Mimba ya kwanza nilikuwa nasahau na kupotea njia ya kwenda nyumbani kila siku. nashuka kwenye daladala naanza kujiuliza niende upande gani? Nikiwa naendesha napitiliza au naenda different direction. Ikabidi nipunguze safari na zile za muhimu niende na mtu wa kunikumbusha njia. Cha ajabu sikuwa nasahau vitu vingine.
Mimba ya pili ilikuwa ni kulia all the time, mahali popote muda wowote nilianza kulia bila sababu. Kilio kiliweza last a few min to a few hours. Athubutu mtu kuniuliza nilikuwa nalia nini kilio kilianza upya.
Namba tatu nilikuwa nakula barafu/ ice lollies na chumvi. Muda wowote ule asubuhi, mchana, usiku, barabarani, nyumbani ofisini. Vigari vya azam vilinijua. Au ningegandisha soda sprite au ginger ale nimechanganya na chumvi. Kwa sababu nilikuwa na watoto wengine wadogo ilibidi nijifiche wasinione nikila barafu. Chumbani, kwenye gari, chooni, nje ya fence.