu tu ila sio professional yaani kama li nyani tu!bongo tuna safari ndefu!jamaa nimecheki rekodi yake ameshindwa mapambano yote ya nje!kaishia kupiga akina kaseba(rasta) tu!
 
halafu cheka na yeye ana minguvu tu ila sio professional yaani kama li nyani tu!bongo tuna safari ndefu!jamaa nimecheki rekodi yake ameshindwa mapambano yote ya nje!kaishia kupiga akina kaseba(rasta) tu!

sasa mbona ni bingwa wa dunia wa mkanda wa ICB (correct me if i'm wrong) huo ubingwa ameupataje kama amepigwa mapambano yote ya nje?
 
wangeruhusu kutumia pamoja na miguuu, cheka leo angerudi bila uti wa mgongo, au magoti yote yangekuwa mdebwedo. wengi ni maprofesional wa karate, na shaurin kong fu, sana tena, ila ukituambia tutumie za kulenga kwenye uso tu, unakuwa umetuonea, kwasababu kupigana kwa namna hiyo ni kwa kitoto. kick boxing ambayo huchezwa zaidi na watu waliowahi kucheza shotokan karate, na karate inafundisha speical areas za kumdunda mtu. mfano. chembe ya moyo, kwenye maini, na delicate areas nyingi sana. I tell you, if that cheka angekuwa anapigana kama kawaida tu kwa kutumia miguu, jikono,viwiko,visigino etc, ingekuwa kitu hatari sana kwake kwasababu yeye hicho hajasomea. kasema alifanya kitu cha hatari kwake kwa kuacha kile alichosomea ili atumie kile ambacho hakipo kwenye control ya mwili wake akijua anapigana na mtu ambaye yeye emesomea icho tu.

ile kwa kulinganisha, kati ya martial art zote, karate, combut, Tai kondo, kong fu etc, ndo the best of all. ngumi za kulengana uso ni utoto. manake mtu anakuletea mwili mzima na huruhusiwi kumpiga teke, wakati ktk karate etc, mtu akileta mwili kama wanavyoleta maboxer vile, hakika atajikuta amepaishwa na teke hatua mia hivi. na mchezo unaishia hapo. mpiga ngumi hawezi kupigana na watu zaidi ya watano, lakini karate man anaweza kupigana na watu zaidi ya watano peke yake. kwawaulize wachina, wajapan na wakorea.
 
Kwa kweli, mambo yalikuwa mazito kwa Kaseba hasa kuanzia round ya tano. Pambano lilivunjika katika round ya 9 wakati Kaseba akiwa yupo hoi!!! However, it was good timing for him (na wapambe wake), otherwise, it could have been a big shame for Kaseba.

I think Kaseba did not understand the real power of Cheka, alifikiria jinsi round zilivyokuwa zinaenda, then Cheka angechoka, na hivyo ammalize kwa KO, kumbe it was complete vice versa!!!

Hata hivyo, Kaseba alijitahidi, kwani kufika round ya 9 kwa Cheka (given, Kaseba hajapigana boxing for ages) was not easy job.


Let us hope Kaseba will bounce back, kwani na yeye ni mgumu....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…