Kasheshe vituko na vitimbwi vya mimba

Naomba kuuliza wadau hivi ile story ya mwenzetu mmoja rafik yake alivozalishwa hospitalini na dokta wa kiume halafu akamzimia sana dokta hadi akawa analia kua anampenda sana na ilihali ana mme wake ...imekuwaje ??
Mh hii sijaisikia bado hebu nipe link yake
 
Mh hii sijaisikia bado hebu nipe link yake
Ngoja niitafute mkuu....huyo dada ambae ndo best yake huyo mwanamke hakurud kuttupa mrejesho kwamba ilikuwaje. Sasa sjui ndo hizi dalili kuna wakat through pregnancy na kuna zile baada ya kujifungua sjui wanaitaje kitaalamu.
 
Omba sana Mungu mimba ya shemeji isiangukie kwenye kupenda vitu kama hiviutatoboa kibubu nakuapia, ikishanasa tu omba apende vitu vya chukuchuku na achukie nyama choma na roast na tuskeri barrrid sana . ...yani awe mpenzi wa bamia mlenda na ugali wa muhogo daily [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
 
Duu pole sana ni mapito yatapita jipe uvumilivu zaidi
 
Dhu! Jana nimetibuana na mke wangu na ni mjamzito. Kumbe kile kisirani na hasira yawezekana sio kile kiburi chake cha kila siku. Hata kabla ya mimba hua ana kiburi sana. Muda mwingi nashindwa kutofautisha kiburi chake cha asili na kile cha mimba. Nitaisoma namba mwaka huu.
 
Siku shemeji yenu aliniamsha satisa usiku nimpikie chai kisa nlikula embe lake mchana... Nlitaman nimpeleke kwao kwa muda.
Ulitakiwa kwenda kumtafutia embe lenye rangi na ukubwa kama ulilokula. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
mimi nilidhani ubuyu wa instagram!
 
Mi mke wangu alikuwa ananipenda mimi kiasi kwamba hataki niende hata kazini. Na jioni nisiporudi mapema hari. Sku izi ameacha.
 
Mimba acheni tu.....me zinanipa kisirani na hasira za kufa mtu....pia nmetokea kuwachukia Sana wanaume na nnahasira nao balaaaa
[emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji87] [emoji87] [emoji87] [emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…